Rais Kikwete amteua Prof. Mussa Assad kuwa CAG mpya akimrithi Ludovic Utoh

Rais Kikwete amteua Prof. Mussa Assad kuwa CAG mpya akimrithi Ludovic Utoh

Hawa ma profesa siwaamini

kweli kabisa mkuu, ma professor wengi ni janga katika kazi za serikali, labda wanafanya vema katika taasisi binafsi.
Mfano :Nani alitegemea kwa CV aliyokuwa Mh. Prof. muhongo , PROFESSOR anna Tibaijuka, PROFESSOR Maghembe, PROFESSOR @Msola , nani alitegemea kuwa watakuja kufanya madudu namna hii.
Kuna mtu alikuwa na CV safi na yenye kuvutia kama Mh. Nundu? peruzi CV yake utaona, ila mwisho wa siku ni aibu tupu.
 
Last edited by a moderator:
Huu uteuzi nina mashaka nao...ngoja niingie chimbo nitarudi!!

Uteuzi uneanza tarehe 5 Nov, umetangazwa tarehe 1 Dec anaapishwa tarehe 2 Dec.(hii trend ya kutufumba macho hakuna ukweli hapa)

Hii ya kuteuliwa tarehe 5 tunafubwa macho tusiringanishe na matokeo ya Report ya CAG kuhusu ESCROW. Maana halisi hapa kwa mtazamo wangu ni kwamba Mwakapalila anawekwa kando kama punishment (indirect) na CAG mpya atake over na kwa msimamo wa Govt kwamba Pesa sio za UMMA atakuja huyu Prof. Asad a-approve kwamba its not public fund. Hiyo ndo itakuwa asante yake kubwa kwa JK, Ccm na Serikali kwa ujumla. Tumeliwa watanzania.
 
Inaonekana atastaafu mwakani kabla hata raisi hajamaliza muda wake, JK ni noma kwa fadhila. Namkemea anayeendekeza mambo ya udini kwa nguvu zangu zote
 
Uttoh amewasaliti wamempiga chini.

By the way Prof Asaad ni 'm'baya' katika uhasibu.
Wadau waliosotea CPA(T) wanamtambua vizuri sana huyu profesa.
 
Historia inaonyesha Maprofessor hawadumu sana katika nafasi za uongozi. They don't make good leaders in Tanzania. Mfano:
- Prof Machunda
- Prof Kapuya
- Prof Meena (Mb)
- Prof Msola
- Prof Muhongo
Endelea
-
-
-
 
Maslahi ya Haifa mbele Kama kawa...kimcngi ninachoamini you can't hide anything mathemsticiali..unless escrow ingezimwa since jikoni
 
Prof Assad Record yake nzuri sana lakini siwezi kujua utendaji wake katika nafasi hii.....hata Prof Muhongo sijawahi kutilia shaka record yake lakini alianza kupata shida tangu alipokuwa Waziri wa Nishati
 
Francis limekuponza hilo jina la kwanza. Ungekuwa Juma au Khamis ungepata...

Profesa Assad ni msomi, mwenye weledi, ujuzi na uzoefu mkubwa wa uhasibu na udhibiti wa fedha ambaye ana Shahada ya Uzamivu wa Uhasibu (PHD in Accounting) kutoka Chuo Kikuu cha Southampton, Uingereza mwaka 2001 na Shahada ya Uzamivu katika Udhibiti wa Fedha (MA in Financial Accounting) kutoka Chuo Kikuu cha Dublin City, Jamhuri ya Ireland mwaka 1991.

Profesa Assad pia ana Stashahada ya Kitaaluma ya Uhasibu (Professional Diploma in Accounting) kutoka Chuo Kikuu cha Dublin City mwaka 1990 na Shahada ya Biashara (Bachelor of Commerce) ya Chuo Kikuu cha Dar Es Salaam mwaka 1988.

Pamoja na uzoefu wa kitaaluma, Profesa Assad anao uzoefu mkubwa katika eneo la uhasibu na ukaguzi. Alikuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Wahasibu na Wakaguzi (NBAA) kwa miaka saba (2007 - 2014); ni Rais na Mjumbe wa Chama cha Wahasibu Afrika (Pan African Federation of Accountants) tangu mwaka 2012; na ni mjumbe wa Bodi kadhaa za Wakurugenzi nchini Tanzania.
 
Historia inaonyesha Maprofessor hawadumu sana katika nafasi za uongozi. They don't make good leaders in Tanzania. Mfano:
- Prof Machunda
- Prof Kapuya
- Prof Meena (Mb)
- Prof Msola
- Prof Muhongo
Endelea
-
-
-
Anna Tibaijuka
 
Nakumbuka Assad alikuwa mwenyekiti wa board ya NBC limited. Je alifanikiwa kivipi au mafanikio yake ni yapi!? Any news kabla hatujasema lolote.
 
Hata Professor Mark Mwandoswa naye ni mzigo tu ndio maana kapewa wizara isiyokua maalum!
 
Hii nchi inatakiwa Dar es Salaam nzima tuandamane... Kuonesha ni kiasi gani wananchi tuna hasira na wizi wao. Tunakua kama wajinga kila siku tunaskia wizi lakni hatujui hatma na muafaka wa hayo matukio. Tusiishie tu kuongea
 
Back
Top Bottom