Rais Magufuli aamuru Kikokotoo kilichokuwa kinatumiwa awali kiendelee hadi 2023 (kulingana na mfuko husika)

Nilijua hili lingetokea tu mwisho wa siku.Maana hata mahakama ingewapatia haki walalamikaji.Ama kweli fumbo mfumbie mjinga......😀😀😀
 
Hongera sana rais wetu kwa kusimama upande wa watumishi ambao wengi wao walikuwa wameanza kupoteza matumaini.Tunaomba pia ulishughulikie suala la nyongeza ya mishahara.Maneno yako yalidhihirisha nia njema uliyo nayo kwa Tanzania na watu wake wote.Viva JPJM.

Kupinga kila kitu na kusifia kila kitu ni upungufu wa fikra pevu.

Be blessed abundantly my president.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Tundu lisu endelea kukazia kwenye kugombea urais 2020 mpaka wafanyakazi waongezwe mshahara
 
Very easy to fool Tanzanians

Huu ni muswaada uliotokea Baraza la Mawaziri ambalo yeye ni mwenyekiti.

Unapataje sifa kwa kufuta muswaada wako ulioshindikana kwa wananchi?
 
Mtaje tu huyo waziri kivuli. Tuwape moyo wenzetu hawa wanaotutetea. Wakifanya vema, tuwape credits zao. Hiyo itatupa haki ya kuwananga pale wanapoboronga au kushindwa kutimiza wajibu wao.

Hata Mh Mnyika pia anastahili pongezi maana naye hakusita kuchagiza kuhusu kikokotoo pale alipopata dk 5 za "kusalimia" (sote tunajua alivyonangwa baada ya hapo!)

Halafu kuna watu wanatamani "upinzani" ufe!!!
 
unajisahaulisha kuwa wapinzani ndio waliopiga kelele hadi huyo kichaa wenu akaamua kuwasaliti wasaidizi wake. Unadhani mswada hadi unaenda bungeni na kupitishwa na wabunge wa chama chake yeye alikuwa hajui
Hizo kelele za wapinzani ni zipi?
 
Uzuri ni kwamba Rais Magufuli ni msikivu!
 
Reactions: SMU
Kwanza namshukuru Mwenyezi Mungu kwa kumjalia mtumishi wake Na Rais wetu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania karama ya neno la hekima na maarifa iliomwongoza leo kufanya maamuzi makubwa na yenye maslahi kwa watumishi wa umma na sekta binafsi na taifa kwa ujumla. Hii ni zawadi tosha ya mwaka mpya. Najua wako watakaobeza uamuzi huu lakini watakaofanya hivyo watakuwa wamesongwa na inda na taadi na hivyo wapuuzwe.
Mhe. Rais nakupongeza sana kwa usikivu wako. Wengine wataimba kuwa hoja iliibuliwa na Waziri kivuli. Tunasema huu ndio ushaihidi kuwa Rais wetu husikiliza watu wote na akiona hoja mantiki hufanyia kazi na kutolea uamuzi. Hii pia inadhihirisha kuwa nchi yetu ina uhuru wa mawazo. Hongera sana Mhe. Rais kwani wewe umemaliza sehemu inayokuhusu kama mamlaka ya nchi.
Wito wangu kwa Waziri mwenye dhamana ya sekta ya hifadhi ya jamii Ni kuwa chukua hatua ya kurasimisha maelekezo ya Rais ili watendaji wasitumie mwanya kuwa sheria imeelekeza hivi na hivyo kuendelea kuwamiza wastaafu kama ilivyotokea sekta ya fedha ambapo Rais alielekeza tozo stahiki kwa nyumba lakini Wizara na TRA wakaendelea kuwabamiza wenye nyumba kwa madai kuwa wanatekeleza sheria. Tunaendelea kujenga na imani na Mhe. Rais na tunakushukuru kwa maamuzi yako.

Mhe. Rais nakutakia kheri ya mwaka mpya 2019.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…