Hah Hah siasa haihitaji hasira, ndiyo tatizo la kukosa mfumo kila kitu wateuliwa kama ma-RC, DC, DED hawajiamini kutoa maamuzi wanasubiri Mh. Rais atatue. Hili pia lipo ktk mhimili wa Bunge ambapo wabunge wa CCM wanashindwa kuiwajibisha serikali wanawaachia mawaziri watoe maswali na majibu kwa niaba ya wabunge wa CCM.
Uchaguzi wa Oktoba 28 , 2020 wagombea wa CCM watakuwa wapweke hakuna wa kuwabeba kutoka mhimili wa serikali kuu (dola) wala spika kuwalinda dhidi ya maamuzi magumu ya wananchi kuchagua wabunge kutoka upinzani wenye uwezo wa kusema kwa niaba ya wananchi na kuibana serikali ili iweze kuamka toka usingizini ipate kuwajibika.