Rais Kikwete Bado Anatusubiri Tukamwone

Rais Kikwete Bado Anatusubiri Tukamwone

Mtsimbe,

Nadhani Rais atafurahi kukuona/kuwaona... ikiwa mkifika pale mtakuwa mumeonyesha mangapi mumekukuruka wenyewe mkayafanyia kazi!.

In short lazima muuende na nondo zilizoandikwa munazoziamini in addition 2 maneno mtakayoongea wakati mkinywa kahawa na Mh. Rais.

Vizuri ni kuwa na moyo... kwa kuwa mawazo mengi utakayoyapata hapa uchuje vizuri sana.. maana kuna watu hawajui Tanzania ya sasa iko je lakini kwa bahati mbaya wao ndio wachangiaji wakuu...

Ukiangalia hotuba ya mheshimiwa rais imesema makundi ya wataalaamu... haikusema mtu mmoja mmoja and surely you are in the right direction.

Wazo Langu kwa Mh. Rais hilo hapo chini... ninayo mengi lakini nadhani nitawaachia wengine nao waseme.


Asante Mkuu Kasheshe . . . Now you are talking . . .
 
Ili kuhakikisha huduma kwa wananchi zinaimarika na ili kuhakikisha fedha zetu zinatumika vizuri, na ili kuhakikisha kazi zinazofanyika zinafanyika kwa kiwango cha hali ya juu sana. Nashauri yafuatayo.

1. Kuwepo na mashindano ya ubora wa huduma, ubunifu ambao unakuwa aidha unalisaidia taifa kwa kuokoa fedha nyingi... au kwa kuwapa wananchi wengi huduma zaidi bila kutumia rocket science. Nia ya hii ni kuhakikisha proffesional boards zitoe mfano engineer ambaye ataoa design ya barabara ambayo ni cheaper kufanya yetu inaweza saidia tatizo la foleni kwa Dar es Salaam... huu ni mfano tu.

2. Washindi wanaweza kutoka kwenye proffesional boards mbalimbali, mfano kutoka kwa madaktari, wahandisi,wauguzi,wahasibu, wanaICT etc.

3. Washindi wapewe recognition (nishani ya Rais wa Jamhuri iliyotukuka au hata nishani ya Jamhuri) na zawaidi kwenye sherehe aidha za Mashujaa ya za Jamhuri.

4. Washindi waweze ku-reclaim tax for say 5 years kwa matumizi yao ya kawaida... au mfumo mwingine wowote utakaomsababisha aliyeshinda aone umuhimu wa nishani yake kwa miaka isiyopungua mitano.

Umuhimu wa hayo hapo juu ni kwamba kwa mfano: Staff wa BOT ambaye yuko say pale BOT kwenye internal audit ambaye angekuja akasema fedha ya EPA inachezewa... alafu ikagundulika kweli inachezewa, kama ilivyoonekana... na tukajua ni bil. 133... tunafanya juhudi zikarudi... huyu bwana ana-be-nominated na bodi ya wakaguzi wa mahesabu na anapewa nishati iliyotukuka na Rais wa Jamhuri... pia anapata advantages fulani kwa muda fulani kama tax excemption to say equivalent to 200mil. au say kwa muda fulani... vyovyote vile itakavyoonekana.

Nimekupata Mkuu, maoni yako ni mazuri.

Je hili linaweza kuingizwa katika TUZO YA MTANZANIA ALIYEFANYA VIZURI?
Tafadhali angalia thread hii . . . https://www.jamiiforums.com/showthread.php?t=16002
 
Mkuu Kasheshe,

Ninaungana na wewe katika hili.

Ugumu unakuja kwenye huo mfano wako.
Tungekuwa na ma-internal auditors wenye meno, je kungekuwa na haja ya kuajiri makampuni ya nje? Tatizo liko hivi ma-internal auditors wetu ni kama rubber stamps, wako pale kusafisha maovu yanayotendeka. Mfano mzuri ni ule uliotokea kwanye Richmond, jinsi TUKUKURU ilivyo sema Richmond hakuna dalili za Rushwa. Sehemu zote za idara za serikali ni hivyo hivyo.

Njimba

Njimba, umegusia kitu ambacho ni muhimu sana. Ni vema sasa ibuniwe mikakati ya kuwapa meno hawa Auditors au watu wengine watakaogundua maovu bila kuogopa wala kuwa na wasiwasi na kitu au mtu yeyote.

Kuna dada yetu Vicky Mtetema wa BBC ambaye alifanya coverage nzuri sana juu ya mauaji ya Maalbino lakini mpaka sasa hajapewa ulinzi wowote pamoja na vitisho vya kuuwawa anavyovipata. Nadhani masuala yote haya inabidi yaangaliwe kwa makini.
 
Njimba,

Njia nzuri ni kuwa-recognise wale wanaofanya kazi vizuri... watapatikana tu... Njia za kuwaogopesha, kuwaambia hamjui, kuwaambia hamna ethics etc... zimeshindikana sasa tujaribu kuwa-motivate... na kwa kweli niliyoyasema ndio uzalendo wenyewe...

Tunaweza kuwa na levels... za hizo nishani, ya wilaya, mkoa, taifa... ya proffesional board yenyewe...

Na ya Jamhuri.... hii ya Jamhuri... lazima uimbiwe wimbo wa Taifa na ikiwezekana na gwaride juu... kama protocal zinaruhusu...

Duu! Mkuu, hiyo Creativity yako ni kali sana. Inabidi tufanye consultation na research fulani kuangaalia possibilities zinazoweza kuwepo. Ila kama kutakuwa na uwezekano huo, basi itaboost morale wa wahusika kwa kiaasi kikubwa.

Suala la security yao na maslahi inabidi pia liangaliwe sana.
 
Kasheshe,

Kuna chama kingine nimesahau jina huwa kinaanda mkutano kila mwaka na rais, jamaa hata hawajui biashara, ni wajanja tu wa mjini ambao wanatumia hiyo nafasi kujenga connections. Unajua TZ connections zinalipa.

Ushauri wangu kwenye hiki chama chenu ni kukaa chini na vikundi vya watu ambao wamejaribu kufanya mambo mbalimbali na kusikiliza matatizo yao kisha kuandaa malengo yenu kwa lengo la kuondoa hivyo vikwanzo. Hivyi vyama inatakiwa visaidie wale wanaostruggle kutekeleza malengo yao na wala sio wale ambao tayari wako peak na wanafaidi matunda ya uhuru. Watu wa namna hiyo wako wengi, wakati sisi tunaenda kuitikia wito wa rais, tulikutana na watu kibao, ukiwasikiliza matatizo yao yalikuwa yanafanana sana na ya kwetu. Nafikiri baadaye rais alipata habari na idadi ya watu walioenda pale, hakurudia tena kuongelea hilo suala.

Duu! Mzalendo Mtanzania, umenifanya nibaki mdomo wazi kwa simulizi yako. Ama hakika inatakiwa ifanyike kazi ya ziada kuleta mabadiliko, vinginevyo itachukua muda mrefu sana kuweza kuleta mafanikio ya kweli.

Nadhani hicho chama kingine unachokitungumzia ni Tanzania National Business Council (TNBC).

Nimependa hiyo paragraph yako ya mwisho hapo juu. . . kama ni kweli mlihangaika hivyo, basi ni vema tujihesabu kuwa hatuna wazazi wa kutusaidia pamoja na kuwa na jitihada za dhati ya kujikomboa zilizohitaji msaada wa wazazi.

Unanikumbusha mbali sana. Nilikuwa na project yangu iliyokuwa inahitaji TIC Certificate nadhani 2005, ilinichukua miezi kadhaa kuipata, na baada ya hapo nikaanza kupambana na TRA ambako huko ndo usiseme, kidogo nikate tamaa. Kilichonisaidia ni kutokukubali kukata tamaa na kuendelea kufuatilia katika kila ngazi na hatimye nikafanikiwa kupata msamaha kwa baadhi ya vitu tu. Wakati huo hata pesa niliyobudget ikawa imepungua na gharama zingine zimeenda juu. Na hata charges za bandarini za storage nazo zikawa ziko juu sana kwa sababu ya muda mrefu kupita.

Ndugu zangu, mimi nadhani tujipange na kujiunda vizuri ili tujisaidie wenyewe. Tutakwenda kumwona rasmi Mh. Rais na kumwandikia ili kutimiza wajibu wetu kutokana na ahadi yake ili kuweka kumbukumbu sahihi ya nini tulifanya baada ya yeye kutoa ile ahadi yake. Na tunapoandika nitapenda hiyo resolution itiwe saini na wanataaluma wengi kuonyesha seriousness na ukubwa wa tatizo.

Kweli tunahitaji kazi ya ziada kuweza kusonga mbele. Natoa mwito tusikate tamaa.
 
Mtsimbe,

Kama kuna mambo unataka kujua niandikie hata kupitia PM yangu. naweza hata kukuunganisha na hao wenzangu wanaochakarika hapo Dar kila siku na wakakusaidia
kwa maelezo zaidi na si ajabu ukaona na barua zote za Ikulu, Ngasongwa wakati huo na mpaka tulikoishia kwa mama Meghji.

Kwa mfano rais alisema kulikuwa na fungu, baadaye ikaja onekana hakukuwa na fungu. Wanasiasa si wa kuwaamini sana.

Mimi nimepania tukimaliza project yetu nitatunga kitabu juu matatizo ya kufungua miradi TZ. Kuna haja ya kukabiliana ana kwa ana na hao middle class wa Tanzania ambao ndio kikwazo kikubwa cha maendeleo yetu.

Wakati machifu wetu walipouza nchi kwa peremende na magoboli walikuwa hawajui dunia wala hawakuwa na elimu, hawa wasomi wetu maofisini na idara mbalimbali wanauza nchi huku wanajua madhara zake. Either ni wapumbavu au ni waroho waliozidi kiasi. Mtu anaona ni bora amsaidie Mchina aliyefika jana kuliko Mtanzania mwenzake, sijui huyo mtu tumwitaje kama sio mpumbavu?

Mtanzania, TPN iliwahi kufuatilia suala la BOT guarantee ili tuone ni vipi ingeweza kusaidia kupata mikopo. Tuliambiwa hiyo guarantee inatolewa kwa mikopo ya nadhani mpaka TZS 350 Million. BoT wanacover 50% Security na nyingine unacover mwenyewe. BoT wanasema hiyo pesa inatolewa na Ministry of Finance ili wao wai-manage na inatakiwa kuwekwa katika budget ya Serikali.

Kuna mabenki ambayo BoT imeingia nayo mkataba wa kuweza kutumia hiyo Guarantee facility, lakini inaonekana ni mambo ya kwenye makaratasi tu kwani mabenk mengi hawaitumii isipokuwa kwa benki chache sana ambazo nazo pia hazipendelei sana mpango huu.

Pamoja na hayo yote nimeambiwa kuna maombi mengi sana ambayo yako pending BoT kutoka katika hizo bank chache na BoT kwa sasa hawana pesa yoyote toka serikalini. Inaonekana hiyo Guarantee ilitengewa budget kidogo sana ambayo hata hivyo imekwisha.

Ndugu zangu, ni bora kubuni mfumo wetu wenyewe kama kuanzisha TPN Fund, Venture Capital Fund au Investment Fund etc. I believe tukiunganisha nguvu kwa maelfu, we can start making little difference. Let us try that way.

Sometimes the road to success is very rough and hard.
 
Rais ana nia nzuri.
Mimi nafikiri tamko hilo tulilichukulia ndivyo sivyo ,Bado naamini mtu akiibuka na solutions nzuri serikali itamuunga mkono na ukisoma ktk habari hiyo utaona neno wasomi wabunifu.

Yani ninachojaribu kumuelewa Rais ni kua wasomi wabuni miradi na sio ubabaishaji na mradi huo uwe na mtazamo wa ku solve matatizo common ama compusory ya wananchi ,na sio mradi wowote utakua supported eti kwa vile kuna tamko la Rais.

Mfano hata kama mimi ningekua Rais nikatoa tamko kama lile kwa nchi yenye matatizo kama Tz ,siwezi pokea mradi mfano wa kujenga HOTEL,kujenga INTERNET,MTANDAO WA SIMU na mingine ya aina hiyo.Natambua vichochezi vya vitu hivyo ktk maendeleo lakini siwezi vipa GO AHEAD.Na ukizingatia kuna neno ubunifu

Miradi ambayo imebuniwa na ninayoweza ipa GO AHEAD ni kama vile matunda na mazao ya msimu kama vile viazi n.k hua vinafurika kwa mda mfupi na kutoweka na kufuatiwa na njaa kali, sasa basi atakaye kuja na solution ya jinsi ya kusindika mazao haya na matunda ya kaishi zaidi ya mwaka mradi huu nitauwezesha.

Ama mfano kuna tatizo la umeme hasa vijinini atakaye kuja na solution ya UMEME wa wireless,ama wa kutumia spectrum na kununua kifaa hicho kwa bei nafuu kabisa ,basi mradi huu nitauwezesha.

Nimekusoma Mkuu, tutatilia maanani ushauri wako. Kama una specific issues pia unaweza ukashare ili nazo zifanyiwe kazi.
 
mimi nafikiri inawezekana maana wanahitajika wasomi wabunifu,Na sio wasomi wapiga desa kwi kwi kwi utani

Mkamap, umesoma lakini post ya Mtanzania? Do u think they never had a good project? Soma tena maelezo yake. I think walijitahidi sana.
 
So far, kunajamaa wamejaribu kurusha up to 6v for a distance of 1metre. Ambayo kwa kweli ni kidogo sana. Umbali ni mkubwa sana huko tz, vijiji vimetapakaa mno.

Pia ukitumia high frequecies, to try to transmit power you will FRY everything on the way! Just like the Microwave would do to you if you put your hand in there.

Wakuu, naona hapa mnazungumza mambo ya Kitaaluma kidogo. Kama mnafikiri this could be a Feasible Project, ileteni TPN ifanyiwe kazi. . . . People can then see how we can move forward.
 
MkamaP,

Unaloliona wewe ni tatizo mtu mwingine anaweza asilione kama ni tatizo.

Pia aukitegemea rais atoe pesa ni kujisumbua bure.

Kinachotakiwa hapa ni change, systematic change ambayo ikifanyika ndio itaweza kuzaa wabunifu kwenye nyanja mbalimbali.

Ubunifu hautokei kwenye jangwa, innovation yoyote inatokana na watu na society ambayo imejengwa mazingira ya innovation kuzaliwa na kukua.

Kwa Tanzania ninayoiona mimi leo sahau innovation kama hatutashughulikia hayo mambo niliyoyaandika hapo juu.

Invention yoyote mpaka ifikie level ya innovation jua imeshakula pesa kibao na kama
hatuna jinsi ya kufund hizo activities, sahau kabisa?

Umeongelea umeme wa wireless, why bother na huo umeme wakati kuna solar power? Je ni kwanini solar power inashindwa kuongezeka TZ? Tatizo ni hilo hilo.

Pia watu wengine wanafikiri ubunifu ni kutoa product, ubunifu unaweza kutokea hata kwenye services, in fact western world sasa innovation zao nyingi ni kwenye process na wala sio products.

Akija mtu akatengeneza system ya kuondoa usumbufu wa TRA inaweza kuwa innovation nzuri kuliko hata kutengeneza product.

Wachina sasa wana copy kila kitu na wanaenda mbele. Dunia hii imejaa technologies mbalimbali na inatosha ku copy unachotaka na kukifanyia mabadiliko. Huawei Technolgies leo wanatamba duniani lakini ukiangalia product yao ya kwanza upande wa switching ilikuwa copy right na Lucent Technologies wakati upande wa data waliiga Cisco.

Hivyo ninachoona mimi ni kwamba rais anaweza kusaidia kubadili system ili ijenge mazingira ya wabunifu wa aina zote bila kuchagua. Huwezi kuona umuhimu wa jambo mpaka siku mamilioni wanafaidika. Mfano mzuri ni google, wakati wanaanza bank zote ziliwanyima pesa, lakini leo sidhani kuna mtu ambaye hajutii kwanini hakutoa pesa au hakununua shares zao mapema.

Kama kutunza viazi mbona kwetu kule miaka ya zamani walikuwa wanafanya hivyo? Walikuwa wanafukia viazi chini na vinadumu karibu mpaka msimu mwingine. Nilienda Sweden nikakuta na wenyewe kule vijijini wanatumia njia hiyo hiyo. Tatizo kwasasa huenda ni uzalishaji, kama huzalishi viazi vya kutosha na kuna demand ya viazi hivyo mjini, matokeo yake ni kuuza vyote. Kutunza viazi inatakiwa isiwe kazi ngumu kabisa.


Mkuu, nikipata muda mzuri nitakutumia PM.
 
Mtanzania
Nimekuelewa ,Lakini swala na innovation unalosema haliwezekani ama nisahahu wenda si kweli maana juzi tu nimeona JK akifungua mradi kule tanga wa kufua umeme kwa kutumia mkonge(katani).

Umeongelea swala la SOLAR kushindwa kuongezeka hii ni kwa sababu za msingi kabisa sola ni bei ghari hapo ndipo ubunfu unatakaiwa uchukue nafasi yake ili huduma iweze mfikia mwananchi kiurahisi na kwa bei nafuu.

Mfano simu za landline pamoja na huduma zake zimeshindwa kumeet watumiaji wengi ama kwa sababu za kiufundi,kijografia n.k kwa mapungufu yake sio lazima tuyalizimishe badala ya ke wabunifu wamebuni simu za mkononi ili kukidhi mapungufu yake,na bado kuna mapungufu ya simu za mkononi bado wamebuni VOIP ili kukabiliana na mapungufu hatimaye huduma imufikie mhusika na kwa bei nafuu.

Hatuwezi ng'ang'ania Solar kama solar ilivyo maana tayari imeshaonyesha mapungufu kwa miaka sasa na ndio maana imeshindwa ku deliver na badala yake wataalamu wabunifu wanaweza tumia hiyo solar kurekebisha ama kuongeza na hatimaye huduma imufikie mlengwa kwa bei rahisi na yenye tija,nimeongelea wireless ukiwa ni mfano tu.

Tupo pamoja ktk ku copy na kufanya marekebisho na mimi hicho ndicho naongelea na sio ku copy na ku pest kizima kizima.

Na nilichokua najaribu kuongelea ni miradi ambayo moja kwa moja inamsaidia mhusika kutoka chini ili aje avitumie vya juu,mfano huwezi mtu kumpa simu ya mkononi na ukampa masharti aitumie kuandika sms na kusoma sms wakati hajui kusoma na kuandika badala yake unatakiwa umfundishe kusoma na kuandika ndipo umpe simu ya namna hiyo.

Mkuu, nitakutafuta pia kwenye PM. Nataka nipate mawazo yenu ili kuandaa mazungumzo na hata masuala ya kiutendaji.
 
Ninataka kuanzisha huduma ya tiba ya moyo. Nina ujuzi wa kimataifa lakini mtaji wangu si mkubwa sana, hata hivyo nina washirika kitaaluma na kimtaji kutoka ujerumani na marekani ambao ni mahiri sana katika nyanja hii. Ninachoomba ni ushirikiano na serikali yako kuwa inisadie katika maswala ya mikataba ya kuwaleta washirika wangu hao wanapohitajika, na vile bvile niwe ninapewa nafasi ya kuhudumia wagonjwa wa moyo kabla serikali haijawapeleka nchi za nje. Kulingana na maadili ya taaluma yangu, sitalazimisha kutibu mgonjwa ambaye anahitaji huduma ambayo siwezi kutoa.
 
Ninataka kuanzisha huduma ya tiba ya moyo. Nina ujuzi wa kimataifa lakini mtaji wangu si mkubwa sana, hata hivyo nina washirika kitaaluma na kimtaji kutoka ujerumani na marekani ambao ni mahiri sana katika nyanja hii. Ninachoomba ni ushirikiano na serikali yako kuwa inisadie katika maswala ya mikataba ya kuwaleta washirika wangu hao wanapohitajika, na vile bvile niwe ninapewa nafasi ya kuhudumia wagonjwa wa moyo kabla serikali haijawapeleka nchi za nje. Kulingana na maadili ya taaluma yangu, sitalazimisha kutibu mgonjwa ambaye anahitaji huduma ambayo siwezi kutoa.

........huo ugomvi unaotaka kuuanzisha sijui kama utauweza.....lol
 
Mkuu, LOL unaelekea kama unamsemea Dr. Masu wa THI . . . LOL.

Inavutia sana kwa issue kama hii ikiwa moja ya ajenda ya kuongelea huku tukiwa na facts zote. Si hivyo tu kwa maoni yangu ni wakati muafaka sasa kuwa na Sera Mahsusi ambazo zitawasaidia kwa makusudi Wanataaluma wetu ambao wana nia ya dhati ya kutumia taaluma zao kuondoka matatizo ya watu au kuleta maendeleo. Of course haya yote ni vema yafanyike katika mchanganuo ambao utaonyesha wazi kuwa hatimaye Project hiyo/hizo zitajiendesha yenyewe.
 
Ninataka kuanzisha huduma ya tiba ya moyo. Nina ujuzi wa kimataifa lakini mtaji wangu si mkubwa sana, hata hivyo nina washirika kitaaluma na kimtaji kutoka ujerumani na marekani ambao ni mahiri sana katika nyanja hii. Ninachoomba ni ushirikiano na serikali yako kuwa inisadie katika maswala ya mikataba ya kuwaleta washirika wangu hao wanapohitajika, na vile bvile niwe ninapewa nafasi ya kuhudumia wagonjwa wa moyo kabla serikali haijawapeleka nchi za nje. Kulingana na maadili ya taaluma yangu, sitalazimisha kutibu mgonjwa ambaye anahitaji huduma ambayo siwezi kutoa(contradiction with nipewe wagonjwa kabla..).

Sio nataka kuanzisha...nilishaanzisha na nimeshakula vichwa kadhaa.
Pia nimekula NSSF contributions za wafanyakazi wangu.

...halafu ongezea na hii:

"Vile vile kwa kuwa mimi ni Mtanzania, ningeomba ushindani wa soko huru usiwe applied kwangu. Kuna wabaya wangu wanataka kuwaleta Apollo Hospital ambao wako mbali katika quality na organization. Naomba MONOPOLY katika sekta hii.

Sijafanya feasibility study kabla ya kuchukua msaada wa vifaa kutoka nje. Ningeweza kabisa kurudi MUCHS nilipokuwa mwanzo na vyombo hivi vingekuwa huko LAKINI bahati nzuri niliporudi nilipata fala mmoja akanikodishia nyumba yake. Sijamlipa kodi hata siku moja na nilihakikisha ndoto yangu ya kuwa na hospitali yangu inatumia MGONGO wake kisawasawa!

Baadaye jamaa alifungua kesi, lakini nilijua kesi ya madai haiuwi na kwa kuwa alikuwa na asili ya kiarabu haikuwa kazi kumzungusha na mahakama zetu njaa.

Mungu si Athumani, NSSF nao wakajilengesha. Nimewapiga bao la tiktak lakini beki wao, Ramadhani Dau ametoka kujaribu kurudisha hili bao. Nilifanikiwa kupata wachezaji wa kulipwa kutoka USA na kwingineko akiwepo Mganga wa timu Mtikila ambao wanafanya vitu vyao.

So far upepo sio mbaya...kesi Tanzania inasukuma siku ziende...HALLELUJAH!
 
Ninataka kuanzisha huduma ya tiba ya moyo. Nina ujuzi wa kimataifa lakini mtaji wangu si mkubwa sana, hata hivyo nina washirika kitaaluma na kimtaji kutoka ujerumani na marekani ambao ni mahiri sana katika nyanja hii. Ninachoomba ni ushirikiano na serikali yako kuwa inisadie katika maswala ya mikataba ya kuwaleta washirika wangu hao wanapohitajika, na vile bvile niwe ninapewa nafasi ya kuhudumia wagonjwa wa moyo kabla serikali haijawapeleka nchi za nje. Kulingana na maadili ya taaluma yangu, sitalazimisha kutibu mgonjwa ambaye anahitaji huduma ambayo siwezi kutoa.


Kichuguu & Others,
Nadhani kabla ya kuendelea kuchangia please ninawaomba muingie hapa

http://www.coping.org/write/percept/fallacies/content.htm#Missing

Nina amini baada ya kupitia hapo hali ya uchangiaji katika thread hii itaimarika.

Mtsimbe usichoke, kawaida mwanzo ni mgumu na niimani yangu kuwa baada ya muda sio mrefu thread hii itabakia na watu wachache huenda wasizidi watatu. Wengi wetu humu ni makada wa Chama fulani na kazi yetu kila siku ni kufuatilia tuiseme vipi serikali na kawaida hatupendi hata kuangalia ukweli, sisi tunaangalia nani!!
 
Back
Top Bottom