Rais Kikwete atangaza nia ya kuanza kwa Ujenzi wa Reli ya Kati kwa kiwango cha Kimataifa (SGR)

Rais Kikwete atangaza nia ya kuanza kwa Ujenzi wa Reli ya Kati kwa kiwango cha Kimataifa (SGR)

Anataka aonekane na yeye kama amejenga wakati ukweli hakuna alichokifanya zaidi ya kusafiri kwenda ulaya kubembea na mke wake kwenye nursery school za marekani na kuenda kufanya upasuaji wa tezi dume.kwenye sgr kikwete hakuwa na mpango huo Bali yeye alipendekeza ijengwe gari Moshi la kizamani la diseli na akashindwa kutekeleza hata nusu kilomita zaidi ya maneno tupu.Na kituko kingine alichopendekeza eti kununua mabasi ya kutembea kwenye maji sijui wangepanda watu wa wapi na kwenda wapi!Ni Bora anyamaze maana kipindi chake Nchi aliifisadi sana kama Yale ya sakata la IPTL,meremeta,gesi ya mtwara kuwa na mkataba tata,n.k

Rais Kikwete atangaza nia ya kuanza kwa Ujenzi wa Kimataifa wa Reli ya Kati.​

Soma huo uzi 2013.. acheni kumbeza mzee wetu.
 
Mbona ameongea alichokianzisha, mwenyewe na anaona fahar kimetumia na amekishuhudia kama hajaondoka katika uso wa Dunia, kila mtu anapenda kuona kile anachoweza kinatimia hata sio yeye atakitimiza
Mwenyewe kasema alianzisha Mkapa, yeye kaendeleza mchakato.
Kila kitu kikubwa au kizuri ili kifanikiwe kikamilike lazima kipitie michakato (processes).
 
Kila project kubwa atakuambia ana mchango. Alitoa maagizo akiwa anaondoka madarakani ifanyike. Alianza na uhamisho wa Makao Makuu Dodoma. Akasema ana mkono wake. Wakati tunajua mikono yake ilikuwa kwenye projects nyingi za kifisadi.

Hii SGR anakuambia ilianzishwa na Mkapa yeye sijui akafanya nini then akamwambia Magufuli ajenge. Yaani hata hajielewi.

Kwanini asinyamaze aonekane ana busara? Kwani ni lazima naye aongee aongee? Au umri nao ni tatizo? Amwache Samia afanye kazi bila naye kujichomekq chomeka.

Kwa nini asinyamaze? Au yeye hapendi kuonekana ana busara?
Ni misifa kwa kwenda mbele, watz wanajua nani shujaa wa taifa hili, hayupo lakin kazi zake twaziona vema, miradi ya shujaa haihitaji filters ili iinekane ku shine
 
Anajaribu kusawazisha Ili tuache kuaminishana ujinga!

Miradi yote migumu sana alipewa chuma kutokana na haiba yake ya uchuma na kutoyumbishwa!

Yes aliahidi maisha Bora kwa kila Mtz asingeanzisha hiyo miradi coz ingembana kutekeleza ilani yake ya maisha Bora Kwa Kila mtz!!

Tujaribu kufikiri katika nyuso tofauti sana kauli za viongozi!!
 
JK kasema baada ya kukamilisha ujenzi wa barabara sasa mkazo ni ujenzi wa reli ya kisasa(SGR).
 
Technology bana watoto walikuwa bado hawajazaliwa wakatiki anaongea thus akaja kukurupuka na uzi huu, kuwa makini unapoandika
Mzee kikwete alifanya mambo mengi saana na yy ndo alimwambia Magu agombee na jk ndo founder wa makonda watchout bro
 
Rais Kikwete ametangaza nia ya kuanza kwa ujenzi wa Reli ya Kati kwa kiwango cha kimataifa. Rais amesema reli nyembamba inapatikana eneo la Afrika Mashariki tu.

Mh. Rais kayasema hayo mkoani Simuyi wakati akiweka jiwe la msingi kuzindua ujenzi wa barabara itakayounganisha mkoa wa Simiyu na mikoa ya jirani.

View: https://youtu.be/CAe_1eN8VAM?si=V_nFyEigpZq3r2_u

CHANZO: ITV

MY TAKE:
Hivi hizi ahadi zinatekelezeka kweli??!!

Aiseeee
 
Kwahiyo leo mimi nikitangaza nitajenga daraja la kutoka Magogo mpaka Zanzibar nakuwa namaanisha au ni usanii?
 
..mkataba wa bandari ya Bagamoyo ulisainiwa wakati Raisi wa China ametembelea Tz.

..sasa tangu wakati Raisi wa China amekuja hapa ni muda gani?

..majuzi PM Pinda alikuwa China anazungumzia bandari ya Mtwara.

..hawa watu wako very efficient ktk kusafiri tu, lakini ni zero kwenye kufanya kitu kikaonekana.

..tukubali ukweli kwamba JK na serikali yake wako too slow, na ndiyo maana nikatoa mfano wa Raisi Uhuru Kenyatta.
Uliona mbali sn
 
Watu wamemshambulia juzi Kati aliposema mchakato ulianza na Mkapa ukaendelea awamu yake na Magufuli akaanza utekelezaji.
Wakasema yeye mpenda sifa kumbe mzee Jakaya Kikwete kaongea ukweli.
Mnyonge mnyongeni lakini haki yake mpeni.
Uzuri wa Kikwete hana shida na kelele za watu.
Hata mm imeniuma sana baada ya kuuina uzi huu wenye ushahidi wa aliyoyasema juzi. Watu wametokwa na povu kama lote, lkn kumbe alichokisema ndiyo ukweli wenyewe.

Kikwete huwa ni mkweli sana huyu mzee, Mungu ampe maisha marefu
 
Watu husifiwa kwa mambo waliyotekeleza, sio waliyopanga au kuacha katika makaratasi, Elon Musk anajulikana kama yeye ndio kila kitu Tesla wakati alinunua. hakuna mtu anayekumbuka tena hata majina tu ya hao ambao kampuni ilichukuliwa kutoka mikononi mwao.
Wewe ni mwongo. Kwa kauli yako unajuwa kuwa Elon Musk alinunua kampuni kwa watu wengine, halafu unasema hakuna mtu anakumbuka majina yao wakati wewe mwenyewe inajuwa. Contradiction
 
Hata mm imeniuma sana baada ya kuuina uzi huu wenye ushahidi wa aliyoyasema juzi. Watu wametokwa na povu kama lote, lkn kumbe alichokisema ndiyo ukweli wenyewe.

Kikwete huwa ni mkweli sana huyu mzee, Mungu ampe maisha marefu
Hata mimi kwa kweli imeniuma sana.
Sema ndo hivyo watu wakishakuchukia, hata ukisema ukweli lazima watautilia shaka.
 
Back
Top Bottom