Mnaosema daraja hilo halina impact kicuhumi nina hakika hampafahamu Busisi na huenda hata Mwanza pia hamuifahamu and may be hata Geography pia kwenu ni changamoto; kwangu mimi daraja la Kigamboni ni la starehe Zaidi na kupendezesha mji wa Dar kuliko la Busisi. Iko hivi, ferry ya Busisi kama ilivyo ferry ya Kigamboni ni sehemu inayo unganisha mikoa, sio RAS kama ilivyo Kigamboni, MWanza mjini inatenganisha na ziwa, mikoa inatengwa na ziwa ni Geita, wilaya ya Sengerema, Kigoma, Kagera/Bukoba but again nchi za Rwanda, Burundi, Uganda na hata Congo kwa kupitia Goma, Bukavu; hawa watu kama wanataka kuingia Tanzania kwa kupitia Mwanza ni LAZIMA wapiti kivuko cha BUSISI; umbali huo wa kutoka ng'ambo ya Sengerema to Mwanza mji (Kigongo ferry to Busisi ) ndio hizo 3.12 km, sio sawa na magogoni to Kigamboni ambako sidhani kama zinazidi hata mita 200. Mikoa na nchi nilizozitaja, zinafanya sana biashara na Mwanza kwa saa 24; sometimes watu mnaweza kua mnampinga mhe Magufuli kwa kila kitu but sio kwa daraja, daraja lile litaimaisha uchumi wa Tanzania na nchi jirani. Nani asiyejua kule mwanza watu wanakwenda Uganda kila siku kufata bidhaa? Nani asiyejua kama Uganda, Rwanda, Burundi wankuja kuchukua mizigo mingi ikiwepo chakula Tanzania? Waganda, Rwanda na Burundi hawaendi Dar kufata chakula, wanakwenda MWanza, Kigoma, Geita nk kufata chakula. Tutumie Zaidi busara katika kujenga HOJA kuliko kujazana CHUKI. Elimu, afya nk vyote vina umuhimu but haitakuja kutokea duniani kote kwamba uachane na vitu vinavyo endeleza uchumi uka base kwenye elimu na afya pekee, Maisha mengine pia lazima yaendelee, hao Waganda, Rwanda, Burundi wakija Mwanza wataleta pesa, serikali itapata kodi na hiyo kodi itaendeleza elimu na afya.