Rais kutokupokelewa na Rais mwenzake: Tutofautishe kati ya State Visit (Ziara ya Kitaifa) na Working Visit (Ziara ya Kikazi)

Kabisa. Tena akija Biden Jo; tutamuelekeza madame akapige stori na Bi Sandra (mama ake Diamond) au kwa mama ake Zuchu.....over
Subutuuu. Heeeeeee, barabara zitapigwa dekiiii, media zitalindimaaa kama zoteee
 
Rais ni Rais tu, state visit na work visit ni jambo lile lile tu, tuache ujuaji mwingi.
Mbona katika "wprk visit" ya hivi karibuni huko USA aliweza kukutana na US Vice President.

Kwa hiyo basi uwepo wa Rais wa nchi moja katika ardhi ya nchi nyingine kwa vyovyote vile ni suala lenye kuhusisha itifaki ya kimataifa na pia ya kidiplomadia kwake yeye binafsi na msafara wake wote.

Na hii ndiyo sababu ya uwepo wa ofisi ya ubalozi katika nchi husika. Rais hawezi kwenda ziara ya kikazi katika nchi nyingine kienyejienyeji tu.

Sent from my Nokia 2.3 using JamiiForums mobile app
 
Naona kuna utofauti kati ya Ziara ya kikazi AfDB na ziara ya mwaliko toka serikali ya Ghana. Pengine jinsi vyombo husika vinavyotoa habari huchanganya wasomaji na kushindwa kuelewa dhumuni la safari, shughuli gani itafanywa na nani ametoa mwaliko n.k


23 May 2021​

MOZAMBICAN PRESIDENT ARRIVES IN GHANA FOR STATE VISIT




The President of the Republic of Mozambique, Filipe Jacinto Nyusi, has arrived in Ghana on Sunday for a four-day state visit, ending Wednesday 25 May 2022.

President Nyusi was met on arrival at the Jubilee Lounge of the Kotoka International Airport (KIA) in Accra by Ghana’s Vice President Mahamudu Bawumia.

President Nyusi will officially commence his visit with a meeting with Ghana’s President Akufo-Addo, at the Jubilee House this Monday 23 May 2022.

The President will also pay a visit and lay a wreath at the Kwame Nkrumah Mausoleum.

Also on the agenda of the visit of the Head of State is participating alongside President Akufo-Addo inthe opening ceremony of the African Development Bank Group’s 2022 Annual Meetings, being held from 23-27 May in Accra. President Nyusi will also pay a courtesy visit to the AfCFTA (African Continental Free Trade Area) Secretariat, as well as to the Parliament of the Republic of Ghana.

On this State Visit, President Nyusi is accompanied by the Minister of Foreign Affairs and Cooperation, Verónica Macamo; the Minister of Economy and Finance, Max Tonela; the Minister of Agriculture and Rural Development, Celso Correia; by the Deputy Minister of State Administration and Public Service, Inocêncio Impissa; deputies of the Assembly of the Republic; members of staff of the Presidency of the Republic and other State institutions.

ALSO READ: AfDB’s 57th annual meetings to kick off in Accra on Monday



Source: Asaasse Radio / O País

24 May 2022
Accra, Ghana

AFRICAN DEVELOPMENT BANK ANNUAL MEETING IN ACCRA 2022

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akiwa amesimama na Rais wa Ghana Mhe. Nana Akufo-Addo, Rais wa Msumbiji Mhe. Filipe Nyusi, pamoja na Rais wa Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB) Dkt. Akinumwi Adesina wakati wa nyimbo za Taifa zikipigwa kabla ya kuanza kwa Mkutano wa 57 wa AfDB unaofanyika katika ukumbi wa Kimataifa wa Mikutano wa Accra nchini Ghana tarehe 24 Mei, 2022
 
Usiifananishe USA na nchi nyingine. Hata Obama akija hapa leo kuangalia Tembo atakaribishwa magogoni.
 
Achana na Biden, hata wakija Obama au Bush kufanya utalii tu magogoni lazima watinge.
Hivi raisi wa marekani anaweza akaja hapa nchini akamaliza mwezi mzimaaa bila kuonana na samiaa??
 
Kwahiyo rais wa Marekani akija kwa work visite, Samia atauchuna ikulu hata enda kumpokea??
Hatalazimika kwenda kumpokea, wala rais wa marekani akija kwa work visit hatadai kupokelewa na Rais! Lakini kwa kawaida sijui kwa nini (labda kwa ajili ya ukarimu), ikulu hapatakalika itabidi tu aende kumpokea! Si unajua sisi waafrika tunajisikiaga vizuri kupokea wageni!
 
Hivi raisi wa marekani anaweza akaja hapa nchini akamaliza mwezi mzimaaa bila kuonana na samiaa??
Work visit haina maana hatakiwi kuonana na Rais, ila Rais hawajibiki na ujio huo!! Japo kwa kawaida hizi nchi za ulimwengu wa tatu huwa zinawashobokea sana marais toka nchi tajiri!! Kwa sababu mshoboko tu itabidi program nyingi za rais zisitishwe ili ampokee huyu mgeni ambaye kimantiki hahusiki naye!

Lakinin niseme jambo moja, usitegemee Rais wa Marekani aje bongo kwa work visit!! Labda Rais mstaafu!!! Work visit mara nyingi zinawahusu watendaji na si mkuu wa nchi!! Ukiona Rais ana safari nyingi za nje za work visit HAPO KUNA TATIZO!!
 
Sawa tumekuelewa,ila Rais anapokelewaje na mtu amevaa safety boots?Au hii nayo ni sheria ya working visit Kwa maana ya kazi kazi?
Hakuna hata dress code Kwa watu wanaompokea Rais,wale wa Ghana walivaa kishkaji sana.
Usalama wa mkuu wetu wa nchi ukoje huko nje ya nchi?Huko nje hatuoni hata mtutu wa bunduki,ngoja awe nchini,utasema tuko Somalia!!!!
 
Work visit bado siyo kienyeji!! Lakini Rais akienda nchi za nje kama work visit HAHESABIKI KAMA NI MGENI WA KITAIFA!! ASITEGEMEE KUPOKELEWA NA MKUU WA NCHI!! ASITEGEMEE KUPIGIWA MIZINGA!! ASITEGEMEE KUKAGUA GWARIDE LA KIJESHI!! Hii ndiyo hoja iliyopo!! Watu wamekuwa wakijiuliza kwa nini mama akienda nchi za nje mara nyingi hapokelewi na Rais mwenzake!! Majibu yametolewa kwa ufafanuzi wa kina kwenye post namba 1 ya uzi huu. Nchi alizotembelea kwa State visit alipokelewa na Rais!! Mfano mzuri ni alipotembelea Kenya!!
 
Hayo ni makosa ya balozi wetu wa Ghana, maana kwenye work visit balozi inabidi ahusike sana kuandaa mapokezi ya bosi wake, akishirikiana na wale ambao rais atahusika nao kwenye ziara hiyo ya kikazi. Ilibidi awaandae pia watanzania walioko huko wampokee kwa shangwe na mambo kama hayo!
 
 

Attachments

  • Screenshot_20220524-202751.png
    145.5 KB · Views: 11
  • Screenshot_20220524-202708.png
    156.8 KB · Views: 11
Bado balozi ni mteuliwa na mwakilishi wa Rais!Pia Rais ana team yake ambayo nadhani wanatakiwa waconfirm na balozi kama maandalizi yamekamilika!
Haya,naomba unijibu kuhusu masuala ya kiusalama!
 
Acha kudanganya na kulisha watu matangopori. Hakuna tofauti ya work visit na state visit kwa Rais.
 
Bado balozi ni mteuliwa na mwakilishi wa Rais!Pia Rais ana team yake ambayo nadhani wanatakiwa waconfirm na balozi kama maandalizi yamekamilika!
Haya,naomba unijibu kuhusu masuala ya kiusalama!
Hoja ya msingi iliyopo ni Rais kutokupokelewa na Rais mwenzake!! Watu walikuwa wanahoji ni kwa nini?? Jibu ni kwamba Rais wetu yuko kwenye work visit na SIYO STATE VISIT!! Kwenye work visit Rais mwenyeji HALAZIMIKI kumpokea Rais mwenzake, HALAZIMIKI KUMTUMA AFISA MWINGINE aende kumpokea!! Anaweza kwenda kumpokea KWA MAPENZI YAKE mwenyewe lakini SI WAJIBU WA KIKAZI!! Logistics zingine zote anatakiwa ashughulikie balozi wa Tanzania (kwa mfano) aliyeko Ghana kwa kushirikiana na mamlaka mbalimbali za nchi anakotembelea Rais yakiwemo masuala ya kiusalama!!

Kwenye state visit kila kitu kinapangwa na ikulu ya nchi mwenyeji, na balozi wa nchi anakotoka Rais anakuwa ni mmoja wa waalikwa rasmi tu kwenye kumpokea Rais.
 
Kwahiyo work visit inahalalisha Rais kupokelewa kihuni namna Ile?Mimi sipo kwenye hizo tofauti za visits,I'm concerned na jinsi Rais anavyoshushiwa heshima Kwa kupokelewa na watu wamevaa kihuni kihuni tu!
Hata kama ni work visit,basi hata waziri wa mambo ya nje?Yaani uhuru ashuke Airport DSM,apokelewe na mkuu wa wilaya kwasababu ni work visit?
 
Kwa taarifa tu: Huu mkutano mkuu wa Benki ya maendeleo ya Afrika unawahusu kina nani hasa kuhudhuria?

The 57th Annual AfDb meetings will bring together Finance and Central Bank Governors of all the 54 Africa Countries to meet in Accra,Ghana from May 23 to 27 May 2022 for their statutory meetings of Governors of the Bank.

Wanaotakiwa kimsingi ni Magavana wa Benki kuu wa mataifa yote ya Afrika. Rais wa Msumbiji yeye pamoja na kuhudhuria mkutano mkuu huo lakini pia alikuwa kwenye state visit nchini Ghana, ndiyo maana Rais wa Ghana alimtuma makamu wake kumwakilisha kwenye mapokezi ya Rais mwenzake!!
Ila Rais kuhudhuria mkutano huo ni sawa akiona anahitaji kujifunza kitu hapo na kupata mawazo mbalimbali!!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…