Rais Magufuli aamuru Kikokotoo kilichokuwa kinatumiwa awali kiendelee hadi 2023 (kulingana na mfuko husika)

Mama mzazi ni Msukuma? According to list ya watani wako upande wa mama.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hapa ndipo unagundua Admin na members wake kuna upande hawana nati zilizotimilifu vichwan mwao
Admin yy kaamua kujisafisha baada ya kugundua urafik na watumishi(ata jeshi limpalo kiburi) unazid kupungua kwa speed ya mwanga maana sheria n msumeno
Sasa yale mabwana yaliyoupitisha kwa mbwembwe na vifijo utadhan ni king Columbus kagundua bara jipya cjui yana hali gan maana admin kayachomesha mahind kwa tochi
Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nani angeenda mahakamani,kuwa na shukrani mkuu,mh, rais akiamua ameamua.kuwa na shukrani aisee!!

Sent using Jamii Forums mobile app
Mkuu Mimi ningekuwa nastaafu ningeenda kwani mkataba niliousaini na serikali sio huo wa 25%.Hivi niwe na shukrani kwa jasho na haki yangu?Umesikia kuwa pension ni hisani au?Acha basi uoga usiofaa mkuu.Kwenye haki ukweli husimama daima.Aluta continua!
 
CCM Ni slow learners siku zote.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
kasema after 2023 hata wakikubaliana 70% hana tatizo hahah yaan jamaa huyu bana
Huyu bwana mkubwa anajua kucheza na akili za watu sana, baada ya kupima upepo kwenye 25% na kutopata uungwaji mkono akaja kama mkombozi wa watumishi kwa kuondoa hizo 25%. Kinachofuata hapo ni kuongeza mishahara kwenye Mei mosi ya 2019 ili kujihakikishia kura kwenye chaguzi za serikali za mitaa 2019 na uchaguzi mkuu wa 2020. The guy is so predictable in every mark of his steps.
 
Rais J.P.M mtu wa watu. Wafanyakazi Mna kila sababu ya Kuendelea Kumuombea.Live long Mr President.Tanzania Tulikuwa tunahitaji Kiongozi wa nchi wa namna hii.Kiongozi/Rais wa wanyonge.Hakika tumepata Baba.
 
Hongera sana Rais J.P. Magufuli kwa uamuzi wa kuwajali na kuwatetea wafanyakazi, hakika wewe ni Rais wa watanzania wote. Asiyekubali hilo anywe dawa ya usingizi alale . Live long mr President tunakuhitaji sana watanzania.
 
Mbona zipo baadhi ya sekta binafsi zina mishahara mikubwa zaidi ya iyo ya serikali
ni kweli lakini nyingi ni vurugu tu ndugu yangu binafsi nimefanya kampuni moja zaidi ya miaka 10 lakini nilichopata hakilingani na kazi ya miaka 3 wengi wanaumia kwa kweli labda uwe NGO
 
wadau mfano umefanya kazi kwa miaka 10,na ukaachishwa kazi ukiwa na umri wa miaka 40,je kwa mujibu wa hotuba ya rais ya jana,naweza pewa hela yangu yote niliyochangia nssf?kama zamani?
 
wadau mfano umefanya kazi kwa miaka 10,na ukaachishwa kazi ukiwa na umri wa miaka 40,je kwa mujibu wa hotuba ya rais ya jana,naweza pewa hela yangu yote niliyochangia nssf?kama zamani?
Amesema mambo yarudi kama zamani hadi 2023. Ametolea mfano kadhia ya watu wanaofanya kazi za mikataba ya muda mfupi kama miaka 3 hakuna sababu ya kusubiria chao mpaka sijui afikishe miaka 60, wapewe chao wakafie mbele. So fao la kujitoa limerudi.
 
Amesema mambo yarudi kama zamani hadi 2023. Ametolea mfano kadhia ya watu wanaofanya kazi za mikataba ya muda mfupi kama miaka 3 hakuna sababu ya kusubiria chao mpaka sijui afikishe miaka 60, wapewe chao wakafie mbele. So fao la kujitoa limerudi.
asnte mdau,tusubiri wengine
 
Hapana, kilichofutwa ni kanuni ya kikokotoo kipya cha 25% na siyo sheria mpya (iliyofuta fao la kujitoa).

Sent using Jamii Forums mobile app
Watanzania mbona mnakuwa wagumu sana kuelewa? Au hukumsikiliza rais bali umesimuliwa? Kuna vitu vingine sio lazima aviseme kwa kuvirudiarudia. Swala la ajira za muda mfupi kaliongelea tena kwa kutoa na mifano kabisa ya mikataba ya muda mfupi. Sasa sijui mpaka atamke kabisa "fao la kujitoa limerudi" ndio uelewe? Achilia mbali mifano aliyoitoa kuhusu ajira za muda mfupi amesema mambo yarudi kama zamani mpaka 2023. Aisee watanzania bhana!
 
nikopeeni nauli niende arusha nikadai pesa zangu nssf, npo moro wajameni. Ole waniambie utumbo wao mle ndani nitawaua kabisa
 
Duuuu sio poa kujumuisha.kwan ww mrundi
Sent using Jamii Forums mobile app
 
Duuuu sio poa kujumuisha.kwan ww mrundi

Sent using Jamii Forums mobile app
Samahani mkuu. Acha na mimi niji-include, "sisi watanzania ni wagumu sana kuelewa". Rais kaongea tena kwa kutolea mfano "kwenye hizi miradi ya serikali ambayo mkandarasi anajenga kwa muda wa miezi 36, unamwambia mtu asubirie mafao yake mpaka afikishe miaka 60, si umpe hela yake akafie mbele, akifikisha miaka 60 hata mkandarasi mwenyewe anakuwa kesha ondoka, hata nyinyi mifuko ya kijamii hata hamumkumbuki huyu mfanyakazi" mwisho wa kunukuu. Sasa mtu anakuja kusema fao la kujitoa hajaliongelea, aisee! Kweli sisi watanzania ni wagumu wa kuelewa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…