Rais Magufuli aamuru Kikokotoo kilichokuwa kinatumiwa awali kiendelee hadi 2023 (kulingana na mfuko husika)

Rais Magufuli aamuru Kikokotoo kilichokuwa kinatumiwa awali kiendelee hadi 2023 (kulingana na mfuko husika)

Nadhani mmesikia na kuona wenyewe kutoka Ikulu. Wale wambeya mpasuke sasa.
 
INAKUJIA HIVI PUNDE. RAIS WA WANANCHI NA MASKINI WA TANZANIA, DR JIOHN POMBE MAGUFULI KUKUTANA NA VIONGOZI WA VYAMA VYA WAFANYAKAZI PAMOJA NA MIFUKO YA HIFADHI YA JAMII KUZUNGUMZIA NA KUTATUA TATIZO LA KIKOKOTOO CHA MAFAO YA KUSTAAFU AMBACHO KIMELETA GUMZO KUBWA KATIKA SIKU ZA HIVI KARIBUNI HAPA NCHINI.

RAIS MAGUFULI AMBAYE NI RAIS MSIKIVU NA MCHUKUA HATUA NA MTEKELEZAJI WA KILE ANACHOKISEMA ATATOA KAULI KUHUSU KADHIA HII KUBWA KWA WAFANYAKAZI. STAY TURNED KUPATA HABARI MUBASHARA KUPITIA UZI HUU.

UPDATES.
katibu mkuu wa TUCTA YAHAYA MSIGWA, TALGWU WAPO WAKIONGOZWA NA KM WAO EKINGO YUPO MKUNDA, WAPO TUIKO WAKIONGZWA NA PAUL SENGEZE, RAU WANAONGOZWA NA KM WAO, CHAMA CHA WAFANYAKAZI WA MADINI, CHAMA CHA RELI CHINI YA YUSUFU MANDAO, CHAMA CHA WAMILIKI WA MITANDAO YA SIMU, CHAMA CHA TAASISI ZA VYUO VIKUU, VIONGOIZ WA MIFUKO YA HIFADHI YA JAMII CHINI YA ADAMU MAYINGU NA ADAM MSANGI

RAIS NDIO ANAONGOZA MJADALA HUU NA MJADALA UMEANZA. RAIS ANASEMA TUZUNGUMZE, NA HAYA MASUALA LAZIMA YAFIKIE MWISHO, NTAWASIKILIZA NA NITATOA JIBU LEO.

TUANZE KWA KUWASIKILIZA VIONGOZI WA WAFANYAKAZI, SEMENI MTAKA TUENDEJE.

UPDATES...
MWENYEKITI WA TAASISI ZA VYUO VIKUU ANAANZA KUTOA HOJA. ANASEMA MJADALA HUU UMEKUWA MKUBWA SANA BAADA YA MIFUKO YA HIFADHI YA JAMII KUUNGANISHWA NA KIKOKOTOO KUWA KIKUBWA. WAFANYAKAZI WALIOKUWA WANASTAAFU WAKAANZA KUPOKEA MAFAO KIDOGO NA HIVYO KUONEKANA WAFANYAKAZI
WANAPUNJWA. KATIKA MAZINGIRA HAYA MTOAJI ANASEMA TUKITOA ZOTE MFUKO UTAKUFA, SASA SISI TUNAHOJI, MBONA ZAMANI TULIKUWA TUNALIPWA??? MH RAIS NAOMBA IUNDWE KAMATI IKASIKILIZE PANDE ZOTE IJE NA MAJIBU YA KISAYANSI NA KITAALAM KULIKO UPANDE MMOJA KUAMUA.

UPDATES...
MZUNGUMZAJI WA PILI
ANASEMA HILI SUALA LA KIKOKOTOO HALIFAHAMIKI KWA WENGI, SISI VIONGOZI TULISIKILIZWA NA SHERIA IMEANGALIWA VIZURI. SHERIA ZOTE ZINA KANUNI. SISI TUMESHINDWANA NA SERIKALI KWENYE KIKOKOTOO. UMRI WA KUISHI, KUTOKA 15.5, MSHAHARA WA MWISHO PIA IMEBADILIKA NA HIVYO SASA INACHUKULIWA ASILIMIA 15 AMBAYO INAPUNGUZA KIWANGO ANACHOCHUKUA MFANYAKAZI BAADA YA KUSTAAFU. WAPO WALIOZIMIA, WAPO WALIOCHANGANYIKIWA, WAPO WALIOKATA TAMAA KABISA....WAZIRI ALITOA AGIZO SHERIA IFUATWE NA BADAE TUKAPIGA KURA. TULIKATA RUFAA KABLA WAZIRI HAJASAINI ILE SHERIA NA LEO TUNASHUKURU UNATUSIKILIZA KILIO CHETU HAPA MH RAIS.
OMBI....TUNAOMBA TURUDI TENA MEZANI MH RAIS

UPDATE: VIKOKOTOO VYA ZAMANI KWA MIFUKO YOTE KUENDELEA KUTUMIKA KWA KIPINDI CHA MPITO HADI 2023
 
Loh
IMG_20181228_114326.jpeg


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Huyu jamaa ni muhini sana. Alichowafanyia wafanyakazi ni kma machinga. Yan katuma wakuu wa mikoa awafukoze, wapigwe na wabomolewe mabanda yao, alafu baada ya wiki akaibuka kuwatetea.

Leo wafanyakaz wamekuwa affected psychologicaly. Ndyo anakuja kujisemesha. Siku zote alkuwa wapi?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Naona magu anajisafisha anaelekea kuwa win wastaafu uchaguzi ujao ni habari njema kwakweli kuwarejeshea wastaafu kikokotoo cha zaman 50% maana watu walikua wanakufa na pressure
 
Huyu jamaa ni muhini sana. Alichowafanyia wafanyakazi ni kma machinga. Yan katuma wakuu wa mikoa awafukoze, wapigwe na wabomolewe mabanda yao, alafu baada ya wiki akaibuka kuwatetea.

Leo wafanyakaz wamekuwa affected psychologicaly. Ndyo anakuja kujisemesha. Siku zote alkuwa wapi?

Sent using Jamii Forums mobile app
Hahahaah na wengine wamekufa kwa mishtuko....!!!
 
Screenshot 2018-12-28 11.40.31.png


1.Jenga tatizo
2.Wacha walumbane wee
3.Then waite wote ikulu
4.Weka kamera kubwa sana
5.Toa uamuzi ambao ndio sahihi tangu mwanzo
6.Then beba sifa na utakatifu wote kwa kutatua tatizo ulilolijenga wewe mwenyewe.

Aisee jiwe ni wa kuhurumia kabisa!
 
Kikokotoo kimerudishwa kama kilivyokuwa zamani

Sent using Jamii Forums mobile app

Kumbuka Wafanyakazi wengi Serikalini ni Walimu na hao hao Walimu ndiyo Waratibu Wakuu wa Uchaguzi kwa miaka mingi nchini na ndiyo Watu ambao wapo karibu sana na Jamii Kubwa ya Kitanzania hivyo ukiwagusa au kuwaudhi kuna hatari kubwa ama mwaka 2020 au 2025 wakakuangusha vibaya sana Wewe au na Chama chako hivyo njia pekee ya Kujikosha Kwao ni Kuwafurahisha katika hili lakini pia hapo hapo Sifa aipate Mtu fulani kwamba anawajali Wafanyakazi na Watumishi wa Umma hasa kuelekea mwakani 2019 ambako kuna Chaguzi kabla ya ule wa 2020. Wenye akili na maono waliposikia tu kuwa leo kuna Kikao / Mkutano huo walijua kuwa una Agenda Kuu mbili 1. Kujikosha na 2. Kuwahadaa Wafanyakazi baada ya Kuiona hatari iliyokuwa inakuja hasa kwa upande wa Serikalini. Naomba niishie hapa tafadhali.
 
Naombeni Mods msiunganishe huu uzi, usimame kama ulivyo.
Nyie Wabunge wa Upinzani Mungu atawabariki sana,mlipiga kelele sana juu ya Ukatili na Mateso ya Kikotoo Kipya cha 25%,mlipiga kelele, wabunge wenzenu wa CCM walikuwa kimya, na wengine walienda mbele kumpongeza Raisi kwa Kikotoo kipya na kuwaita wale wote waliokuwa against the new 25% scheme kuwa ni maadui wa Taifa.
Juzi tu Mh John Mnyika katika uwekaji wa jiwe la Msingi ujenzi wa Barabara Mpya uliofunguliwa na Rais Magufuli Mnyika alizungumzia kuhusu adha ya 25% wanayopata wastaafu.
Leo Raisi amepiga mule mule walipokuwa wanapiga wapinzani, ni aibu kubwa sana kwa wale wote waliokuwa wana support that new Scheme kwa Kigezo cha Kumuunga Mkono Raisi.
Raisi amewaumbua.
Mungu wabariki wana Wabunge wa Upinzani.
 
Back
Top Bottom