Rais Magufuli aamrisha wananchi kwenda kujisaidia nyumbani kwa mkurugenzi na DC Kibiti

Rais Magufuli aamrisha wananchi kwenda kujisaidia nyumbani kwa mkurugenzi na DC Kibiti

Mbona kama maamuzi ya hasira sana?Mara gari ya DED igeuzwe ambulance,huku tena watu wakajisaidie kwa DC, aisee
Halafu hapo wateule waache kwenda kutafuta uhuru wao kupitia nafasi za ubunge?

Yote tisa, alipokuwa Kilwa akaelezwa changamoto ya stendi akasema tatizo wamechagua mbunge wa upinzani ila hapo Kibiti hakuna vyoo tatizo limekuwa Dc na DED, Meko kwa double standards hajambo.
 
Halafu hapo wateule waache kwenda kutafuta uhuru wao kupitia nafasi za ubunge?

Yote tisa, alipokuwa Kilwa akaelezwa changamoto ya stendi akasema tatizo wamechagua mbunge wa upinzani ila hapo Kibiti hakuna vyoo tatizo limekuwa Dc na DED, Meko kwa double standards hajambo.
Kuna shida kwakweli
 
Safi sana Mh Raisi,

Hivi ndivyo inavyotakiwa.

Unajenga soko, una toza ushuru na kukusanya kodi kwa wafanya biashara alafu huduma muhimu kama choo eti hakuna!

DED yupo, DC yupo na mbunge yupo

This is rubbish
 
Nafikiri kipindi hiki kuna shida kwa local governments kujiendesha, ni kama zimenyanga'anywa mamlaka yake. Makusanyo mengi ya halmashauri kwa sasa yatakuwa yanakwenda hazina, hivyo hata ukihitaji kutumia pesa lazima uombe kutoka huko serikali kuu jambo ambalo linazifanya halmashauri kushindwa kutekeleza mipango yake kwa uhuru kama ilivyokuwa huko nyuma.
 
Dawa wananchi wachague wabunge wengi wa upinzani ili serikali yoyote itakayoingia madarakani baada ya uchaguzi wa Oktoba 2020 iweze kubanwa na iwajibike kuwatumikia wananchi walipa kodi.
Hapa tunazungumzia watumishi wa serikali wanaoteuliwa wapo wasiokidhi viwango wanahitaji in service training.
 



Rais Magufuli leo akiwa njiani kutoka msibani, amesimama mara kadhaa kuwasalimu wananchi na kuwasikiliza. Ameshangazwa na watu walio chini yake kushindwa kujenga choo cha soko ilihali mapato ya halmashauri yao ni zaidi ya bilioni 1.8

Rais Magufuli ametoa agizo la choo husika kukamilika ndani ya siku saba la sivyo mkurugenzi aandike barua ya kuacha kazi. Pia ameagiza siku saba wakati choo kinajengwa wananchi waende kujisaidia nyumbani kwa DC pamoja na mkurugenzi ambae nyumba yake iko mtaa wa pili kutoka soko lilipo kwani nchi haiwezi kukosa choo wakati wanakusanya bilioni 1.8.

Amesema yuko 'very serious' na suala hilo hivyo mwananchi akibanwa afungunguliwe. Amewaamirisha wawatayarishie maji ya kutosha lakini kama wana akili watajenga usiku na mchana.

Rais Magufuli amesema haiwezekani wakusanye bilioni moja kutoka kwa wananchi alafu washindwe kuwajengea choo hivyo amewataka wafanyibiashara sokoni hapo kutolipa ushuru sokoni hapo kuanzia leo mpaka siku kitapojengwa choo.


Fair enough!
 
Huyu mtu nahisi kuna muda dishi huwa linacheza. Hivi kikawaida tu kwa mtu Mwenye akili nani anaweza tamka hadharani au hata kufikiria kumpelekea mama yake mzazi mwanaume??
Hayuko sawa kichwani alafu kapanic sn hasa baada ya Lissu kulakiwa na maelfu ya watz lkn zaidi hotuba ya Kikwete imemshusha sn sn.........
 
Back
Top Bottom