Rais Magufuli aagiza magari 130 yaliyotaifishwa yagawanywe kwenye Taasisi za Serikali

Rais Magufuli aagiza magari 130 yaliyotaifishwa yagawanywe kwenye Taasisi za Serikali

RtsHjcq

JF-Expert Member
Joined
Aug 19, 2017
Posts
4,753
Reaction score
5,512
.
 

Attachments

  • Maga.jpg
    Maga.jpg
    37.1 KB · Views: 3
  • Magari.jpg
    Magari.jpg
    29.5 KB · Views: 4
  • Ikulu.jpg
    Ikulu.jpg
    47.6 KB · Views: 3
  • Magali Ikulu.mp4
    10.4 MB
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli leo amekagua magari yaliyotaifishwa baada ya kuhusika katika matukio ya uhujumu uchumi na kisha kuhifadhiwa katika kituo cha mabasi cha zamani Jijini Dodoma.

Idadi ya magari hayo ni 130 yakiwemo makubwa na madogo yalikamatwa katika maeneo mbalimbali hapa nchini, kisha wahusika kufikishwa Mahakamani na Mahakama kutoa uamuzi wa kuyataifa.

Akizungumza baada ya kuyakagua, Rais Magufuli ameipongeza Ofisi ya Mkurugenzi wa Mashtaka (DPP), Jeshi la Polisi na wote waliohusika kuwakamata waliokuwa wanajihusisha na vitendo hivyo (ikiwemo biashara haramu ya meno ya tembo) na ameagiza magari hayo yagawanywe katika taasisi mbalimbali za Serikali ili yatumike kuendesha shughuli za kuwahudumia wananchi na kuzalisha mali.

Mhe. Rais Magufuli pia amewapongeza wananchi waliojitokeza kutoa taarifa zilizosaidia kukamatwa kwa watu waliokuwa wanafanya uhalifu kwa kutumia magari hayo na amewaomba waendelee kutoa ushirikiano kwa vyombo vya dola ili kukomesha vitendo hivyo.


Millardayo.com
 
Hivi Muzungu anaekamataga ndege zetu.
Mbona yupo kimya sana, kunani huko ughaibuni?
Nawaza tu kwa sauti.
 
Wazee wa sheria, VP Rais hajavunja kifungu?
 
Chadema watapinga
Alishawahi kufunga wahujumu UCHUMI Wangapi tangu aingie madarakani? Je sio kweli kwamba wabunge wa CCM Waliopitishwa wote walishindana kwa RUSHWA kwenye mchakato? Huyo anapambana na watu asiowapenda co wahujumu uchumi.
Ile mahakama ya Mafisadi pale UBUNGO ilikufa peeeeee
 
Bado kuna watu walitaka akapange foleni kule kama wagombea wengine huku ana majukumu makubwa kama haya
 
Moja kwa moja kwenye pointi, mzee ameamua magari 130 yaliyokamatwa kutokana na shughuli za uwindaji haramu, uhujumu uchumi pamoja na matukio mbalimbali kupelekwa kwenye idara za serikali yakafanye kazi.

Ndio imeisha hivyo.

 
Back
Top Bottom