Rais Kikwete Bado Anatusubiri Tukamwone

Rais Kikwete Bado Anatusubiri Tukamwone

Ili kuhakikisha huduma kwa wananchi zinaimarika na ili kuhakikisha fedha zetu zinatumika vizuri, na ili kuhakikisha kazi zinazofanyika zinafanyika kwa kiwango cha hali ya juu sana. Nashauri yafuatayo.

1. Kuwepo na mashindano ya ubora wa huduma, ubunifu ambao unakuwa aidha unalisaidia taifa kwa kuokoa fedha nyingi... au kwa kuwapa wananchi wengi huduma zaidi bila kutumia rocket science. Nia ya hii ni kuhakikisha proffesional boards zitoe mfano engineer ambaye ataoa design ya barabara ambayo ni cheaper kufanya yetu inaweza saidia tatizo la foleni kwa Dar es Salaam... huu ni mfano tu.

2. Washindi wanaweza kutoka kwenye proffesional boards mbalimbali, mfano kutoka kwa madaktari, wahandisi,wauguzi,wahasibu, wanaICT etc.

3. Washindi wapewe recognition (nishani ya Rais wa Jamhuri iliyotukuka au hata nishani ya Jamhuri) na zawaidi kwenye sherehe aidha za Mashujaa ya za Jamhuri.

4. Washindi waweze ku-reclaim tax for say 5 years kwa matumizi yao ya kawaida... au mfumo mwingine wowote utakaomsababisha aliyeshinda aone umuhimu wa nishani yake kwa miaka isiyopungua mitano.

Umuhimu wa hayo hapo juu ni kwamba kwa mfano: Staff wa BOT ambaye yuko say pale BOT kwenye internal audit ambaye angekuja akasema fedha ya EPA inachezewa... alafu ikagundulika kweli inachezewa, kama ilivyoonekana... na tukajua ni bil. 133... tunafanya juhudi zikarudi... huyu bwana ana-be-nominated na bodi ya wakaguzi wa mahesabu na anapewa nishati iliyotukuka na Rais wa Jamhuri... pia anapata advantages fulani kwa muda fulani kama tax excemption to say equivalent to 200mil. au say kwa muda fulani... vyovyote vile itakavyoonekana.
 
Mkuu Kasheshe,

Ninaungana na wewe katika hili.

Ugumu unakuja kwenye huo mfano wako.
Tungekuwa na ma-internal auditors wenye meno, je kungekuwa na haja ya kuajiri makampuni ya nje? Tatizo liko hivi ma-internal auditors wetu ni kama rubber stamps, wako pale kusafisha maovu yanayotendeka. Mfano mzuri ni ule uliotokea kwanye Richmond, jinsi TUKUKURU ilivyo sema Richmond hakuna dalili za Rushwa. Sehemu zote za idara za serikali ni hivyo hivyo.

Njimba
 
Njimba,

Njia nzuri ni kuwa-recognise wale wanaofanya kazi vizuri... watapatikana tu... Njia za kuwaogopesha, kuwaambia hamjui, kuwaambia hamna ethics etc... zimeshindikana sasa tujaribu kuwa-motivate... na kwa kweli niliyoyasema ndio uzalendo wenyewe...

Tunaweza kuwa na levels... za hizo nishani, ya wilaya, mkoa, taifa... ya proffesional board yenyewe...

Na ya Jamhuri.... hii ya Jamhuri... lazima uimbiwe wimbo wa Taifa na ikiwezekana na gwaride juu... kama protocal zinaruhusu...
 
Kasheshe,

Suala ni utawapataje hao watakaofanya vizuri huko mbeleni?

Tamko la rais lilitia matumaini kwa watu wengi na ndio maana wengine tukaamua kwenda kumuona. Bahati nzuri sisi tulikuwa na nondo zote maana tulikuwa tumezunguka kwenye system kuanzia mwaka 2003. Vijana wasomi, tuliungana pamoja kujaribu kufanya miradi ya maana kule tunakotoka kwa lengo la kuendeleza hilo eneo, kupunguza umaskini na of course sisi wenyewe kujitengenezea vijisenti kidogo.

Wengine tulikuwa Ulaya na wengine wako TZ. Bahati nzuri wengine pamoja na kuwa Ulaya tunaijua TZ vizuri labda kuliko jamaa wengi tu walioko pale Dar.

Tatizo ni lile lile, ili ufanye jambo lolote la maana mahali popote unahitaji mtaji, kwa sehemu kubwa watu wanategemea banks. Banks nyingi zinalenga kwenye faida kwa kutumia vigezo ambavyo vimeonyesha kufanya kazi huko nyuma. Kama mahoteli yanalipa, basi wanatoa mikopo ya mahoteli, kama kukopesha wafanyakazi kujenga nyumba kunalipa wanafanya hivyo, hivyo hivyo na kununua magari kwa middle class ya TZ. Ukitaka pesa kwenye miradi ya namna hiyo una nafasi ya kupata pesa TZ.

Ukija na mradi wako ukasema unataka kujenga kiwanda cha matunda Tanga, unataka kutengeneza innovation centre Mbeya, na mambo mengi ya kitaalamu hapo ndio sahau mikopo ya bank unless una jina linaishia na Lowassa au Kikwete. Kumbuka hata USA Google walistruggle kupata pesa lakini wote tunaona matunda yake. Miradi mingi ya kitaaluma na ambayo ni mipya sio rahisi kupata pesa kwenye mfumo uliopo wa utoaji pesa.

Hapo ndipo serikali inatakiwa isaidie kupitia banks kama TIB kama ingelikuwa inafanya kazi ipasavyo na vitengo vingine ambavyo serikali itaamua. Nchi zote zilizoendelea na zinazoendelea kuna fungu la namna hii la kusaidia ile unaweza kuiita unconventional miradi iweze kupata funding. Kuna miradi itakufa lakini kuna mingine mingi itafanikiwa na kuleta a big impact kwenye society. China sasa inaongoza kwa kutenge fungu kubwa la pesa kusaidia miradi ya namna hii.

OK, umepata pesa, tena za mkopo, inatakiwa uzitumie haraka ili biashara ianze na ulipe deni haraka ili interests zisiendelee kukua. Hapo ndipo unakumbana na idara za serikali mbalimbali ambazo ni kikwazo kwa Watanzania wabunifu. Imagine unaanza na TIC ili upate certificate yao ikusaidie kupunguza gharama za VAT na vitu vingine. Wageni wote hapo ndipo wanaanzia maana kila anayejua uchumi anajua hata saving ya asilimia moja ni bora kuliko saving ya zero.

Unaanza TIC, sio wabaya sana na wanajitahidi lakini hata wao kuna mambo wanaweza kuyarekebisha hasa kwa makundi ya wataalamu wa Kitanzania. Hapo kuna kuandika proposal ambayo nilivyoona mimi hawasomi, ni usumbufu tu usio na maana, kuna kulipa, kuna kuandaa documents kibao. Vitu vyote hivyo vinahitaji pesa.

Ukimaliza hapo ndipo sasa unaanza kukumbana na idara zingine za serikali hasa TRA. Bahati mbaya mradi wako unataka uwe Kigoma. Ili kupata kibali tu cha kununua cement unaweza kulazimika safari za Kigoma na Dar kama tatu, zote hizo ni gharama. Anayejenga Dar anapata kibali si ajabu siku hiyo hiyo, kwanini watu wapeleke miradi mikoani?

Nimetoa mfano wa community radio, kuna mtu atasema sasa mambo yamebadilika. Hiyo info niliyotoa ni ya wiki jana. Unaambiwa utengeneze proposal na ili proposal yako ipite nenda kwa watu hawa na hawa. Ukiwaona hao jamaa gharama yake sio chini ya milioni. Kama ni mikoani haipungui 1.5M. Bado mambo mengine chungu nzima, kwenda kuisajili hiyo radio BRELA, kwenda wapi, gharama za kushughulikia tu kupata leseni tena ya community radio
ambayo huku kwa wenzetu kama ni eneo ambalo halina radio nyingi, unaweza kupata kwa siku moja, kwa TZ ni project ya miezi zaidi ya minne na gharama kibao.

Kwa mawazo yangu hapo ndipo penye matatizo. Kama rais anataka kusaidia basi kwenye maeneo husika lazima hizi taratibu zipunguzwe sana ili iwe rahisi kuanzisha hivi vikundi vya wasomi na kuanza kufanya mambo yao bila usumbufu mkubwa na gharama kubwa mwanzoni.

Mfano mzuri ni kuwa na one stop center ambayo inashughulikia mambo yote. Kuanzia kuangalia proposal yako mpaka kuku advice namna ya kupata funding. Hiyo center iwe kama mlezi wa hivyo vikundi na kuvisaidia mwanzoni ili visimame vyenyewe. Hii ikiongozana na vitu kama msamaha wa kulipa kodi au VAT kwa miezi sita ya mwanzo nk.

Tatizo nililoliona TZ kwenye boards au vyama hivi vya wataalamu au wafanyabiashara ni kwamba havina faida kubwa kwa watu wanaotaka kuanza biashara. Viko pale kulinda maslahi yao na kutafuta connections. Ukiangalia mabaraza ya biashara kama kile chama cha akina Musiba. Wale hawako pale kusaidia wafanyabiashara wapya, hata ukienda kuwaona unajisumbua bure. Wako pale kulinda maslahi yao na kuangalia wataendelea kufaidika vipi.

Kuna chama kingine nimesahau jina huwa kinaanda mkutano kila mwaka na rais, jamaa hata hawajui biashara, ni wajanja tu wa mjini ambao wanatumia hiyo nafasi kujenga connections. Unajua TZ connections zinalipa.

Ushauri wangu kwenye hiki chama chenu ni kukaa chini na vikundi vya watu ambao wamejaribu kufanya mambo mbalimbali na kusikiliza matatizo yao kisha kuandaa malengo yenu kwa lengo la kuondoa hivyo vikwanzo. Hivyi vyama inatakiwa visaidie wale wanaostruggle kutekeleza malengo yao na wala sio wale ambao tayari wako peak na wanafaidi matunda ya uhuru. Watu wa namna hiyo wako wengi, wakati sisi tunaenda kuitikia wito wa rais, tulikutana na watu kibao, ukiwasikiliza matatizo yao yalikuwa yanafanana sana na ya kwetu. Nafikiri baadaye rais alipata habari na idadi ya watu walioenda pale, hakurudia tena kuongelea hilo suala.

Kikubwa zaidi kwa hivi vikundi vya watanzania wanaotaka kuungana na kufanya mambo ya maana nyumbani ni kujua toka mwanzoni kwamba msaada wa serikali unaweza kuwa mdogo sana hivyo ni bora kujiandaa kwa mapambano toka mwanzoni. Kama mradi wako unafikiri utagharimu milioni 100, basi weka 150M, hiyo 50M ni matokeao ya urasimu kwenye idara za serikali. Sasa kama unakopa sijui hizo pesa utazihalalisha vipi?

Nikisoma matatizo ya Dr. Masua binafsi sishangai maana nimepitia karibu yote hayo anayoyasema. Ni kweli hata sisi wenyewe kuna makosa tumefanya lakini huwezi ku avoid makosa, muhimu ni kujifunza na kusonga mbele. Taifa linaloshindwa kuwasaidia watu kama huyo dr. lisitegemea kuendelea au kujitegemea. Muhimu ni dialogue kati ya hawa wabunifu na serikali. Kiburi toka upande mmoja haisaidii. Watu wanafikiri wanamkomoa Dr.Masau kumbe in fact wanaliua taifa.
 
Mtanzania, kwanza nakupongeza sana wewe na wenzako ambao mliliona hili na kulifanyia kazi mapema. Inasikitisha sana kuona kuwa mlizungushwa sana. Nadhani hili kwa hakika ni moja ya tatizo kwa Wasomi na Wanataaluma.

Tumedhamiria kumwona mwenyewe, huenda kuna nia nzuri alikuwa nayo alipotoa ahadi yake. Ningeshauri kama una details kuhusu mambo ambayo ulipenda yafanyiwe kazi tuweze kuwasiliana kupitia barua pepe president@tpn.co.tz.

Nashukuru pia kwa baadhi ya kero ulizoziorodhesha ambazo kwa hakika tukipata na maelezo ya kutosha tutazichukua kama agenda.

Mtsimbe,

Kama kuna mambo unataka kujua niandikie hata kupitia PM yangu. naweza hata kukuunganisha na hao wenzangu wanaochakarika hapo Dar kila siku na wakakusaidia
kwa maelezo zaidi na si ajabu ukaona na barua zote za Ikulu, Ngasongwa wakati huo na mpaka tulikoishia kwa mama Meghji.

Kwa mfano rais alisema kulikuwa na fungu, baadaye ikaja onekana hakukuwa na fungu. Wanasiasa si wa kuwaamini sana.

Mimi nimepania tukimaliza project yetu nitatunga kitabu juu matatizo ya kufungua miradi TZ. Kuna haja ya kukabiliana ana kwa ana na hao middle class wa Tanzania ambao ndio kikwazo kikubwa cha maendeleo yetu.

Wakati machifu wetu walipouza nchi kwa peremende na magoboli walikuwa hawajui dunia wala hawakuwa na elimu, hawa wasomi wetu maofisini na idara mbalimbali wanauza nchi huku wanajua madhara zake. Either ni wapumbavu au ni waroho waliozidi kiasi. Mtu anaona ni bora amsaidie Mchina aliyefika jana kuliko Mtanzania mwenzake, sijui huyo mtu tumwitaje kama sio mpumbavu?
 
Rais ana nia nzuri.
Mimi nafikiri tamko hilo tulilichukulia ndivyo sivyo ,Bado naamini mtu akiibuka na solutions nzuri serikali itamuunga mkono na ukisoma ktk habari hiyo utaona neno wasomi wabunifu.

Yani ninachojaribu kumuelewa Rais ni kua wasomi wabuni miradi na sio ubabaishaji na mradi huo uwe na mtazamo wa ku solve matatizo common ama compusory ya wananchi ,na sio mradi wowote utakua supported eti kwa vile kuna tamko la Rais.

Mfano hata kama mimi ningekua Rais nikatoa tamko kama lile kwa nchi yenye matatizo kama Tz ,siwezi pokea mradi mfano wa kujenga HOTEL,kujenga INTERNET,MTANDAO WA SIMU na mingine ya aina hiyo.Natambua vichochezi vya vitu hivyo ktk maendeleo lakini siwezi vipa GO AHEAD.Na ukizingatia kuna neno ubunifu

Miradi ambayo imebuniwa na ninayoweza ipa GO AHEAD ni kama vile matunda na mazao ya msimu kama vile viazi n.k hua vinafurika kwa mda mfupi na kutoweka na kufuatiwa na njaa kali, sasa basi atakaye kuja na solution ya jinsi ya kusindika mazao haya na matunda ya kaishi zaidi ya mwaka mradi huu nitauwezesha.

Ama mfano kuna tatizo la umeme hasa vijinini atakaye kuja na solution ya UMEME wa wireless,ama wa kutumia spectrum na kununua kifaa hicho kwa bei nafuu kabisa ,basi mradi huu nitauwezesha.
 
Vyema sana kufikiria outside the box. Ila hiyo combination ya bei nafuu na hiyo teknolojia haiwezekani kwa sasa!
 
mimi nafikiri inawezekana maana wanahitajika wasomi wabunifu,Na sio wasomi wapiga desa kwi kwi kwi utani
 
Kama ilikuwa inawezekana ingekwisha fanyika. Kurusha umeme unaoweza kutumika kwa matumizi ya nyumbani kwa njia ya upepo ni ngumu. Kuna sababu nyingi za kiutaalamu. Mojawapo ni Voltages and Current levels required.

Ila sema unaweza kutuma data (intaneti and co) kupitia waya hizi hizi za umeme!
 
Mimi bado nafikiri inawezekana mkubwa

Ukichukua umeme mdogo kutoka kwenye spectrum, tuseme utumie fotodiode harafu u amplify current na voltage tuseme 30A na 50V hapo una 1.5kW harafu una upitisha kwenye step up transformer,hapo unaonaje mkuu??
Lakini hiyo DC unayotoa kwenye fotodiode unai change inakua AC kabla ya kui feed ktk transformer.

Ama unaweza tumia filter circuit kuchota spectrum fulani.
 
So far, kunajamaa wamejaribu kurusha up to 6v for a distance of 1metre. Ambayo kwa kweli ni kidogo sana. Umbali ni mkubwa sana huko tz, vijiji vimetapakaa mno.

Pia ukitumia high frequecies, to try to transmit power you will FRY everything on the way! Just like the Microwave would do to you if you put your hand in there.
 
Rais ana nia nzuri.
Mimi nafikiri tamko hilo tulilichukulia ndivyo sivyo ,Bado naamini mtu akiibuka na solutions nzuri serikali itamuunga mkono na ukisoma ktk habari hiyo utaona neno wasomi wabunifu.

Yani ninachojaribu kumuelewa Rais ni kua wasomi wabuni miradi na sio ubabaishaji na mradi huo uwe na mtazamo wa ku solve matatizo common ama compusory ya wananchi ,na sio mradi wowote utakua supported eti kwa vile kuna tamko la Rais.

Mfano hata kama mimi ningekua Rais nikatoa tamko kama lile kwa nchi yenye matatizo kama Tz ,siwezi pokea mradi mfano wa kujenga HOTEL,kujenga INTERNET,MTANDAO WA SIMU na mingine ya aina hiyo.Natambua vichochezi vya vitu hivyo ktk maendeleo lakini siwezi vipa GO AHEAD.Na ukizingatia kuna neno ubunifu

Miradi ambayo imebuniwa na ninayoweza ipa GO AHEAD ni kama vile matunda na mazao ya msimu kama vile viazi n.k hua vinafurika kwa mda mfupi na kutoweka na kufuatiwa na njaa kali, sasa basi atakaye kuja na solution ya jinsi ya kusindika mazao haya na matunda ya kaishi zaidi ya mwaka mradi huu nitauwezesha.

Ama mfano kuna tatizo la umeme hasa vijinini atakaye kuja na solution ya UMEME wa wireless,ama wa kutumia spectrum na kununua kifaa hicho kwa bei nafuu kabisa ,basi mradi huu nitauwezesha.

MkamaP,

Unaloliona wewe ni tatizo mtu mwingine anaweza asilione kama ni tatizo.

Pia aukitegemea rais atoe pesa ni kujisumbua bure.

Kinachotakiwa hapa ni change, systematic change ambayo ikifanyika ndio itaweza kuzaa wabunifu kwenye nyanja mbalimbali.

Ubunifu hautokei kwenye jangwa, innovation yoyote inatokana na watu na society ambayo imejengwa mazingira ya innovation kuzaliwa na kukua.

Kwa Tanzania ninayoiona mimi leo sahau innovation kama hatutashughulikia hayo mambo niliyoyaandika hapo juu.

Invention yoyote mpaka ifikie level ya innovation jua imeshakula pesa kibao na kama
hatuna jinsi ya kufund hizo activities, sahau kabisa?

Umeongelea umeme wa wireless, why bother na huo umeme wakati kuna solar power? Je ni kwanini solar power inashindwa kuongezeka TZ? Tatizo ni hilo hilo.

Pia watu wengine wanafikiri ubunifu ni kutoa product, ubunifu unaweza kutokea hata kwenye services, in fact western world sasa innovation zao nyingi ni kwenye process na wala sio products.

Akija mtu akatengeneza system ya kuondoa usumbufu wa TRA inaweza kuwa innovation nzuri kuliko hata kutengeneza product.

Wachina sasa wana copy kila kitu na wanaenda mbele. Dunia hii imejaa technologies mbalimbali na inatosha ku copy unachotaka na kukifanyia mabadiliko. Huawei Technolgies leo wanatamba duniani lakini ukiangalia product yao ya kwanza upande wa switching ilikuwa copy right na Lucent Technologies wakati upande wa data waliiga Cisco.

Hivyo ninachoona mimi ni kwamba rais anaweza kusaidia kubadili system ili ijenge mazingira ya wabunifu wa aina zote bila kuchagua. Huwezi kuona umuhimu wa jambo mpaka siku mamilioni wanafaidika. Mfano mzuri ni google, wakati wanaanza bank zote ziliwanyima pesa, lakini leo sidhani kuna mtu ambaye hajutii kwanini hakutoa pesa au hakununua shares zao mapema.

Kama kutunza viazi mbona kwetu kule miaka ya zamani walikuwa wanafanya hivyo? Walikuwa wanafukia viazi chini na vinadumu karibu mpaka msimu mwingine. Nilienda Sweden nikakuta na wenyewe kule vijijini wanatumia njia hiyo hiyo. Tatizo kwasasa huenda ni uzalishaji, kama huzalishi viazi vya kutosha na kuna demand ya viazi hivyo mjini, matokeo yake ni kuuza vyote. Kutunza viazi inatakiwa isiwe kazi ngumu kabisa.
 
MkamaP,

Unaloliona wewe ni tatizo mtu mwingine anaweza asilione kama ni tatizo.

Pia aukitegemea rais atoe pesa ni kujisumbua bure.

Kinachotakiwa hapa ni change, systematic change ambayo ikifanyika ndio itaweza kuzaa wabunifu kwenye nyanja mbalimbali.

Ubunifu hautokei kwenye jangwa, innovation yoyote inatokana na watu na society ambayo imejengwa mazingira ya innovation kuzaliwa na kukua.

Kwa Tanzania ninayoiona mimi leo sahau innovation kama hatutashughulikia hayo mambo niliyoyaandika hapo juu.

Invention yoyote mpaka ifikie level ya innovation jua imeshakula pesa kibao na kama
hatuna jinsi ya kufund hizo activities, sahau kabisa?

Umeongelea umeme wa wireless, why bother na huo umeme wakati kuna solar power? Je ni kwanini solar power inashindwa kuongezeka TZ? Tatizo ni hilo hilo.

Pia watu wengine wanafikiri ubunifu ni kutoa product, ubunifu unaweza kutokea hata kwenye services, in fact western world sasa innovation zao nyingi ni kwenye process na wala sio products.

Akija mtu akatengeneza system ya kuondoa usumbufu wa TRA inaweza kuwa innovation nzuri kuliko hata kutengeneza product.

Wachina sasa wana copy kila kitu na wanaenda mbele. Dunia hii imejaa technologies mbalimbali na inatosha ku copy unachotaka na kukifanyia mabadiliko. Huawei Technolgies leo wanatamba duniani lakini ukiangalia product yao ya kwanza upande wa switching ilikuwa copy right na Lucent Technologies wakati upande wa data waliiga Cisco.

Hivyo ninachoona mimi ni kwamba rais anaweza kusaidia kubadili system ili ijenge mazingira ya wabunifu wa aina zote bila kuchagua. Huwezi kuona umuhimu wa jambo mpaka siku mamilioni wanafaidika. Mfano mzuri ni google, wakati wanaanza bank zote ziliwanyima pesa, lakini leo sidhani kuna mtu ambaye hajutii kwanini hakutoa pesa au hakununua shares zao mapema.

Mtanzania
Nimekuelewa ,Lakini swala na innovation unalosema haliwezekani ama nisahahu wenda si kweli maana juzi tu nimeona JK akifungua mradi kule tanga wa kufua umeme kwa kutumia mkonge(katani).

Umeongelea swala la SOLAR kushindwa kuongezeka hii ni kwa sababu za msingi kabisa sola ni bei ghari hapo ndipo ubunfu unatakaiwa uchukue nafasi yake ili huduma iweze mfikia mwananchi kiurahisi na kwa bei nafuu.

Mfano simu za landline pamoja na huduma zake zimeshindwa kumeet watumiaji wengi ama kwa sababu za kiufundi,kijografia n.k kwa mapungufu yake sio lazima tuyalizimishe badala ya ke wabunifu wamebuni simu za mkononi ili kukidhi mapungufu yake,na bado kuna mapungufu ya simu za mkononi bado wamebuni VOIP ili kukabiliana na mapungufu hatimaye huduma imufikie mhusika na kwa bei nafuu.

Hatuwezi ng'ang'ania Solar kama solar ilivyo maana tayari imeshaonyesha mapungufu kwa miaka sasa na ndio maana imeshindwa ku deliver na badala yake wataalamu wabunifu wanaweza tumia hiyo solar kurekebisha ama kuongeza na hatimaye huduma imufikie mlengwa kwa bei rahisi na yenye tija,nimeongelea wireless ukiwa ni mfano tu.

Tupo pamoja ktk ku copy na kufanya marekebisho na mimi hicho ndicho naongelea na sio ku copy na ku pest kizima kizima.

Na nilichokua najaribu kuongelea ni miradi ambayo moja kwa moja inamsaidia mhusika kutoka chini ili aje avitumie vya juu,mfano huwezi mtu kumpa simu ya mkononi na ukampa masharti aitumie kuandika sms na kusoma sms wakati hajui kusoma na kuandika badala yake unatakiwa umfundishe kusoma na kuandika ndipo umpe simu ya namna hiyo.
 
So far, kunajamaa wamejaribu kurusha up to 6v for a distance of 1metre. Ambayo kwa kweli ni kidogo sana. Umbali ni mkubwa sana huko tz, vijiji vimetapakaa mno.

Pia ukitumia high frequecies, to try to transmit power you will FRY everything on the way! Just like the Microwave would do to you if you put your hand in there.

Hii mkuu vipi?
hebu tuwekane sawa sio ku transimit power signal ila una transimit ka-signal kadogo tu kenye power kidogo tu.

Haka kasignal kakafika una kaingiza kwenye power amplifier harafu hiyo signal inaingizwa kwenye transformer.

wapi ambapo kunashindikana ktk hili?
 
Mtanzania
Nimekuelewa ,Lakini swala na innovation unalosema haliwezekani ama nisahahu wenda si kweli maana juzi tu nimeona JK akifungua mradi kule tanga wa kufua umeme kwa kutumia mkonge(katani).

Umeongelea swala la SOLAR kushindwa kuongezeka hii ni kwa sababu za msingi kabisa sola ni bei ghari hapo ndipo ubunfu unatakaiwa uchukue nafasi yake ili huduma iweze mfikia mwananchi kiurahisi na kwa bei nafuu.

Mfano simu za landline pamoja na huduma zake zimeshindwa kumeet watumiaji wengi ama kwa sababu za kiufundi,kijografia n.k kwa mapungufu yake sio lazima tuyalizimishe badala ya ke wabunifu wamebuni simu za mkononi ili kukidhi mapungufu yake,na bado kuna mapungufu ya simu za mkononi bado wamebuni VOIP ili kukabiliana na mapungufu hatimaye huduma imufikie mhusika na kwa bei nafuu.

Hatuwezi ng'ang'ania Solar kama solar ilivyo maana tayari imeshaonyesha mapungufu kwa miaka sasa na ndio maana imeshindwa ku deliver na badala yake wataalamu wabunifu wanaweza tumia hiyo solar kurekebisha ama kuongeza na hatimaye huduma imufikie mlengwa kwa bei rahisi na yenye tija,nimeongelea wireless ukiwa ni mfano tu.

Tupo pamoja ktk ku copy na kufanya marekebisho na mimi hicho ndicho naongelea na sio ku copy na ku pest kizima kizima.

Na nilichokua najaribu kuongelea ni miradi ambayo moja kwa moja inamsaidia mhusika kutoka chini ili aje avitumie vya juu,mfano huwezi mtu kumpa simu ya mkononi na ukampa masharti aitumie kuandika sms na kusoma sms wakati hajui kusoma na kuandika badala yake unatakiwa umfundishe kusoma na kuandika ndipo umpe simu ya namna hiyo.

MkamaP,

Solar power ni aghali kwasababu serikali haijaipa kipaumbele. Inatakiwa waondoe ushuru na watengeneze incentives ili watu wengi zaidi hasa wilayani na vijijini watumie solar. Matokeo yake watumiaji wataongezeka, panels zote zitatengenezwa hapo hapo Tanzania na bei itashuka sana. Tunatumia muda mwingi kujaribu kupata pesa ya leo, badala ya kuwa na long term strategies ili kupata pesa nyingi zaidi kwa kesho kuendelea.

Matumizi ya katani kuzalisha umeme ni njia mojawapo lakini kuna njia zingine kama kutumia pumba za mahindi na mpunga kwa kazi hiyo hiyo.

Kule Kyela walikuwa wanamaliza miti kuchomea tofali, ghafla wamegundua pumba huweza kuchoma matofali sawa tu na miti na sasa wanatumia pumba. Inatakiwa iende zaidi ya hapo, watu watumie hizo pumba hata kupikia na shughuli zingine za maendeleo.

Ukiwa umetayarisha mazingira ya ubunifu, mambo hayo ni rahisi mno kuweza kutokea kuliko ilivyo sasa kwa Tanzania.

Kazi ya serikali lazima ibaki kutengeneza mazingira mazuri kwa wabunifu na wajasiliamali wengine. Hata kama kuna funding inatakiwa basi serikali itoe quarantee kupitia mabank badala ya wao kujihusisha moja kwa moja, yataishia kama ya mabilioni ya JK.

Mazingira ya TZ kwa mfanyabishara ni magumu mno, sasa kama wewe ndio unaanza ni magumu hata zaidi.

Nikisoma tatizo la Dr. Masua yaani liko wazi mno. Priorities zetu zimeenda mrama. Mtu anafikiri kupeleka watu India ni solution, eti ni bei rahisi. Kwanini wasikae na huyu mtaalamu wetu, wakamsaidia na wakakubaliana hata kupunguza bei? Wote tunajua faida za economies of scale, kama atakuwa na wagonjwa wengi itamwezesha kupunguza bei na kutoa mishahara mizuri kwa wafanyakazi wake. Ningelikuwa waziri wa Afya, ningelikuwa mtu wa kwanza kwenda kumwona Dr. Masua, wala nisingesubiri hata anifuate ofisini. Lakini ndio hivyo tena akili ni nywele na kila mtu ana zake, ndio maana wengine wanaendelea wengine tunabaki kutegemea wageni kutufanyia kila kitu.
 
Re: MKJJ; Excuse Me Sir...! What About Dr. Masau...?

Nakuomba Sir Mtsimbe unieleze kwa kina kupitia e-mail yangu kama una ushahidi wowote juu ya Serikali kusaidia wataalamu tangu kuanzia kipindi Kikwete. Achilia mbali kipindi cha Mkapa kwenda nyuma hadi Nyerere...

Ushahidi kuhusu serikali kuzima vipaji vya wataalamu na wataalamu wenyewe tunaona wazi kila siku kwahiyo usitake kutuchanganya kwa kutudanganya kwamba prezidaa anatusubiri. Labda anamsubiri mkewe na mahawara zake huko Ikulu lakini sio wataalamu wa nchi hii, prezidaa gani kila siku anapigwa fix kila siku ikiwa hiyo ni matusi ya juu kabisa kwa prezidaa kwa sasa achilia mbali mambo mengine yaliyotokea.

Wewe una uhusiano au ukaribu gani na huyo prezidaa kiasi cha kuwa na uhakika na tutachoongea au prezidaa atakachoahidi maana ni ahadi tu hapa zinatembea na hatujawahi kuona chochote. Pili utamgeuza vipi prezidaa aone sisi ambao mchango wetu haujaonekana kuwa wa maana uwe wa maana wakati walioonyesha michango yao kama akina akina Dr. Masau wamepigwa mgongo na serikali...??? nakuomba upeleke ujumbe kwa prezidaa aachane kwanza na mahawara na mafisadi ashughulikie mambo nyeti. Baada ya hapo mimi naahidi tutakuja kumwona mkuu, vinginevyo kama kuna wenye kiherehere cha kumwona huyo prezidaa bishoo mwizi na fisadi mkubwa basi wanaweza kwenda. Mimi sitaweza kwenda kuongea chochote maana sana sana nitajikuta nimemtukana nikakamatwa likaanza zogo lingine ambalo halikuwa kwenye ratiba na kufanya vyombo makini vya habari kuuza magazeti.
 
Mkuu,

Looh! nimesoma ujumbe wako na kucheka sana. Labda ni kweli inabidi tuchukie sana ili japo mabadiliko ya aina fulani yatokee.

Muhimu ni kuto kukata tamaa tu maana mabadiliko tunayotaka yafanyike ni kwa faida ya Watanzania wenzetu na wala sio JK ambaye tayari ana bilioni zake kaficha sehemu.

Tuendelee kuhangaika hata bila ya msaada wa serikali. Suala la Dr. Masua kwa kweli linasikitisha sana.
 
Wakuu,

Nawapata sana. Niko Dodoma kikazi na pia jana Sunday tulikuwa tunafungua TPN Chapter Dodoma. Nitakapopata nafasi wakati wowote, nami nitaendelea kuchangia wakuu.

Kila la kheri
 
mimi naunga mkono hoja ya TPN kumwona na kukumkumbusha kuhusu hiyo hotuba yake kwa wasomi jinsi ya kujiwezesha. Raisi ana mambo mengi na wasaidizi wake wa karibi si wakweli sana kwake kumpa UKWELI WA MAMBO. akumbushwe kwa kuonana naye na iwe ni movement iliyo systematic through TPN and we can make a difference. Vijana wa sasa ni watekelezaji tusiige UBABAISHAJI. Mtsimbe tusonge mbele kwa hoja.
 
Back
Top Bottom