kinepi_nepi
JF-Expert Member
- Aug 16, 2007
- 869
- 239
Raisi wa Jamhuri ya Watu wa Tanzania atawasili Houston, Texas USA kwa ziara ya siku mbili kuhudhuria ufunguzi wa DICOTA iliyoandaliwa na baadhi ya watanzania waishio marekani wakishirkiana na balozi Sefue. Dicota inasemekana ni mchakato wa kukusanya na kutafuta wawekezaji walioko Marekani na kuwaunganisha na Tanzania.
Wanaohudhuria mkutano huo ni pamoja na balozi Sefue balozi wa tanzania nchini marekani pamoja na maofisa ubalozi, Bernard Membe waziri wa mambo ya nje wa Tanzania, Mr Emmanuel Ole Naiko(TIC) na msafara wa raisi na ule wa waziri wa mambo ya nje pamoja na TIC.
Ni mwaka mmoja tu tangu kikao cha kwanza cha chombo hiki kufanyika nchini marekani jijini Houston na iliwahusisha maofisa mbali mbali kutoka tanzania na ubalozi wa Tanzania nchini marekani, na safari hii karibu sura zote zinarudi tena houston safari hii na raisi anaonekana atajumuika nayo. Chanzo cha habari hii ni mwaliko uliopo kwenye website ya DICOTA inayoonyesha wageni wote waalikwa akiwemo mheshimiwa raisi.
Safari hii ni mjumuiko wa safari za Raisi zinazopigiwa kelele nyingi na watanzania kuwa amekuwa na safari nyingi zinazoitia nchi hasara. Kumsafirisha Raisi wa nchi kwa ajili ya ufunguzi ni gharama kubwa sana kwani fedha anazotumia yeye na msafara wake ungeweza kujenga clinic kadhaa nchini.
Mkutano wa kwanza uliofanyika Houston inasadikika ulifadhiliwa na fedha za walipa kodi wa tanzania na kusafirisha viongozi mbalimbali kutoka ubalozini na TIC tanzania, na hakuna anayejua ni kiasi gani kilitumika. Au nini walikiongea au walikipata. Hii imekua ni kawada ya nchi yetu kutumia fedha za walipa kodi bila ya kutangaza matokea ya matumizi hayo kwamba tumeliwa au tumepata faida.
Habari za kichunguzi zinaonyesha kwamba huu ni mradi wa baadhi ya viongozi wa kutengeneza safari za nje kwa kisingizio cha mikutano na hivyo kujiongezea vipato kwa ile staili ya malipo ya safari na kujikim pamoja na marupurupu ya safari. haiingii akili kama nia ni kuwapata wafanyabiashara, kwa nini balozi asifanye hizi kazi na kutembea sehemu mbali mbali ndani ya eneo lake la kazi na kutangaza nchi huku akitoa maelezo ya maeneo ya uwekezaji. Kwanini kuhamisha wizara na taasisi za kiserikali na kutumia gharama kubwa kila mara kwa kisingizio cha kutafuta wawekezaji.
Kinacho shangaza ni pale viongozi wanzilishi wa chombo hiki pamoja na Balozi sefue kwa makusudi kutowaambia watanzania kupitia vyama vyao vya majiji na majimbo ya Marekani kwamba chombo hiki kimeanzishwa. Inaonekana kwa sasa wanahitaji watanzania kuhudhuria sana mkutano huu ili kujaza ukumbi. Wanzania waishio Marekani wanasema kuna vyama vya watanzania vingi Marekani na kama vingeshirikishwa zoezi hili lingeweza kuwa na manufaa zaidi. Kwani watanzania wengi wanafanya kazi mbali mbali kwenye makumpuni mbalimbali na kuwa na info tofauti. Viongozi wa vyama vya watanzania wanashangaa kwa kutoshirikishwa kulitafutia Taifa wawekezaji na Balozi Sefue kuamua kutafuta kajikundi kwa ajili ya kupitishia sera zake.
Tangia waanzishe DICOTA na kuleta ujumbe mzito sana je ni mangapi tayari yamefanikiwa au wawekezaji wangapi wamepatikana na kuona uwezekano wa kulipa gharama zinazotumika za mamilioni ya shilingi kwa kisingizio cha utangazaji.
Wakati viongozi wanchi wakinadi kutafuta wawekezaji huku nyumbani umeme hautapatikana kwenye mikoa kama sita hivi, Mwanza, Kilimanjaro,Dodoma,Arusha, Shinyanga na Tabora. Tatizo la umeme naona linakuwa sugu. Ni mwekezaji gani atawekeza gizani?
Wazo la DICOTA ni zuri sana na linaweza kuisaidia nchi kwa kiwango kikubwa, ila likiendeshwa kiutapeli au kiujanja ujanja linaweza kuliiingizia Taifa gharama kubwa sana.
Naomba kutoa hoja.