Rais Magufuli aagiza vijana 800 wa JKT kuajiriwa

dubu

JF-Expert Member
Joined
Oct 18, 2011
Posts
3,502
Reaction score
3,483
[IMG alt="
Rais wa Tanzania, John Magufuli"]https://www.mwananchi.co.tz/image/v...1466/-/maxw/600/-/t5rk83/-/magu+pic.jpg[/IMG]

Rais wa Tanzania, John Magufuli

Kwa ufupi
Serikali ya Tanzania imetangaza ajira 40,000 kati ya hizo, 800 zitawahusu vijana waliojitolea kwa miaka miwili katika Jeshi la Kujenga Taifa (JKT).

Dodoma. Rais wa Tanzania, John Magufuli ameagiza vijana 800 wenye shahada waliojitolea katika Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) kwa miaka miwili kuajiriwa serikalini kuanzia Februari, 2020.

Akizungumza na waandishi wa habari leo Jumatatu Desemba 23, 2019 jijini Dodoma, Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Menejiment ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Dk Laurean Ndumbaro amesema Rais Magufuli aliagiza vijana hao wenye kiwango cha shahada waajiriwe serikalini kwa kuwa wamejitolea kwa muda mrefu hivyo wamejenga uzalendo.

"Katika kipindi cha 2019/20 Serikali imetangaza nafasi 40,000 na ajira zinaanza Februari, lakini cha msingi tutaanza na hao vijana ambao kwa hesabu ya kawaida hawazidi 800 wenye sifa," amesema Dk Ndumbaro.

Katibu mkuu huyo amewataka vijana hao kuandika barua utumishi wakiambatanisha na nakala za vyeti vya taaluma pamoja na uthibitisho wa wakuu wa kambi zao na wakifanya hivyo, watambue kazi wamepata.

Ameonya watumishi ndani ya Serikali ya Tanzania ambao wanaendelea kuwatetea wenzao ambao walioondolewa kwa kuwa na vyeti feki kwamba Serikali itaanza kuwashughulikiwa.

Chanzo: Mwananchi
 
wanaokwenda kujitolea nafasi inapatikana kwa shida sana...wanaotamani kwenda niwengi lakini wanaopata niwachache....wale wenye connection...nasasa wamepata nafasi za kazi bwerere...kweli Bongo bila connection hutoboi !
 
Nafasi 40,000 wanaanza na vijana 800 wenye shahada,onyo pia latolewa kwa watumishi wanaowatetea waliotumbuliwa.....sawa.
 
Hii ndio faida ya uzalendo..... Naam na ajira zimetangazwa sasa.... Wakuandamana na waandamane..
 
Duuuh hivi namna ya utoaji wa ajira siku hizi siuelewi,...nini kazi ya Psrs maana hii itajenga Mazingira ya upendeleo
 
[IMG alt="
Rais wa Tanzania, John Magufuli"]https://www.mwananchi.co.tz/image/v...1466/-/maxw/600/-/t5rk83/-/magu+pic.jpg[/IMG]

Rais wa Tanzania, John Magufuli

Kwa ufupi
Serikali ya Tanzania imetangaza ajira 40,000 kati ya hizo, 800 zitawahusu vijana waliojitolea kwa miaka miwili katika Jeshi la Kujenga Taifa (JKT).

Dodoma. Rais wa Tanzania, John Magufuli ameagiza vijana 800 wenye shahada waliojitolea katika Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) kwa miaka miwili kuajiriwa serikalini kuanzia Februari, 2020.

Akizungumza na waandishi wa habari leo Jumatatu Desemba 23, 2019 jijini Dodoma, Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Menejiment ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Dk Laurean Ndumbaro amesema Rais Magufuli aliagiza vijana hao wenye kiwango cha shahada waajiriwe serikalini kwa kuwa wamejitolea kwa muda mrefu hivyo wamejenga uzalendo.

"Katika kipindi cha 2019/20 Serikali imetangaza nafasi 40,000 na ajira zinaanza Februari, lakini cha msingi tutaanza na hao vijana ambao kwa hesabu ya kawaida hawazidi 800 wenye sifa," amesema Dk Ndumbaro.

Katibu mkuu huyo amewataka vijana hao kuandika barua utumishi wakiambatanisha na nakala za vyeti vya taaluma pamoja na uthibitisho wa wakuu wa kambi zao na wakifanya hivyo, watambue kazi wamepata.

Ameonya watumishi ndani ya Serikali ya Tanzania ambao wanaendelea kuwatetea wenzao ambao walioondolewa kwa kuwa na vyeti feki kwamba Serikali itaanza kuwashughulikiwa.

Chanzo: Mwananchi
Aisee kujitolea kumbe ni kipimo cha uzalendo?

Kwa nini usifikirie ni kukosa mbadala kwa hiyo wanaona bora wawepo huko watalala na kula kwa uhakika.

Miongozo ya namna tunafikia maamuzi inabidi itazamwe.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Sisi ambao hatutaki kazi za taasisi za kiraia tufanyaje!

5/5
 
Ngoja nimpigie mjamaa mmoja anipe ukweli katika hili. Maana huu mwaka wa 3 na bachelor yake yuko JAKATA
 
Back
Top Bottom