Rais kukukumbusha maono yangu ya kulifanyia kazi eneo la Jangwani. Vizazi vitakuingiza katika kundi la mashujaa moja kwa moja

Rais kukukumbusha maono yangu ya kulifanyia kazi eneo la Jangwani. Vizazi vitakuingiza katika kundi la mashujaa moja kwa moja

NIMEONA

JF-Expert Member
Joined
Aug 4, 2019
Posts
3,862
Reaction score
5,693
Hili ono haliishi kunijia, nami, kwa upendo mkuu, nakufikishia Rais wangu mpendwa.

Tafadhali fanya kitu pale jangwani; ondoa mateso ya mafuriko kila mwaka tangu tupate uhuru na badala yake ligeuze liwe eneo la kufurahi na kiuchumi, yaani 'kijiutalii' fulani hivi.

Mama uwezo (fedha au mbinu za kupata fedha) unao, sababu unayo (watu wanateseka) na nia (moyo mwema) unao nami mwananchi wako nakuongezea na kukukumbusha umoyo mwema hapa, nakazia.

Mama ukifanya hilo vizazi vitakukumbuka daima na wale wasiokukubali kama bashiru na polepole hawatokuwa na jinsi bali kulitaja jina lako kila ubinadamu utakapotajwa!

Nawasilisha, kwa mara nyingine tena!
 
Hili jukwaa limeharibiwa na walimu, nimesema mara nyingi hii. Ona sasa hiki kinachoandikwa hapa. Ushauri gani huu kwa raisi?

Jangwani nj waterlogged, sana Sana huu ushauri unataka kuingiza watu chaka. Sehemu Kama hiyo haiwezi kubadilika matumizi labda zitumike bilion nyingi sana kulibadilisha hilo eneo na kuacha asili yake. Hizo billions zote za nn ikiwa tuna mahitaji mengi?

US nchi iliyoendelea kiteknolojia hadi leo hii miji yake mingi tu inakumbwa na mafuriko. Unafikiri ni rahisi sana kudhibiti waterlogged areas?
 
Hili jukwaa limeharibiwa na walimu, nimesema mara nyingi hii. Ona sasa hiki kinachoandikwa hapa. Ushauri gani huu kwa raisi...
Utakuwa una matatizo ya kijinsia wewe, si bure!
 
Wewe usitafute sehem yenye makaz bora uhamie endelea kuota ivo ivo na maono yako ya mchongo..
Ilo eneo linahitaj gharama kubwa sana kubadili uasili wake ambao sidhan kama unatija yoyote kwa kulingana na gharama itakayowekwa hapo
 
Back
Top Bottom