Rais Kikwete atangaza nia ya kuanza kwa Ujenzi wa Reli ya Kati kwa kiwango cha Kimataifa (SGR)

SGR
 
Watu wameshafukua makaburi..kuna uzi humu wa 2013..Ni kweli kabisa hicho alichokisema.
 
Anaweka rekodi sawa tu
 
2013 to date ni 10 years
 
Unavyosema pesa zilikuwa hakuna vipi kuhusu upigwaji wa Escow, meremeta, utorowoshaji wa mali zetu asili kama tembo nk, tulisainishwa mikataba mibovu mfano kufaidika na madini kwa 3% tena ni madina yetu, matumizi mabaya ya fedha za umma yote haya yalikuwa kipindi chake. JK hakuwa mtendaji mzuri, siwezi kukataa kwamba inaweza akawa amechangia kwenye ideas kwenye projects but tunamuhukumu kwa sababu hakuwa mtendaji wala msimamizi mzuri na ndio maana ufisadi ulidominate sana kipindi cha utawala wake na wala hakuwa na action zozote zilizochukuliwa hatua.
 
Mkuu, habari za siku?
 
Alikuwa mzee wa michakato tupu, nchi ilipata hasara sana kuwa na huyu uongozini
 
umesahau bwawa la nyerere alipoenda kuwashwawashwa pembeni yake. si alete na mada motomoto kama alivyoponea tundu la choo 2010
 
Mkuu, kwani akiongea anakutekenya? Au unakwaruzika? As long as yupo hai muache aongee. Wajibu wako wewe ni kusikiliza anachokiongea kwa umakini utajifunza na kujua mengi.
Akiongea vitu visivyo vya kweli na Wananchi wanajua kuwa anasema uongo sio vizuri...inamwondolea Busara, na hali ya kuaminiwa kwa yote atakayosema
 
Watu wamemshambulia juzi Kati aliposema mchakato ulianza na Mkapa ukaendelea awamu yake na Magufuli akaanza utekelezaji.
Wakasema yeye mpenda sifa kumbe mzee Jakaya Kikwete kaongea ukweli.
Mnyonge mnyongeni lakini haki yake mpeni.
Uzuri wa Kikwete hana shida na kelele za watu.
 
Ametukumbusha, kuna watu wameanzisha hadi uzi eti mzee akae kimya. Sasa atakaae kimya wakati na yeye alikuwa sehemu ya hii mipango ambayo tunaona matunda yake.

Mzee wa msoga udumu sana.
 
Mbona ameongea alichokianzisha, mwenyewe na anaona fahar kimetumia na amekishuhudia kama hajaondoka katika uso wa Dunia, kila mtu anapenda kuona kile anachoweza kinatimia hata sio yeye atakitimiza
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…