Rais kuteua makada UVCCM kuwa Wakurugenzi ni kuvuruga Utumishi wa Umma

Kama haya ndiyo majukumu ya DED basi maDED wote wawe either WACHUMI ama WAHASIBU.
Kiutaratibu ilikua wanapandisha vyeo kwa aliyekua Muhasibu wa halmashauri (DT)/Mchumi wa halmashauri/Afisa mipango wa halmashauri/Afisa utumishi wa halmashauri (DHRO) au mwanasheria wa halmashauri

Ila toka 2015 tukaanza kudemka
 
Duuuuhh.
Kazini kuna wasomi na wabobezi wenye uzoefu kwenye mambo ya management lakini hawajateuliwa kwakuwa si wanaccm
Yaani huu ni upumbavu mkubwa sana,hao makada waliowachukua wangewapa U-dc tu,Kuwa Ded unatakiwa kuwa mtendaji na sio mwanasiasa,halafu kuwa Ded unatakiwa uwe ni mtumishi wa umma ambae umepitia kuwa mkuu wa idara ama kitengo chochote na pia sifa mojawapo ni lazima uwe umefanya kazi si chini ya miaka 10 taasisi za Umma ama binafsi
 
Hapana..katiba sio mwisho wa matatizo..unaweza kuja na katiba mpya na bado watu wakaikanyaga pia..jambo la msingi ni kuchagua watu wenye weledi
Unaweza kudhani una akili kumbe ni sivyo. Kama jambo la msingi ni kuteua watu wenye weledi mbona hajawateuwa sasa? Si ndiyo jambo la msingi uliloona wewe? Kama habanwi na sheria yoyote unadhani atachague watu wenye weledi? Kazini kunakuwa na kanuni na sheria ili watu wasijifanyie watakavyo. Bila katiba mpya ya kubadilisha utaratibu wa namna hao wateule wanavyopatikana unadhani atabadilika. Na inapondikwa katiba mpya inaandikwa kiasi ambacho kama kuna rais anataka kuikajaga kuwe na ugumu na siyo kama sasa. NB: Katiba haiwezi kuwa mwisho wa matatizo lakini ni mwanzo mzuri wa kujenga msingi.
 
Ila mkitumia hicho kigezo vipi wengine kujifunza na ku grow, watumishi wengi wa umma ni magoi goi flani na wamezoea kufanya kazi bora liende tu. So kuchaganya watu tofauti tofauti sio mbaya. Walio kwenye miradi ukifanya na watumishi wa umma wako lazy sana bora liende tu bora kuwe na mixture flani hivi
 
Watajifunza kwani wapo wale wenye uzoefu kisha wanashika hatamu.

Nadhani wazo la raisi ni kutaka kuona mabadiliko ya fikra.

Kuna watu wapo wilayani humo miaka nenda rudi ukimuuliza amebuni njia zipi sahihi za kuleta mapato wilayani atapiga kiswahili atazungurusha wee.

Kwa mfano, namna ya kupata kodi katika maeneo ambayo hakuna ofisi za TRA ni kutafuta njia ya kupata fedha hizo maana zipo.

Yaani kutumia akili na elimu ulopata.
 
Kama hata hewa wamepangiwa vituo, ya nini kwa hao watu kabisa!? Ndio kuchomekea!! Work experience counts
Magufur hakupenda kuchomekewa majina na kupelekewa vimemo
 
Mkuu hata hawa wengine wapya hakutakuwa na tofauti. Trust me. Sababu zinazofanya hao wengine kuwa magoigoi ndiyo hizi hizo zinakwenda kufanya hao wapya wawe hivyo. Hawa watu walitakiwa wawe wanabanwa na sheria kanuni ili wasiwe magoigoi. Tubadilishe wanavyopatikana na jinsi wanavyopimwa kwa kazi. Tufumue mfumo!
 
Bora hata huyo kachagua makada wengine wanateua mademu zao kuwa viongozi tuna mifano mingi
 
Ndiyo. Huku ni kinajisi kabisa utumishi wa umma. Mbaya zaidi utaratibu huu unawavunja moyo watumishi wa umma.
 
Kwa maoni yangu, serikali isione aibu, pangia hawa watu wasio na sifa majuku mengine mara moja. System

Upo sahihi kabisa kuhusu makada wa chama cha CCM na naongeza kwa mfano hai kwenda ktk tovuti za serikali za mikoa na Mitaa kuona Dhima ya serikali za mitaa zinakinzana na utawala wa CCM unaoabudu 'ubaguzi wa kisiasa na kiitikadi, kupuuza haki ya utu, kutopeleka miradi mfano ujenzi wa barabara maeneo ya wapinzani , kushiriki ktk uchafuzi wa chaguzi n.k' :

Serikali za Mitaa​

Mkoa wa Dar es Salaam una Halmashauri za Manispaa tano (5) ambazo ni Ilala, Kinondoni na Temeke, Ubungo, Kigamboni na Halmashauri ya Jiji. Halmashauri za Manispaa pamoja na Halmashauri ya Jiji zinaongozwa na Wastahiki Mameya ambao ni Wenyeviti wa Halmashauri, kwa kushirikiana na Wakurugenzi ambao ni Watendaji wakuu wa Halmashauri husika.

Halmashauri za Manispaa za Mkoa wa Dar es Salaam pamoja na Halmashauri ya Jiji hutoa huduma za kiuchumi zikiwepo Kilimo, Mifugo, Misitu, Uvuvi, Miundombinu, Huduma za jamii kama Afya, Maji, Elimu, Maeneo ya burudani, Mazishi, Mipangomiji, Kutunza mazingira, Ustawi wa jamii, Ushirika na mambo mengine yanayoihusu jamii na Taifa kwa ujumla.

Utawala bora ni suala linalotekelezwa na Halmashauri zote katika nyanja za:​

  • Demokrasia
  • Ushirikishwaji
  • Utawala wa Sheria
  • Uadilifu wa viongozi na wafanyakazi wa Serikali za mitaa
  • Uwazi na Uwajibikaji
  • Ufanisi katika utendaji kazi
  • Mchakato wa kijinsia
  • Upangaji mipango
  • Ujuzi wa upangaji Mipango kwa kutumia Rasilimali zilizopo
  • Utekelezaji wa Mipango.

MAJUKUMU YA SERIKALI ZA MITAA:​

Halmashauri za Manispaa zimeanzishwa chini ya sheria za Mamlaka za Miji (Local Government Urban Authorities Act. 1982). Majukumu makuu ya Serikali za Mitaa yaliyofafanuliwa na sheria hiyo ni kama ifuatavyo:-

  • Kusimamia na kudumisha amani ulinzi na usalama katika maeneo ya mipaka yake.
  • Kuhamasisha/kuendeleza na kuwapatia huduma bora za kijamii na kiuchumi wananchi walio katika eneo la mipaka ya Halmashauri.
  • Kusimamia sera za maendeleo ya kiuchumi na kijamii katika maeneo yao.
  • Kuchukua hatua madhubuti za kuhifadhi na kuendeleza mazingira.
  • Kusimamia utawala, fedha, mambo yote ya uendeshaji katika ngazi mbalimbali zilizo ndani ya mamlaka ya Halmashauri ya Manispaa/Jiji.
  • Kusimamia na kuhakikisha demokrasia inadumishwa katika jamii.
  • Kukusanya mapato yatakayowezesha Mamlaka ya Serikali ya Mtaa kuendesha shughuli zake pamoja na kutoa taarifa za matumizi kupitia kamati mbalimbali.
  • Kutoa huduma mbalimbali za kiuchumi na kijamii pamoja na kutekeleza shughuli za maendeleo katika maeneo yao.
  • Kuzingatia na kutambua masuala mtambuka kama vile Jinsia.
  • Kuendeleza na kusimamia kanuni za biashara, viwanda, kilimo n.k.
  • Kusimamia na kuendeleza huduma za Afya, Elimu, Maji, Utamaduni na masuala ya burudani katika jamii.
  • Kubuni mikakati ya kupambana na umaskini pamoja na mbinu za kusaidia kuboresha maisha ya vijana, wazee, walemavu n.k.
 
Utamaduni wa kuteua makada wa CCM kuwa maded na ma dac aliyeuanzisha ni Magufuli. Wakati wa Kikwete jambo hili halikuwepo kabisa. Acha kumsingizia Kikwete kwa dhambi hii.
 
Cha ajabu amewatoa watu muhimu sana Ili kupachika Hawa wapuuzi
 
Ndiyo. Huku ni kinajisi kabisa utumishi wa umma. Mbaya zaidi utaratibu huu unawavunja moyo watumishi wa umma.
Try to be constructive katika hoja yako.

Ni kwa vipi utumishi wa umma wanajisiwa na ni vipi watumishi wa umma wavunjwa moyo?
 
Hata jpm wako ndio alianzisha huu upuuzi,alikaza makada wote kwenye hizo nafasi.

Rais kazingua Sana ,Hawa si angewateua kwenye nafasi za karibu tarafa au Ma DAS
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…