MkamaP,
Unaloliona wewe ni tatizo mtu mwingine anaweza asilione kama ni tatizo.
Pia aukitegemea rais atoe pesa ni kujisumbua bure.
Kinachotakiwa hapa ni change, systematic change ambayo ikifanyika ndio itaweza kuzaa wabunifu kwenye nyanja mbalimbali.
Ubunifu hautokei kwenye jangwa, innovation yoyote inatokana na watu na society ambayo imejengwa mazingira ya innovation kuzaliwa na kukua.
Kwa Tanzania ninayoiona mimi leo sahau innovation kama hatutashughulikia hayo mambo niliyoyaandika hapo juu.
Invention yoyote mpaka ifikie level ya innovation jua imeshakula pesa kibao na kama
hatuna jinsi ya kufund hizo activities, sahau kabisa?
Umeongelea umeme wa wireless, why bother na huo umeme wakati kuna solar power? Je ni kwanini solar power inashindwa kuongezeka TZ? Tatizo ni hilo hilo.
Pia watu wengine wanafikiri ubunifu ni kutoa product, ubunifu unaweza kutokea hata kwenye services, in fact western world sasa innovation zao nyingi ni kwenye process na wala sio products.
Akija mtu akatengeneza system ya kuondoa usumbufu wa TRA inaweza kuwa innovation nzuri kuliko hata kutengeneza product.
Wachina sasa wana copy kila kitu na wanaenda mbele. Dunia hii imejaa technologies mbalimbali na inatosha ku copy unachotaka na kukifanyia mabadiliko. Huawei Technolgies leo wanatamba duniani lakini ukiangalia product yao ya kwanza upande wa switching ilikuwa copy right na Lucent Technologies wakati upande wa data waliiga Cisco.
Hivyo ninachoona mimi ni kwamba rais anaweza kusaidia kubadili system ili ijenge mazingira ya wabunifu wa aina zote bila kuchagua. Huwezi kuona umuhimu wa jambo mpaka siku mamilioni wanafaidika. Mfano mzuri ni google, wakati wanaanza bank zote ziliwanyima pesa, lakini leo sidhani kuna mtu ambaye hajutii kwanini hakutoa pesa au hakununua shares zao mapema.
Kama kutunza viazi mbona kwetu kule miaka ya zamani walikuwa wanafanya hivyo? Walikuwa wanafukia viazi chini na vinadumu karibu mpaka msimu mwingine. Nilienda Sweden nikakuta na wenyewe kule vijijini wanatumia njia hiyo hiyo. Tatizo kwasasa huenda ni uzalishaji, kama huzalishi viazi vya kutosha na kuna demand ya viazi hivyo mjini, matokeo yake ni kuuza vyote. Kutunza viazi inatakiwa isiwe kazi ngumu kabisa.