Mdondoaji;800150Kusema la haki mnyonge mnyongeni but haki yake mpeni. Kikwete kuna mazuri aliyoyafanya. Mosi hii nadharia ya utawala bora na misingi ya utawala bora isingelikuwapo ndani ya midomo yetu isingelikuwa kuwapo kwa uhuru wa vyombo vya habari (Big Ben alikuwa akisikia umemsema anatuma majasusi kukumaliza). Ndio maana hii leo tunaweza kuzungumza EPA, Import support, Radar ni kwasababu ameruhusu transparency katika utawala wa serikali.
What you mean kwamba nadharia ya utawala bora isingekuwepo?Unamaanisha JK ndiye aliyeleta nadharia hiyo?By the way,tunachohitaji sio nadharia bali vitendo.Kuna umuhimu gani wa kuwepo nadharia isiyofanyiwa kazi?Do you think JK angekuwa muumini wa nadharia hiyo tungeendelea kujiuliza Kagoda ni mdudu gani?Au unadhani angeruhusu ufisadi wa Richmond umalizwe kishkaji?Au angeendeleza indefinite deadline ya walaruShwa alodai anawafahamu?Na vipi kuhuu wale mafisadi wa Bandarini Dar aliosema anawafahamu na hajapeleka majina kwa wahusika hadi leo?
Kwa akili yako,unaona kuzungumzia EPA,Import support,Radar,na skandali nyingine kama hizo inatosha kumpongeza JK.Hebu jiulize,kuzungumzia huko kumebadilisha nini so far?Majambazi wa EPA bado wanatesa (I mean wahusika wakuu like Kagoda),Import support imeendelea kuwa ngonjera,Rostam anadaiwa mahela kibao na hajalipa hadi kesho,na kama ishu ya Radar Chenge ndio huyo bado mwenyekiti wa kamati ya maadili CCM!
Tatizo lako unadhani uhuru wa kuongea ni privilege anayotoa mtawala.Huo ni mtindikio wa upeo.That's your natural right,ndugu.
Pili amepitisha muswada wa kuseparate biashara na uongozi ambacho kimesaidia kupunguza walafi serikalini. Hii itasaidia hata wabunge wajao wafikirie waendelee na uongozi wa ubunge au wafanye biashara. Kwa hilo nakubaliana nae sana tu na namuombea lifanikiwe tutapata kuondoa pathetic leaders kama kina Lowassa katika serikali ambao wanakaa kwa maslahi yao binafsi.
Amepitisha Mswada?You mean JK amekuwa Bunge?Hivi unaelewa miswaada inapitishwaje?
Na hata angepitisha,you should remember survival ya CCM inategemea wafanyabiashara wenye fedha chafu.Na hata bila hilo,CCM ni moja ya taasisi inayojishughulisha na biashara ambazo kimsingi ni mali ya watanzania wote e.g. viwanja na kumbi mbalimbali nchini.Sasa unapozungumzia kutenganisha siasa na biashara inamaanisha CCM yenyewe iwe ya kwanza kuachana na biashara,au ichague biashara na kuacha siasa.Unless unataka ku-underline ule msemo wa kibiblia kuwa "fuateni ninachosema lakini sio ninachotenda".
Tatu infrastructure economy nani asiyeona idadi ya barabara zilizojengwa dar acheni kumsema huyu mbagamoyo kuna barabara kibao kilwa road kwenda mbagala, vingunguti, mikoa ya kusini lami tupu kitu ambacho kinasaidia uchumi wa nchi. Upanuzi wa bandari utakuza uchumi na pamoja viwanja vya ndege. Nia na madhumuni ni kwamba Tanzania iwe ni business centre. Just ask yourself why?? Tizama ni nchi iliyokuwa na financial and political stability in the past decade kwa east and central africa. Jibu unakuta ni bongo tu. Tizama the amount of FDI zilizowekeza Tanzania compare to the rest of East Africa. Kwa kweli amejitahidi but nadhani amekosa watu innovative kujaribu kuleta mabadiliko ya kiuchumi kwani pamoja na mafanikio haya yamekuwa overshadow na viongozi walafi ambao wanafikiria kujinufaisha wenyewe without kuangalia wananchi matokeo yake pesa nyingi za maendeleo zinaenda mifukoni mwa watu
.
Kwa mtizamo wa aina hii CCM itatawala milele.Yani wewe kigezo cha maendeleo ni hizo barabara za hapo Dar.Umeshafika kijijini?Kwa akili yako,Tanzania means Dar es Salaam.Kigoma,Lindi,Mtwara,nk kwingine kulikosahaulika ni irrelevant.Na hizo barabara za Dar zimewasaidia vipi wakulima kusafirisha mazao yao?
Hiyo business na financial stability unayozungumzia ni kupanuka kwa empire ya akina Rostam au yale mabilioni ya JK ayaliyoishia mifukoni kwa mafisadi?Au unazungumzia stimulus package ya kisanii ambayo hatuelewi imetumikaje?
Halafu angalia unavyojiumauma.Sasa angekuwa kiongozi mahiri kama unavyojaribu kutuonyesha,how come then awe overshadowed na viongozi walafi kama yeye ni msafi?Kwani hao viongozi walafi alirithishwa au aliwateua yeye mwenyewe?
Tuje katika social welfare. Recently BOT walipewa pesa na World Bank kwaajili ya kuendeleza makazi mazuri ya mtanzania wa kawaida na kipato cha chini. Hizi pesa kama zitatumika inavyotakiwa na kutakikana basi makazi ya wananchi wa kawaida yataboreka (na sio makazi ya wafanyakazi wa BOT na mabosi wao). Kimsingi kama watatumia hizi pesa inavyotakiwa maisha bora ya mtanzania yatakuwapo na sio hivi sasa. Pia matumizi ya IT (Information Technology) ni jambo la kupewa heko kwani itaboresha mawasiliano, biashara na huduma za kibenki.
BOT my a*s.Hao majambazi wanaotumia mabilioni kuboresha makazi yao na huyo JK unayemsifia kakaa kimya kana kwamba ni ubadhirifu huo ni sera ya serikali yake!?Usiwe mzembe wa tafakuri.Tatizo sio kupewa misaada.Tumekuwa tukipewa misaada tangu tulipopata uhuru.La muhimu ni inatumikaje.Na hapo ndipo umuhimu wa uongozi bora unapohitajika.Misaada inatolewa inaishia kujenga mahekalu kwa mafisadi na kuongeza idadi ya nyumba ndogo zao,ma ma-vogue ya kutesa kwenye hizo barabara unazosifia hapo Dar!
Watatumiaje vizuri fedha hizo wakati huyo rais mwenyewe ni maarufu zaidi kwa kuuza sura na kuchekacheka majukwaani badala ya kuwachukulia hatua wanaoofanya ubadhirifu wa fedha za umma?
Maendeleo ya teknohama yanawanufaisha vipi walalahoi wasio na uhakika wa their next meal?Na ni walalahoi wangapi wanaomudu gharama za maunganisho ya intaneti (kwa mfano) licha ya majigambo ya JK wakati anazindua high-speed internet connectivity ya chini ya bahari?
Hayo ni baadhi tu mengineyo watajazilia wengine ila tatizo la Kikwete ni anashindwa kuweka msimamo wake na ndio kitu kinachofanya mafanikio yasionekane.
Sasa mbona mwenzetu umeweza kuyaona mafanikio yake japo unasema kinachofanya yasionekane ni kushindwa kwake kuweka msimamo?Na kiongozi gani mahiri asiye na msimamo?
Katika uongozi kama maisha kuna watu watakupenda na wengine kukuchukia but la msingi tanguliza misimamo yako. Kikwete anaogopa kuudhi watu akihofia ubadhirifu wa kiongozi but hilo ndio linalopelekea kukosekana uadilifu katika uongozi, watu kutoona mafanikio yake na mwishoe kudharaulika maana haongozi bali anaongozwa.Kikwete angelitanguliza misimamo yake wasingelikuwapo mawaziri wabovu kama akina simba kwani angelichagua mawaziri wanaokabiliana na misimamo yake na sio vengine
. Ahhaa,kumbe unafahamu fika kuwa JK ni kiongozi dhaifu lakini bado unamtetea kwa hoja za kujiumauma!
This I hope kama atachaguliwa tena 2010 hatalirudia ama sivyo atakumbukwa na legacy ya kiongozi asiyekuwa na msimamo !!!!
Huu ni outright upuuzi.Yani what you're suggesting ni kwamba achaguliwe tena ili arekebishe makosa yake ya kukosa msimamo!Hivi laiti nchi yetu ingekuwa binti yako,ungeweza kufanya majaribio ya kipunguani kama hayo?Say,kumruhusu binti yako azae na mtu mwenye ukimwi na kuangalia kama kitoto kitachozaliwa kitakuwa kimeambukizwa au la!Na kitoto kikizaliwa kimeambukizwa,what would you do?It's just exactly the same na unachojaribu kushauri hapa.Tumpe tena JK awamu nyingine kwa matarajio kuwa atarekebisha makosa yake.What if kama hatorekebisha?Tutarejeshaje miaka mitano (actually ni 10) tuliyopoteza kwa kumweka madarakani rais wa majaribio?
Na vipi kama baada ya kumpa tena nafasi JK,tunaishia kubaini kuwa kila raslimali ya nchi yetu imeuzwa kiufisadi,just like tulivyobaini ujambazi wa Mkapa baada ya kutoka Ikulu?Lawama kuwa "aaah tatizo la JK hakuwa na msimamo" zitasaidia nini wakati huo?
KAMA AMESHINDWA KATIKA MIAKA MITANO INAYOISHA HIVI PUNDE,ATAWEZAJE KWENYE MIAKA MITANO IJAYO?Kwa wishful thinking zako?