Rais Kikwete atangaza nia ya kuanza kwa Ujenzi wa Reli ya Kati kwa kiwango cha Kimataifa (SGR)


Umefata link hiyo kuisoma au unakurupuka tu?

Canarail reveals Tanzania-Rwanda railway construction underway
 
Wajapan wakasema wanakuja kujenga.
Ghafla Pinda akiwa China kapata mchukua tenda. !!!
 

Mkuu Joka,
Hili tangazo la Kikwete, ni la kujaribu tu kuondoa aibu (pre-emptive strike) kwa vile walivyo-umbuliwa na CoW kuwa wao ndio wazembe kwenye EAC, maana Kenya watatangaza kuanza ujenzi hivi karibuni wakati TZ hakuna kinachoendelea.

Viongozi wetu wamekuwa wazuri sana katika kushugulikia miradi yao binafsi na kuwatupia porojo waTZ bila utendaji au uwajibikaji. Ukichunguza utaona wote wana mabadiliko makubwa binafsi ya kiuchumi tokea walipoingia madarakani lakini miradi ya taifa hawana uchungu nayo, unless wawe na 10% zao au kuwa na vikampuni vyao vishiriki kwenye hiyo miradi.

  1. Reli ni muhimu kwa kuendeleza uchumi, je JK amefanya nini kuiimarisha licha ya kuwa kwenye uongozi kwa zaidi ya miaka 10?
  2. Umeme na hakuna wa uhakika na ni ghali, kwa nini mtu aanzishe kiwanda TZ badala ya Kenya, Msumbiji au SA kwenye uhakika wa umeme rahisi? Ina maana hawalijui hili?
  3. Tumeshindwa kufufua ATC; hivi sasa Kenya, Ethiopia, SA na sasa Rwanda ndio tunaowategemea kubeba mizigo na wafanyabiashara wetu, kwanini?
  4. Kwa nini Kenya wawe na bandari bora kuliko sisi ingawa tuna ufukwe mrefu zaidi? Haka ka-Container terminal tulikonako kamemfanya Rostam Aziz awe bilionaire, je taifa lingefaidikaje kwa kiasi gani kama tungekuwa wamiliki wa bandari nzuri zenye uhakika?
  5. Kwanini ichukue miaka 30-40 kujenga barabara muhimu kwa uchumi wa nchi? i.e. Barabara za kuunganisha bandari zetu na Msumbiji, Malawi, Zambia, DRC, Burundi, Rwanda, Uganda na Kenya zote ni mbaya.
Haya yote yanawezekana na yangefanyiwa kazi kwa haraka muda mrefu nchi ingekuwa mbali sana, kwani siyo magumu bali uzembe na usanii tu ndio umewatawala viongozi wetu.

Kuboreshwa kwa hii miundo mbinu kungeongeza ajira kwa waTZ, maendeleo binafsi ya waTZ, ongezeko la kodi kwa serikali, ongezeko la utalii, ubora wa maisha n.k. Lakini kwa vile serikali yetu haiwajibiki kwa wananchi, ndio maana wanafanya kazi tu kuondoa aibu na sio kujenga nchi.
 

Wewe wacha porojo, kabla ya kushika uongozi Kikwete hata kwenda Mwanza kutokea Dar ilikuwa mpaka tupiptie Kenya. barabara nyang'a nyang'a toka wakati wa Nyerere. Leo unakwenda huku unakunywa gahwa ndani ya gari, hulijui hilo?

Miradi ya barabara Tanzania wakati huu ni mingi kuliko nchi yoyote ya Afrika chini ya Sahara.

Bandari usifikiri ni lelemama ile, usaini mkataba leo kesho uanze kujenga, kuna watu wa kuwahamisha, kuna miundo mbinu ya kutayarishwa, kuna logistics za kutayarishwa, kuna vifaa vya kukusanywa nje na ndani ya nchi, kuna upimaji wa kina cha maji, kuna upimaji wa udongo uliopo nje na na baharini kuna kila namna ya matayarisho (mobilization), na kwa mradi mkubwa haya matayarisho pekee huchukuwa si chini ya miaka miwili. Usifikiri kuna kucheza mdako pale.

Hivi hizo shule mlienda kufutwa ujinga au kujazwa ujinga?
 
Wajapan wakasema wanakuja kujenga.
Ghafla Pinda akiwa China kapata mchukua tenda. !!!

..hilo nilikuwa nimeliweka kiporo.

..sasa Mjapani kasema tuendelee na reli hii hii hakuna kuweka standard gauge.

..wanadai huko kwao wanatumia reli ya gauge kama yetu lakini more efficiently.

..tukienda kwa Mchina tunaambiwa hivi. Tukirudi kwa Mjapani tunapewa ushauri mpya.

..Wajapani wamesema watatuma wataalamu wao kufanya feasibility study. kwa hiyo hii ngoma ina miaka mingine miwili zaidi.

CC Kubwajinga
 
Last edited by a moderator:


..tulitakiwa tuongoze na kwenye miradi ya reli pia.

..wenzetu walishatoka kwenye miradi ya barabara, wako kwenye reli na bandari.

..tangu tutangaziwe "nia" kuhusu bandari ya Bagamoyo is enough time kuwa ktk phase ya ujenzi sasa hivi.
 

Miscommunication kati ya mbwa na mfuga mbwa
 

Mkuu Joka,
Baya zaidi ni kuwa hakuna ratiba ya utendaji wa hii miradi na pia hakuna utaratibu wa bunge kufuatilia yanayodiri kuhusiana na miradi ya maendeleo. Kwa nini tusiweke wazi habari za kila mradi, unatarajiwa kuanza lini, pesa yake inategemewa kupatikanaje na taratibu za tenda ni zipi? Kwa nini tusiwajibishe au kufikisha mahakamani watumishi wanaozorotesha/ kuhujumu miradi ya taifa? Kama hatutabadilika, tutaendelea kuwa nyuma ya wenzetu licha ya rasilimali nyingi tulizo nazo.
 
..tulitakiwa tuongoze na kwenye miradi ya reli pia.

..wenzetu walishatoka kwenye miradi ya barabara, wako kwenye reli na bandari.

..tangu tutangaziwe "nia" kuhusu bandari ya Bagamoyo is enough time kuwa ktk phase ya ujenzi sasa hivi.

Bado hujaisoma link niliyokuwekea, au lugha ya watu inakupiga chenga? Tatizo la magwanda wengi kama wewe ni kujidai unajuwa kila kitu kumbe huna ulijuwalo.

Ukiongelea kutoka, watu walianza na reli ndio wakaja na barabara na sasa hivi wanaenda kwenye Mars. Wewe bado umelala usingizi mzito.

Na hiyo kazi ya reli inayofanyika wewe nna-uhakika huwezi iona kwani bado upo kwenye usingizi mzito kabisa.
 
Watu hawaoni aibu kuendelea kuahidi hata kama kuna mengi yamewashinda kuyatekeleza. Don't promise that which you can't fulfill!
 
[B FaizaFoxy,

..OK, nime-copy taarifa toka link uliyoileta.

..nadhani kichwa cha habari ni kwa ajili ya kuvutia wasomaji.

..JK bado yuko katika hatua ya kutangaza "nia" ya kujenga.

..Wajapani wanadai tubakie na gauge iliyopo mpaka 2030 na wataleta wataalamu wa feasibility study.

..in the middle of the article unayonitaka niisome, mwandishi anadai nchi washirika wa mradi watafute funds ili ujenzi uweze kuanza.

..majuzi napo Rwanda wamechomoka na kuachana na mradi wetu, sasa wanataka kujenga reli kuelekea Uganda na Kenya.

..sasa hebu tueleze tufuate kipi hapa?!!

[/B]


cc FaizaFoxy
 
Last edited by a moderator:
Watu hawaoni aibu kuendelea kuahidi hata kama kuna mengi yamewashinda kuyatekeleza. Don't promise that which you can't fulfill!

Watu wameahidi ndani ya katiba yao kuwa wataongoza kwa muda usiozidi miaka 10 na kwa utamu wa madaraka na fedha za ruzuku wakaamuwa kubadili kinyemela kifungu cha katiba kukifanya kiwe hakina ukomo. Umesahau mara hii? au hujui kasheshe linaloendelea kwa sasa kwa magwanda ni la nini?
 

Mkuu Salary Slip ,bado tunaendelea na ahadi tu kwa wananchi hivi zile ahadi za za uchaguzi tumeisha zimaliza au hazitekelezeki hivyo tunaanza Mpya.Wahusika wamkumbushe Mkuu kwamba amebakiza miezi kama 24 tu aondoke madarakani apunguze ahadi afanye utekeleza hata akishindwa basi ajitahidi atuachie Katiba Bora inaweza ikafunika siyo kuondosha udhaifu mwingi wa Utawala wake
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…