Njimba,
Njia nzuri ni kuwa-recognise wale wanaofanya kazi vizuri... watapatikana tu... Njia za kuwaogopesha, kuwaambia hamjui, kuwaambia hamna ethics etc... zimeshindikana sasa tujaribu kuwa-motivate... na kwa kweli niliyoyasema ndio uzalendo wenyewe...
Tunaweza kuwa na levels... za hizo nishani, ya wilaya, mkoa, taifa... ya proffesional board yenyewe...
Na ya Jamhuri.... hii ya Jamhuri... lazima uimbiwe wimbo wa Taifa na ikiwezekana na gwaride juu... kama protocal zinaruhusu...
Kasheshe,
Suala ni utawapataje hao watakaofanya vizuri huko mbeleni?
Tamko la rais lilitia matumaini kwa watu wengi na ndio maana wengine tukaamua kwenda kumuona. Bahati nzuri sisi tulikuwa na nondo zote maana tulikuwa tumezunguka kwenye system kuanzia mwaka 2003. Vijana wasomi, tuliungana pamoja kujaribu kufanya miradi ya maana kule tunakotoka kwa lengo la kuendeleza hilo eneo, kupunguza umaskini na of course sisi wenyewe kujitengenezea vijisenti kidogo.
Wengine tulikuwa Ulaya na wengine wako TZ. Bahati nzuri wengine pamoja na kuwa Ulaya tunaijua TZ vizuri labda kuliko jamaa wengi tu walioko pale Dar.
Tatizo ni lile lile, ili ufanye jambo lolote la maana mahali popote unahitaji mtaji, kwa sehemu kubwa watu wanategemea banks. Banks nyingi zinalenga kwenye faida kwa kutumia vigezo ambavyo vimeonyesha kufanya kazi huko nyuma. Kama mahoteli yanalipa, basi wanatoa mikopo ya mahoteli, kama kukopesha wafanyakazi kujenga nyumba kunalipa wanafanya hivyo, hivyo hivyo na kununua magari kwa middle class ya TZ. Ukitaka pesa kwenye miradi ya namna hiyo una nafasi ya kupata pesa TZ.
Ukija na mradi wako ukasema unataka kujenga kiwanda cha matunda Tanga, unataka kutengeneza innovation centre Mbeya, na mambo mengi ya kitaalamu hapo ndio sahau mikopo ya bank unless una jina linaishia na Lowassa au Kikwete. Kumbuka hata USA Google walistruggle kupata pesa lakini wote tunaona matunda yake. Miradi mingi ya kitaaluma na ambayo ni mipya sio rahisi kupata pesa kwenye mfumo uliopo wa utoaji pesa.
Hapo ndipo serikali inatakiwa isaidie kupitia banks kama TIB kama ingelikuwa inafanya kazi ipasavyo na vitengo vingine ambavyo serikali itaamua. Nchi zote zilizoendelea na zinazoendelea kuna fungu la namna hii la kusaidia ile unaweza kuiita unconventional miradi iweze kupata funding. Kuna miradi itakufa lakini kuna mingine mingi itafanikiwa na kuleta a big impact kwenye society. China sasa inaongoza kwa kutenge fungu kubwa la pesa kusaidia miradi ya namna hii.
OK, umepata pesa, tena za mkopo, inatakiwa uzitumie haraka ili biashara ianze na ulipe deni haraka ili interests zisiendelee kukua. Hapo ndipo unakumbana na idara za serikali mbalimbali ambazo ni kikwazo kwa Watanzania wabunifu. Imagine unaanza na TIC ili upate certificate yao ikusaidie kupunguza gharama za VAT na vitu vingine. Wageni wote hapo ndipo wanaanzia maana kila anayejua uchumi anajua hata saving ya asilimia moja ni bora kuliko saving ya zero.
Unaanza TIC, sio wabaya sana na wanajitahidi lakini hata wao kuna mambo wanaweza kuyarekebisha hasa kwa makundi ya wataalamu wa Kitanzania. Hapo kuna kuandika proposal ambayo nilivyoona mimi hawasomi, ni usumbufu tu usio na maana, kuna kulipa, kuna kuandaa documents kibao. Vitu vyote hivyo vinahitaji pesa.
Ukimaliza hapo ndipo sasa unaanza kukumbana na idara zingine za serikali hasa TRA. Bahati mbaya mradi wako unataka uwe Kigoma. Ili kupata kibali tu cha kununua cement unaweza kulazimika safari za Kigoma na Dar kama tatu, zote hizo ni gharama. Anayejenga Dar anapata kibali si ajabu siku hiyo hiyo, kwanini watu wapeleke miradi mikoani?
Nimetoa mfano wa community radio, kuna mtu atasema sasa mambo yamebadilika. Hiyo info niliyotoa ni ya wiki jana. Unaambiwa utengeneze proposal na ili proposal yako ipite nenda kwa watu hawa na hawa. Ukiwaona hao jamaa gharama yake sio chini ya milioni. Kama ni mikoani haipungui 1.5M. Bado mambo mengine chungu nzima, kwenda kuisajili hiyo radio BRELA, kwenda wapi, gharama za kushughulikia tu kupata leseni tena ya community radio
ambayo huku kwa wenzetu kama ni eneo ambalo halina radio nyingi, unaweza kupata kwa siku moja, kwa TZ ni project ya miezi zaidi ya minne na gharama kibao.
Kwa mawazo yangu hapo ndipo penye matatizo. Kama rais anataka kusaidia basi kwenye maeneo husika lazima hizi taratibu zipunguzwe sana ili iwe rahisi kuanzisha hivi vikundi vya wasomi na kuanza kufanya mambo yao bila usumbufu mkubwa na gharama kubwa mwanzoni.
Mfano mzuri ni kuwa na one stop center ambayo inashughulikia mambo yote. Kuanzia kuangalia proposal yako mpaka kuku advice namna ya kupata funding. Hiyo center iwe kama mlezi wa hivyo vikundi na kuvisaidia mwanzoni ili visimame vyenyewe. Hii ikiongozana na vitu kama msamaha wa kulipa kodi au VAT kwa miezi sita ya mwanzo nk.
Tatizo nililoliona TZ kwenye boards au vyama hivi vya wataalamu au wafanyabiashara ni kwamba havina faida kubwa kwa watu wanaotaka kuanza biashara. Viko pale kulinda maslahi yao na kutafuta connections. Ukiangalia mabaraza ya biashara kama kile chama cha akina Musiba. Wale hawako pale kusaidia wafanyabiashara wapya, hata ukienda kuwaona unajisumbua bure. Wako pale kulinda maslahi yao na kuangalia wataendelea kufaidika vipi.
Kuna chama kingine nimesahau jina huwa kinaanda mkutano kila mwaka na rais, jamaa hata hawajui biashara, ni wajanja tu wa mjini ambao wanatumia hiyo nafasi kujenga connections. Unajua TZ connections zinalipa.
Ushauri wangu kwenye hiki chama chenu ni kukaa chini na vikundi vya watu ambao wamejaribu kufanya mambo mbalimbali na kusikiliza matatizo yao kisha kuandaa malengo yenu kwa lengo la kuondoa hivyo vikwanzo. Hivyi vyama inatakiwa visaidie wale wanaostruggle kutekeleza malengo yao na wala sio wale ambao tayari wako peak na wanafaidi matunda ya uhuru. Watu wa namna hiyo wako wengi, wakati sisi tunaenda kuitikia wito wa rais, tulikutana na watu kibao, ukiwasikiliza matatizo yao yalikuwa yanafanana sana na ya kwetu. Nafikiri baadaye rais alipata habari na idadi ya watu walioenda pale, hakurudia tena kuongelea hilo suala.
Kikubwa zaidi kwa hivi vikundi vya watanzania wanaotaka kuungana na kufanya mambo ya maana nyumbani ni kujua toka mwanzoni kwamba msaada wa serikali unaweza kuwa mdogo sana hivyo ni bora kujiandaa kwa mapambano toka mwanzoni. Kama mradi wako unafikiri utagharimu milioni 100, basi weka 150M, hiyo 50M ni matokeao ya urasimu kwenye idara za serikali. Sasa kama unakopa sijui hizo pesa utazihalalisha vipi?
Nikisoma matatizo ya Dr. Masua binafsi sishangai maana nimepitia karibu yote hayo anayoyasema. Ni kweli hata sisi wenyewe kuna makosa tumefanya lakini huwezi ku avoid makosa, muhimu ni kujifunza na kusonga mbele. Taifa linaloshindwa kuwasaidia watu kama huyo dr. lisitegemea kuendelea au kujitegemea. Muhimu ni dialogue kati ya hawa wabunifu na serikali. Kiburi toka upande mmoja haisaidii. Watu wanafikiri wanamkomoa Dr.Masau kumbe in fact wanaliua taifa.