Kamanda Francis
JF-Expert Member
- Nov 30, 2013
- 834
- 140
Waheshimiwa nawasalim, poleni na Majukumu,
Mimi naitwa Mohamed Edward Malele ni Mkazi wa Mwanza.
Waheshimiwa, hii ni mara yangu ya tatu najitokeza hadharani Kuomba Kuonana nanyi Uso Kwa Uso Ili niwaelezee Ukweli halisi wenye Ushahidi wa Wazi Kuhusu Tukio la Kifo Cha Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Mwanza marehemu Liberatus Barlow.
Nimewahi Kuhojiwa na Gazeti la Jamhuri Tolea No:81 la Tarehe 21-27, Mei, 2013 na Toleo No:83 la Tarehe 28 Mei-3 June 2013 lililokuwa na Kichwa Cha Habari "MTANDAO WA MAUAJI YA BARLOW WATAJWA NA IGP MWEMA AMPA HIFADHI MUUAJI WA BARLOW". Lakini baadaye nilisikitishwa na Kauli ya Jeshi la Polisi Kupitia Kwa Msemaji wa Jeshi hilo Advera Senso Kwa Vyombo vya Habari Iliyodai Kwamba Mimi nilikuwa na Matatizo ya Kiakili.
Nakanusha leo hadharani mbele ya Umati wa Watanzania wa Eneo la Kemondo Jijini Mwanza Kwamba "Mimi Sikuwa na Matatizo ya akili, mimi nina akili timamu Isipokuwa Waliyasema hayo Ili Kufunika Ushahidi nilionao Kuhusu hili tukio nyeti".
Ni Mimi Mohamed Edward Malele wa Mwanza.
====================
*Mada imefungwa hadi pale itakapo bainika madai ni ya kweli na mrusha mada ndiye Mohamed Edward Malele ni Mkazi wa Mwanza.
JamiiForums.
===================