Rais Kikwete amteua Prof. Mussa Assad kuwa CAG mpya akimrithi Ludovic Utoh

Rais Kikwete amteua Prof. Mussa Assad kuwa CAG mpya akimrithi Ludovic Utoh

maprof ndo wa kwanza kuharibu serikali

Profeza mwingine aliyeharibu kazi ni yule Judge wa mahakama .....nimesahau jina lake aliyepata mgawo wa ishikoro juzi juzi.

Uprofeza ni madarasani tu.
 
Hivi huyu aliyeandika ili tangazo ana-capacity kweli ya kutosha?! angalia level ya degree za mteuliwa - Uzamivu (PHD) badala ya Uzamivu (PhD), halafu Uzamivu (Master's) badala ya Uzamili (Master's). nafikiri hii inaonesha namna gani humo Ikulu watu wasivyokuwa makini.
 
THE UNITED REPUBLIC OF TANZANIA

DIRECTORATE OF PRESIDENTIAL COMMUNICATIONS

PRESIDENT’S OFFICE,
STATE HOUSE,
1 BARACK OBAMA ROAD,
11400 DAR ES SALAAM.
Tanzania.

Telephone: 255-22-2114512, 2116898
E-mail: ikulucommpress@googlemail.com
Website : www.ikulu.go.tz
Fax: 255-22-2113425

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete amemteua Profesa Mussa Juma Assad kuwa Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG).

Taarifa iliyotolewa leo, Jumatatu, Desemba Mosi, 2014 na Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Ombeni Sefue, inasema kuwa uteuzi wa Bwana Assad ulianza Novemba 5, mwaka huu, 2014.

Taarifa hiyo imeongeza kuwa Bwana Assad ataapishwa kesho, Jumanne, Desemba 2, saa nne asubuhi, Ikulu, Dar es Salaam.

Kabla ya uteuzi wake, Bwana Assad alikuwa Profesa Mshiriki, Idara ya Uhasibu, Chuo Kikuu cha Dar es Salaam na anachukua nafasi ya Bwana Ludovick Utouh ambaye amestaafu kwa mujibu wa Sheria za Utumishi wa Umma.

Profesa Assad ni msomi, mwenye weledi, ujuzi na uzoefu mkubwa wa uhasibu na udhibiti wa fedha ambaye ana Shahada ya Uzamivu wa Uhasibu (PHD in Accounting) kutoka Chuo Kikuu cha Southampton, Uingereza mwaka 2001 na Shahada ya Uzamivu katika Udhibiti wa Fedha (MA in Financial Accounting) kutoka Chuo Kikuu cha Dublin City, Jamhuri ya Ireland mwaka 1991.

Profesa Assad pia ana Stashahada ya Kitaaluma ya Uhasibu (Professional Diploma in Accounting) kutoka Chuo Kikuu cha Dublin City mwaka 1990 na Shahada ya Biashara (Bachelor of Commerce) ya Chuo Kikuu cha Dar Es Salaam mwaka 1988.

Pamoja na uzoefu wa kitaaluma, Profesa Assad anao uzoefu mkubwa katika eneo la uhasibu na ukaguzi. Alikuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Wahasibu na Wakaguzi (NBAA) kwa miaka saba (2007 - 2014); ni Rais na Mjumbe wa Chama cha Wahasibu Afrika (Pan African Federation of Accountants) tangu mwaka 2012; na ni mjumbe wa Bodi kadhaa za Wakurugenzi nchini Tanzania.

Katika kumteua Profesa Mussa Juma ASSAD kuwa Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali, Rais anayo imani kubwa kuwa elimu, weledi, ujuzi na uzoefu ambao Profesa Assad anao utamwezesha kutekeleza vema majukumu ya nafasi hiyo muhimu sana katika utawala bora wa nchi yetu.

Imetolewa na:
Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,
Ikulu – Dar es Salaam.
1 Desemba,2014

-----------------------

10313732_648287681948876_6001176764329198945_n.jpg

Hongera Prof Mussa Assad, heko Rais kwa kuteua jembe, professional accountant.
 
THE UNITED REPUBLIC OF TANZANIA

DIRECTORATE OF PRESIDENTIAL COMMUNICATIONS

PRESIDENT'S OFFICE,

Huyu mwalimu wangu wa accounting 101 yuko sawa ila apunguze slang utafikiri muhuni wa brooklyn au bronx.
 
Yule kaimu ESCROW imemponza. Yeye kaibua mambo mazito alifikiri atapandishwa cheo! Thubutu...!
 
Uteuzi uneanza tarehe 5 Nov, umetangazwa tarehe 1 Dec anaapishwa tarehe 2 Dec.(hii trend ya kutufumba macho hakuna ukweli hapa)

Hii ya kuteuliwa tarehe 5 tunafubwa macho tusiringanishe na matokeo ya Report ya CAG kuhusu ESCROW. Maana halisi hapa kwa mtazamo wangu ni kwamba Mwakapalila anawekwa kando kama punishment (indirect) na CAG mpya atake over na kwa msimamo wa Govt kwamba Pesa sio za UMMA atakuja huyu Prof. Asad a-approve kwamba its not public fund. Hiyo ndo itakuwa asante yake kubwa kwa JK, Ccm na Serikali kwa ujumla. Tumeliwa watanzania.

Hata mimi ndo ninavyoona. Wakati anatoa tamko la escrow Kikwete atasema "sasa tumempata nguli wa mahesabu. kwahiyo tunategemea atupatia jibu kama pesa za escrow ni za umma au la". Na amemchukua mwenye CV kubwa ili watu wasihoji majibu atakayotoa. mtakumbuka aliyeteuliwa kupitia mitihani ya kidato cha nne na baadae kulazimisha standardization. Hawa wataalamu anajua kuwapa post na baadae wanakuja kudhaulika kwa kufanya tofauti na maadili ya taaluma zao. ngoja tuone. Yangu macho.
 
Utoh aliweza sana... Hope Prof Assad hatatuangusha ... I wish him nothing but success kwa maslahi mapana ya Watanzania...
 
Really? Hivi udini maana yake ni nini haswa? Tuseme Waislam hawapaswi kuteuliwa japo kama wana sifa za kutosha?. Haya lete comparison yako na Prof Assad kwenye accounting and auditing field. Halafu uteuzi wa Assad unatofautiana vipi na ule wa Utouh?
Let you talk sense. Prof Assad ana deserve hiyo position labda tu haderserve kwa sababu ni Mwislam. Lakini tukienda kwa mwenendo huu ndugu mmmm sidhani kama tuna mwisho mwema.

nafikiri watu wengi wanachukulia ucha mungu kama udini kitu ambacho ni uongo. Hakuna hata mmoja hapa amaeleza udini alio nao. Watu ni kusema udini bila kuwa specific. Kwani pale mlimani alifelisha wakristo na kupasisha waislamu? tuaanzie hapo kwani ndo kazi amekuwa akifanya.
 
Wataalam wa hii kitu mnijuze,Hivi nini mantiki ya hizi teuzi kusema uteuzi wake umeanza toka Nov 5 wakati taarifa imetoka leo na hajaapa bado!?. Je, na mshahara wake unaanzia hiyo Nov 5!?
 
Angemuacha tu yule jembe utoh amsaidie kuimaliz hii ngwe yake katika majembe huyu ni mmoja wapo tatizo la hii nchi ukiwa mchapa kazi na mkweli huwa watu wanatamani hata ukafie mbali hata ushuda wasitoe ila kwa huyu bora angemeimba amsukumie gurudumu mpaka mwisho
 
Utoh aliweza sana... Hope Prof Assad hatatuangusha ... I wish him nothing but success kwa maslahi mapana ya Watanzania...
Wewe unasumbuliwa na chuki na roho ya husda tu.
 
Back
Top Bottom