Rais Magufuli aamuru Kikokotoo kilichokuwa kinatumiwa awali kiendelee hadi 2023 (kulingana na mfuko husika)

Nadhani mmesikia na kuona wenyewe kutoka Ikulu. Wale wambeya mpasuke sasa.
 

UPDATE: VIKOKOTOO VYA ZAMANI KWA MIFUKO YOTE KUENDELEA KUTUMIKA KWA KIPINDI CHA MPITO HADI 2023
 
Huyu jamaa ni muhini sana. Alichowafanyia wafanyakazi ni kma machinga. Yan katuma wakuu wa mikoa awafukoze, wapigwe na wabomolewe mabanda yao, alafu baada ya wiki akaibuka kuwatetea.

Leo wafanyakaz wamekuwa affected psychologicaly. Ndyo anakuja kujisemesha. Siku zote alkuwa wapi?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Naona magu anajisafisha anaelekea kuwa win wastaafu uchaguzi ujao ni habari njema kwakweli kuwarejeshea wastaafu kikokotoo cha zaman 50% maana watu walikua wanakufa na pressure
 
Hahahaah na wengine wamekufa kwa mishtuko....!!!
 


1.Jenga tatizo
2.Wacha walumbane wee
3.Then waite wote ikulu
4.Weka kamera kubwa sana
5.Toa uamuzi ambao ndio sahihi tangu mwanzo
6.Then beba sifa na utakatifu wote kwa kutatua tatizo ulilolijenga wewe mwenyewe.

Aisee jiwe ni wa kuhurumia kabisa!
 
Kikokotoo kimerudishwa kama kilivyokuwa zamani

Sent using Jamii Forums mobile app

Kumbuka Wafanyakazi wengi Serikalini ni Walimu na hao hao Walimu ndiyo Waratibu Wakuu wa Uchaguzi kwa miaka mingi nchini na ndiyo Watu ambao wapo karibu sana na Jamii Kubwa ya Kitanzania hivyo ukiwagusa au kuwaudhi kuna hatari kubwa ama mwaka 2020 au 2025 wakakuangusha vibaya sana Wewe au na Chama chako hivyo njia pekee ya Kujikosha Kwao ni Kuwafurahisha katika hili lakini pia hapo hapo Sifa aipate Mtu fulani kwamba anawajali Wafanyakazi na Watumishi wa Umma hasa kuelekea mwakani 2019 ambako kuna Chaguzi kabla ya ule wa 2020. Wenye akili na maono waliposikia tu kuwa leo kuna Kikao / Mkutano huo walijua kuwa una Agenda Kuu mbili 1. Kujikosha na 2. Kuwahadaa Wafanyakazi baada ya Kuiona hatari iliyokuwa inakuja hasa kwa upande wa Serikalini. Naomba niishie hapa tafadhali.
 
Naombeni Mods msiunganishe huu uzi, usimame kama ulivyo.
Nyie Wabunge wa Upinzani Mungu atawabariki sana,mlipiga kelele sana juu ya Ukatili na Mateso ya Kikotoo Kipya cha 25%,mlipiga kelele, wabunge wenzenu wa CCM walikuwa kimya, na wengine walienda mbele kumpongeza Raisi kwa Kikotoo kipya na kuwaita wale wote waliokuwa against the new 25% scheme kuwa ni maadui wa Taifa.
Juzi tu Mh John Mnyika katika uwekaji wa jiwe la Msingi ujenzi wa Barabara Mpya uliofunguliwa na Rais Magufuli Mnyika alizungumzia kuhusu adha ya 25% wanayopata wastaafu.
Leo Raisi amepiga mule mule walipokuwa wanapiga wapinzani, ni aibu kubwa sana kwa wale wote waliokuwa wana support that new Scheme kwa Kigezo cha Kumuunga Mkono Raisi.
Raisi amewaumbua.
Mungu wabariki wana Wabunge wa Upinzani.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…