Missile of the Nation
JF-Expert Member
- May 24, 2018
- 15,101
- 56,054
Taifa zima limekuwa likidhani kuwa suala la katiba mpya ni hisani ya CCM au rais aliyeko madarakani. Hili jambo siyo kweli hata kidogo.
Suala la katiba mpya linaongozwa na Sheria ya mabadiliko ya katiba ya mwaka 2012.
Katika sheria hii, hakuna mahali rais amepewa mamlaka ya kuzuia mchakato wa katiba mpya kusonga mbele, au kujaribu kuufuta kwa namna yoyote ile.
Ukisoma sheria hiyo, imeweka utaratibu maalum wa namna ya kuunda tume ya kukusanya maoni, ikaweka utaratibuwa kuunda bunge la katiba, ikaweka utaratibu wa kutangaza rasimu pendekezwa kwenye gazeti la serikali, na ikaweka utaratibu wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi kuandaa zoezi la kura ya maoni.
Tukumbuke tu kuwa hatua tuliyokuwa tumefikia ni kusubiri Tume ya Taifa ya Uchaguzi iitishe kura ya maoni kuwauliza wananchikama wanaikubali Rasimu Pendekezwa au la.
Rais Magufuli alivunja sheria pale alipozuia mchakato wa katiba mpya kuendelea mbele, hakuwa na mamlaka hayo kisheria. Hatua iliyokuwa inafuata iko mikononi mwa NEC na si Rais.
Sehemu kubwa ambayo sheria ile imempa rais madaraka juu ya hatma ya katiba ni sehemu mbili, ya kwanza ni ile inayompa mamlaka ya kuitisha tena bunge la katiba kuboresha rasimu hiyo hata kama bunge hilo lilishatoa toleo fulani
Sebemu ya pili ni ile inayompa namlaka ya kuchagua siku baada ya Cycle nzima ya mabadiliko ya katiba kuwa imekamilika kuchagua siku ili hiyo katiba mpya ianze kutumika!
Kwa hiyo kama Rais Samia anawaza kupotezea suala la katiba mpya basi ajue tu kuwa anavunja sheria, tena anavunja shetia ya mabadiliko ya katiba, na yeye akumbuke aliapa kulinda sheria.
Kwa hiyo nampa wito Rais Samia, Ama aitishe upya bunge la katiba lipitie ile rasimu yake (ile ya Chenge) liiboreshe, au atimize sheria kwa kuiachia tume ya Taifa ya uchaguzi iitishe kura ya maoni ili sheria ya mabidiliko ya katiba itekelezwe.
Naambatanisha sheria ya mabadiliko ya Katiba