Rais Kikwete Bado Anatusubiri Tukamwone



Asante Mkuu Kasheshe . . . Now you are talking . . .
 

Nimekupata Mkuu, maoni yako ni mazuri.

Je hili linaweza kuingizwa katika TUZO YA MTANZANIA ALIYEFANYA VIZURI?
Tafadhali angalia thread hii . . . https://www.jamiiforums.com/showthread.php?t=16002
 

Njimba, umegusia kitu ambacho ni muhimu sana. Ni vema sasa ibuniwe mikakati ya kuwapa meno hawa Auditors au watu wengine watakaogundua maovu bila kuogopa wala kuwa na wasiwasi na kitu au mtu yeyote.

Kuna dada yetu Vicky Mtetema wa BBC ambaye alifanya coverage nzuri sana juu ya mauaji ya Maalbino lakini mpaka sasa hajapewa ulinzi wowote pamoja na vitisho vya kuuwawa anavyovipata. Nadhani masuala yote haya inabidi yaangaliwe kwa makini.
 

Duu! Mkuu, hiyo Creativity yako ni kali sana. Inabidi tufanye consultation na research fulani kuangaalia possibilities zinazoweza kuwepo. Ila kama kutakuwa na uwezekano huo, basi itaboost morale wa wahusika kwa kiaasi kikubwa.

Suala la security yao na maslahi inabidi pia liangaliwe sana.
 

Duu! Mzalendo Mtanzania, umenifanya nibaki mdomo wazi kwa simulizi yako. Ama hakika inatakiwa ifanyike kazi ya ziada kuleta mabadiliko, vinginevyo itachukua muda mrefu sana kuweza kuleta mafanikio ya kweli.

Nadhani hicho chama kingine unachokitungumzia ni Tanzania National Business Council (TNBC).

Nimependa hiyo paragraph yako ya mwisho hapo juu. . . kama ni kweli mlihangaika hivyo, basi ni vema tujihesabu kuwa hatuna wazazi wa kutusaidia pamoja na kuwa na jitihada za dhati ya kujikomboa zilizohitaji msaada wa wazazi.

Unanikumbusha mbali sana. Nilikuwa na project yangu iliyokuwa inahitaji TIC Certificate nadhani 2005, ilinichukua miezi kadhaa kuipata, na baada ya hapo nikaanza kupambana na TRA ambako huko ndo usiseme, kidogo nikate tamaa. Kilichonisaidia ni kutokukubali kukata tamaa na kuendelea kufuatilia katika kila ngazi na hatimye nikafanikiwa kupata msamaha kwa baadhi ya vitu tu. Wakati huo hata pesa niliyobudget ikawa imepungua na gharama zingine zimeenda juu. Na hata charges za bandarini za storage nazo zikawa ziko juu sana kwa sababu ya muda mrefu kupita.

Ndugu zangu, mimi nadhani tujipange na kujiunda vizuri ili tujisaidie wenyewe. Tutakwenda kumwona rasmi Mh. Rais na kumwandikia ili kutimiza wajibu wetu kutokana na ahadi yake ili kuweka kumbukumbu sahihi ya nini tulifanya baada ya yeye kutoa ile ahadi yake. Na tunapoandika nitapenda hiyo resolution itiwe saini na wanataaluma wengi kuonyesha seriousness na ukubwa wa tatizo.

Kweli tunahitaji kazi ya ziada kuweza kusonga mbele. Natoa mwito tusikate tamaa.
 

Mtanzania, TPN iliwahi kufuatilia suala la BOT guarantee ili tuone ni vipi ingeweza kusaidia kupata mikopo. Tuliambiwa hiyo guarantee inatolewa kwa mikopo ya nadhani mpaka TZS 350 Million. BoT wanacover 50% Security na nyingine unacover mwenyewe. BoT wanasema hiyo pesa inatolewa na Ministry of Finance ili wao wai-manage na inatakiwa kuwekwa katika budget ya Serikali.

Kuna mabenki ambayo BoT imeingia nayo mkataba wa kuweza kutumia hiyo Guarantee facility, lakini inaonekana ni mambo ya kwenye makaratasi tu kwani mabenk mengi hawaitumii isipokuwa kwa benki chache sana ambazo nazo pia hazipendelei sana mpango huu.

Pamoja na hayo yote nimeambiwa kuna maombi mengi sana ambayo yako pending BoT kutoka katika hizo bank chache na BoT kwa sasa hawana pesa yoyote toka serikalini. Inaonekana hiyo Guarantee ilitengewa budget kidogo sana ambayo hata hivyo imekwisha.

Ndugu zangu, ni bora kubuni mfumo wetu wenyewe kama kuanzisha TPN Fund, Venture Capital Fund au Investment Fund etc. I believe tukiunganisha nguvu kwa maelfu, we can start making little difference. Let us try that way.

Sometimes the road to success is very rough and hard.
 

Nimekusoma Mkuu, tutatilia maanani ushauri wako. Kama una specific issues pia unaweza ukashare ili nazo zifanyiwe kazi.
 
mimi nafikiri inawezekana maana wanahitajika wasomi wabunifu,Na sio wasomi wapiga desa kwi kwi kwi utani

Mkamap, umesoma lakini post ya Mtanzania? Do u think they never had a good project? Soma tena maelezo yake. I think walijitahidi sana.
 

Wakuu, naona hapa mnazungumza mambo ya Kitaaluma kidogo. Kama mnafikiri this could be a Feasible Project, ileteni TPN ifanyiwe kazi. . . . People can then see how we can move forward.
 


Mkuu, nikipata muda mzuri nitakutumia PM.
 

Mkuu, nitakutafuta pia kwenye PM. Nataka nipate mawazo yenu ili kuandaa mazungumzo na hata masuala ya kiutendaji.
 
Ninataka kuanzisha huduma ya tiba ya moyo. Nina ujuzi wa kimataifa lakini mtaji wangu si mkubwa sana, hata hivyo nina washirika kitaaluma na kimtaji kutoka ujerumani na marekani ambao ni mahiri sana katika nyanja hii. Ninachoomba ni ushirikiano na serikali yako kuwa inisadie katika maswala ya mikataba ya kuwaleta washirika wangu hao wanapohitajika, na vile bvile niwe ninapewa nafasi ya kuhudumia wagonjwa wa moyo kabla serikali haijawapeleka nchi za nje. Kulingana na maadili ya taaluma yangu, sitalazimisha kutibu mgonjwa ambaye anahitaji huduma ambayo siwezi kutoa.
 

........huo ugomvi unaotaka kuuanzisha sijui kama utauweza.....lol
 
Mkuu, LOL unaelekea kama unamsemea Dr. Masu wa THI . . . LOL.

Inavutia sana kwa issue kama hii ikiwa moja ya ajenda ya kuongelea huku tukiwa na facts zote. Si hivyo tu kwa maoni yangu ni wakati muafaka sasa kuwa na Sera Mahsusi ambazo zitawasaidia kwa makusudi Wanataaluma wetu ambao wana nia ya dhati ya kutumia taaluma zao kuondoka matatizo ya watu au kuleta maendeleo. Of course haya yote ni vema yafanyike katika mchanganuo ambao utaonyesha wazi kuwa hatimaye Project hiyo/hizo zitajiendesha yenyewe.
 

Sio nataka kuanzisha...nilishaanzisha na nimeshakula vichwa kadhaa.
Pia nimekula NSSF contributions za wafanyakazi wangu.

...halafu ongezea na hii:

"Vile vile kwa kuwa mimi ni Mtanzania, ningeomba ushindani wa soko huru usiwe applied kwangu. Kuna wabaya wangu wanataka kuwaleta Apollo Hospital ambao wako mbali katika quality na organization. Naomba MONOPOLY katika sekta hii.

Sijafanya feasibility study kabla ya kuchukua msaada wa vifaa kutoka nje. Ningeweza kabisa kurudi MUCHS nilipokuwa mwanzo na vyombo hivi vingekuwa huko LAKINI bahati nzuri niliporudi nilipata fala mmoja akanikodishia nyumba yake. Sijamlipa kodi hata siku moja na nilihakikisha ndoto yangu ya kuwa na hospitali yangu inatumia MGONGO wake kisawasawa!

Baadaye jamaa alifungua kesi, lakini nilijua kesi ya madai haiuwi na kwa kuwa alikuwa na asili ya kiarabu haikuwa kazi kumzungusha na mahakama zetu njaa.

Mungu si Athumani, NSSF nao wakajilengesha. Nimewapiga bao la tiktak lakini beki wao, Ramadhani Dau ametoka kujaribu kurudisha hili bao. Nilifanikiwa kupata wachezaji wa kulipwa kutoka USA na kwingineko akiwepo Mganga wa timu Mtikila ambao wanafanya vitu vyao.

So far upepo sio mbaya...kesi Tanzania inasukuma siku ziende...HALLELUJAH!
 


Kichuguu & Others,
Nadhani kabla ya kuendelea kuchangia please ninawaomba muingie hapa

http://www.coping.org/write/percept/fallacies/content.htm#Missing

Nina amini baada ya kupitia hapo hali ya uchangiaji katika thread hii itaimarika.

Mtsimbe usichoke, kawaida mwanzo ni mgumu na niimani yangu kuwa baada ya muda sio mrefu thread hii itabakia na watu wachache huenda wasizidi watatu. Wengi wetu humu ni makada wa Chama fulani na kazi yetu kila siku ni kufuatilia tuiseme vipi serikali na kawaida hatupendi hata kuangalia ukweli, sisi tunaangalia nani!!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…