Rais Magufuli aamuru Kikokotoo kilichokuwa kinatumiwa awali kiendelee hadi 2023 (kulingana na mfuko husika)

Rais Magufuli aamuru Kikokotoo kilichokuwa kinatumiwa awali kiendelee hadi 2023 (kulingana na mfuko husika)

Halafu kila Siku huwa unajinasibu kuwa ni Mtani wangu je unatoka Kabila gani Mkuu?

Watani zangu wakubwa upande wa Baba GENTAMYCINE ni:

1. Wahaya ( Kagera )
2. Wanyiramba na Wanyaturu ( Singida )
3. Waha ( Kigoma )
4. Warangi ( Kondoa Dodoma )
5. Wakara ( Ukerewe Mwanza )

Watani zangi wakubwa upande wa Mama GENTAMYCINE ni:

1. Wangoni ( Ruvuma )
2. Waluguru na Wapogoro ( Morogoro )
3. Wandengereko ( Rufiji Pwani )
4. Wazaramo ( Dar es Salaam )
5. Wakwere ( Pwani )

Nasubiri jibu langu hapo tafadhali ili nianze Kukujua mapema na niwe na Kibali Maalum cha kuwa nakupiga Madongo hapa 24/7.
Mama mzazi ni Msukuma? According to list ya watani wako upande wa mama.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hapa ndipo unagundua Admin na members wake kuna upande hawana nati zilizotimilifu vichwan mwao
Admin yy kaamua kujisafisha baada ya kugundua urafik na watumishi(ata jeshi limpalo kiburi) unazid kupungua kwa speed ya mwanga maana sheria n msumeno
Sasa yale mabwana yaliyoupitisha kwa mbwembwe na vifijo utadhan ni king Columbus kagundua bara jipya cjui yana hali gan maana admin kayachomesha mahind kwa tochi
Nahisi Makao Makuu hasa Kitengo cha Propaganda leo kimetoa AMRI kuwa Wanachama wote waje JamiiForums kuanzisha tu Mada mbalimbali za Kusifu kama siyo Kupongeza na kwakweli leo naziona nyingi sana. Kumbe huwa mpo? Natumai leo ile Bajeti ya Watu wa Propaganda itakuwa imetumika na inatumika vizuri sana na siyo Siri mnajitahidi kwani kila baada ya dakika 15 tu naona ID mpya inaanzisha Mada ya Kupongeza kama zingine ila kinachofanyika ni kwamba kila anayeanzisha anakuja na Topiki yake.

Safi sana!

Nawasilisha.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nani angeenda mahakamani,kuwa na shukrani mkuu,mh, rais akiamua ameamua.kuwa na shukrani aisee!!

Sent using Jamii Forums mobile app
Mkuu Mimi ningekuwa nastaafu ningeenda kwani mkataba niliousaini na serikali sio huo wa 25%.Hivi niwe na shukrani kwa jasho na haki yangu?Umesikia kuwa pension ni hisani au?Acha basi uoga usiofaa mkuu.Kwenye haki ukweli husimama daima.Aluta continua!
 
Hongera Esther Bulaya, hongereni Wapinzani, hongereni Wote mliotetea na kusimama na Wafanyakazi muda Wote. CCM Ni slow learners siku zote. Sheria hiyo imetungwa na serikali JIWE akiwa anafahamu na kutoa maelekezo. Sheria hiyo ilipitishwa kwa wingi wa Kura na Wabunge wa CCM licha ya kupingwa na Wapinzani. CCM msijifanye mnawajali Wanyonge, nyie Ni Kupe na Chawa mnaowamaliza Wanyonge katika Taifa hili. Leo hii JIWE anajadili Nini asichokijua? Au kwakuwa Watanzania wengi wapo gizani basi Ni mwendo wa kutengeneza Tatizo na kulitatua baadae?

Wito kwa Wapinzani! Huu ndio mwaka Mzuri wa kupaza sauti zaidi, ATAFANYA hata Kama Hapendi ili tu, Uchaguzi wa Serikali za mitaa na Uchaguzi Mkuu ujao apate kura. Pazeni sauti kwa Maslahi ya Wanyonge wa nchi hii, sauti hii itasikilizwa Sana hii miaka miwili!

Sent using Jamii Forums mobile app
CCM Ni slow learners siku zote.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
kasema after 2023 hata wakikubaliana 70% hana tatizo hahah yaan jamaa huyu bana
Huyu bwana mkubwa anajua kucheza na akili za watu sana, baada ya kupima upepo kwenye 25% na kutopata uungwaji mkono akaja kama mkombozi wa watumishi kwa kuondoa hizo 25%. Kinachofuata hapo ni kuongeza mishahara kwenye Mei mosi ya 2019 ili kujihakikishia kura kwenye chaguzi za serikali za mitaa 2019 na uchaguzi mkuu wa 2020. The guy is so predictable in every mark of his steps.
 
UPDATES:



Viongozi wa Vyama vya wafanyakazi wametoa historia ya walikotoka hadi walikofika. Aidha, wamedokeza kuwa wapo waliozimia kwenye ofisi za Mifuko ya Hifadhi ya Jamii.

Rais Magufuli anawasikiliza na anataka kila mtu aongee na kutoa dukuduku ili aweze kuongea.

Viongozi wa vyama vya wafanyakazi (upande wa walimu) wanadai kikokotoo kimekuwa ni suala kubwa na Rais Magufuli kama mwalimu anatambua changamoto za walimu. Wanamwomba Rais aliangalie suala la kikokotoo kwa jinsi atakavyoweza kwakuwa wanajua anaweza na kwa wanavyomsaidia Mungu atamsaidia alitatue hili.

TUGHE: Tunakupongeza Mhe. Rais, lakini tunapenda ufahamu kuwa wastaafu wengi hawakuwa wameandaliwa na mabadiliko haya yametokea ghafla na kusababisha negative impact. Morali ya kazi imeshuka!

Waziri Mhagama
Hoja na kuunganisha mifuko ilikuwa ni hoja ya wafanyakazi.

Hapa tunazungumza tu kikokotoo, ili tupate kikokotoo lazima turudi kwenye contribution rate, tukitaka tuendelee na kikokotoo cha 50% contribution itabidi itoke kwenye 20% hadi 25%.

TUCTA: Tunafahamu kwa moyo wako na unavyowasaida wanyonge. Tunaamini utasaidia kutatua

Mwanzo Wastaafu walikuwa wanapata 50% kwa mkupuo na 50% kidogo kidogo kila mwaka

Tulipendekeza mkupuo uwe 40% na si 25%


CHAMA CHA WALIMU: Suala la kikokotoo ni shida, hakuna asiyejua shida za waalimu. Uzuri ni kwamba hata wewe Rais ni Mwalimu

Kwasasa hata mishahara ya mwisho wa mwezi haitoshi. Kwa namna unavyofanya mambo makubwa najua hata hili unaliweza


TUGHE: Wastaafu wengi hatukuwaandaa kisaikolojia. Mabadiliko haya ya kikokotoo cha mafao yametokea kwa ghafla sana.

Wafanyakazi wa umma waliowengi wanalalamika nakuomba mheshimiwa Rais uongee chochote ili Wafanyakazi warudi kwenye morali ya kazi

TUICO: Watu wa sekta binafsi kima chao cha chini ni 100,000. Ili kwenda vizuri kamati itakayoundwa ikachunguze hii mishahara

Pia kuna fao la kupoteza ajira hawalipwi na makampuni mengi yanaondoka bila ya kuwalipa


WAFANYAKAZI WA RELI: Tumepitia misukosuko sana ikiwemo mishahara kuwa kidogo na ulipwaji wake ni wa kusuasua sana

Tulitegemea mafao ya kustaafu yatusaidie kujenga nyumba ili hata tukifa tufe vizuri.

Ile 50% ya awali kama haiwezekani basi tunakubali iwe 40%


TAMICO: Kwenye suala la kikokotoo kuna shida hasa kwenye fao la kujitoa ambalo mbadala wake ni fao la kukosa ajira

Sekta binafsi tunapata shida kwasababu kazi zetu si za muendelezo. Tunaomba iwepo tofauti kwa watu wa sekta ya migodi na ujenzi kwenye fao la kukosa ajira


SERIKALI ZA MITAA: Tunapenda mifuko iwe imara lakini kwa mishahara yetu hii midogo kwa kweli inaumiza

Rais kelele ni nyingi sana, na kwa kikokotoo hiki mfanyakazi akistaafu atashindwa hata kujenga


CHAMA CHA WAAJIRI: Sheria hii ya mifuko ya jamii, ililenga kuiweka mifuko hii kuwa katika hali ya usawa

Baada ya mifuko kuunganishwa uchangiaji umekuwa ukitofautiana kutoka mfanyakazi mmoja hadi mwingine.

Kila mfuko una tafsiri yake ya mchango wa mwanachama


HOTUBA YA RAIS MAGUFULI

Nimeamua niwaite wote ili niwe referee na inawezekana nikawa refaree mbaya

Nisingeweza kuwaita Wafanyakazi wote na tatizo hili naona litafikia mwisho.

Rais Magufuli: Kwenye baraza la Mawaziri tulikubaliana kuinganisha mifuko ya jamii

Hatua hii ilitokana na maombi ya muda mrefu ya vyama vya Wafanyakazi kutaka mifuko iiunganishwe

Watu walijua inaelekea kufa na kweli ilikuwa inaelekea huko

Nimewasikiliza, hapa tunaweza kuongea ikafika jioni. Tunaweza kunaliza yakaletwa mengine na ndio maana nataka tu concentrate sehemu moja. Ndio maana nimeleta regulator ili watoe mawazo yaliyo academic.

Nilipokuwa mwalimu nilianza na mshahara wa 1045, ninapofanya kazi nikataka kustaafu nianze kupata usumbufu naomba sio vizuri ndio maana nimewaita hapa tuzungumze.

Mtakumbuka tarehe 20 Oktoba 2017 baraza la mawaziri tulipitisha kuunganisha mifuko ya kijamii iwe mmoja kwabajili ya watumishi wa umma na NSSF ifanyiwe marekebisho ili iwe kwa ajili ya wafanyakazi wa sekta binafsi.

Sababu ya kuunganisha mifuko hii ni kwamba watu walijua inakwenda kufa na kweli ilikuwa inakwenda kufa.

Kabla ya mifuko kuunganishwa kila mfuko ulikuwa na wanachama wake. Jumla ya wanachama wote ilikuwa milioni 1.2.

Awamu ya tano mifuko ilikuwa hali mbaya na walikuwa wanapigana vita na kugombania wanachama.

Hii mifuko pengine ilikuwa inaendesha kiajabu ajabu. Miradi mingi ikawa inaanzishwa hasa ya majengo. Nenda Dege Eco Village, Kigamboni uangalie majengo yale sasa mwekezaji alikuwa anategemea return gani?

Tulipoingia madarakan tulikuwa deni kubwa la trilioni 1.2, ikabidi tutafuta pesa Serikalini tukaanza kulipa madeni haya na tumelipa yote mpaka March 2017.

Rais Magufuli: Sheria inawataka wapewe kidogokidogo si bora unipe zote nikafe vizuri

Mtu anafanyakazi yake kwa muda wote, halafu anamaliza unamwambia apewe asilimia 25, haiingii akilini. utanipa kidogokidogo? hata Waziri akimaliza Ubunge wake ukimwambia utampa 25% kisha nyingine kidogo kidogo hawezi kukubali

Kuna challanges ambazo hatuwezi kuzikwepa kwenye mifuko hii na ninyi wenyewe mmesema kuwa matatizo yapo

Ni lazima kuzitatua changamoto hizi, mmesema watu wanapenda #Kikokotoo kitoe angalau 50% ya mafao kama ilivyokuwa hapo awali

Wakati wa kuunganisha mifuko wastaafu walikuwa wanadai bilioni 700 na zaidi ya bilioni 500 zimelipwa.

Hii fomula iliyotumiwa na PSPF na NSSF haipo duniani.

Walioiweka ni makatibu wakuu wa wakati ule, sio wakati wangu

Rais Magufuli: Niombe kwenye mifuko waboreshe daftari la wastaafu ili kuondoa wastaafu hewa

Kama tulikuwa na wanafunzi hewa, watumishi hewa, pembejeo hewa hatuwezi kukosa wastaafu hewa

Rais Magufuli: Hifadhi za Jamii zipunguze matumizi ya hovyo, zikiwa fedha za Wastaafu zinatakiwa kulipwa kwa mkupuo hata wa 60% haitawezekana kwasababu hakutakuwa na hizo fedha

Yawezekana tatizo halianzi kwenye kikokotoo bali hata uendeshwaji wa mashirika haya

Nafahamu shirika moja linalotumia bilioni 1.3 kuchapisha kaenda na matangazo. Wanachama hamuwezi kujua kama fedha zenu zinatumika hovyo

Limeajiri walinzi na kuwalipa bilioni 2 kwa mwaka, kama wangeajiri SUMA JKT wangelipa bilioni 1

Nitoe wito kwa watendaji wakuu, tupunguze gharama za uendeshaji wa mifuko. Sasa imebaki mifuko 2 hakuna sababu za kushindana

Wafanyakazi wa Serikali ambao ni wanachama wa NSSF wahamishiwe PSSSF na wale wa sekta binafsi vivyo hivyo

Mashirika yaanze kuangalia namna ya kuongeza wanachama sioni sababu ya NSSF kuwa na wanachama laki nne nchi nzima wakati sekta binafsi inakuwa kila siku

Wale wafanyakazi wa migodi na ujenzi kuna sababu gani ya wao kusubiri hadi miaka 60 wakati kazi zao ni za kipindi kifupi.

Tuongeze option za wanachama. Kustaafu sio dhambi, kustaafu ni heshima lazima mstaafu awe respected

Mwalimu aliyefundisha kwa uaminifu miaka 40 hadi chaki zimemharibia macho na aliowafundisha wamekuwa na mishahara mikubwa na wengine ndio wakurugenzi wa NSSF

Ukitaka kuchukua mafao yake unamwambia nitakupa kidogo ili ukaishi, aliyekwambia nani ataishi?

Nimeamua tuwe na kipindi cha mpito, nimeamua kikokotoo kilichokuwa kinatumika kabla ya mifuko kuunganishwa kiendelee katika kipindi cha miaka yote ya mpito

Kipindi cha mpito ni hadi mwaka 2023 ambapo wanachama wa mfuko 58,000 ndio watastaafu kipindi hicho.

Wanachama watakaokuwa wanastaafu wataendelea na kikokotoo cha 50%

Rais Magufuli: Mimi nitaichungulia hiyo mifuko na nina uhakika Waziri na Katibu Mkuu wa wizara zinazohusika wafuatilie mifuko isitumike hovyo

Katika kipindi hicho watawalipa watu mafao vizuri na kwasababu hali itakuwa imeimarika tutafanya mazungumzo ya mfumo bora

Niakubaliana kuwa si kweli lengo langu mifuko, ndani ya Serikali na vyama vya wafanyakazi mkae mjadili njia bora ya kukokotoa mafao

Mifuko itakuwa imeimarika na itaweza kulipa, hata mkikubaliana kupeana 70% mimi sina neno

Si kweli kwamba lengo langu mifuko ife, ndani ya Serikali na vyama vya wafanyakazi mkae pamoja mjadili njia bora ya kukokotoa mafao

Mifuko itakuwa imeimarika na itaweza kulipa, hata mkikubaliana kupeana 70% mimi sina neno

Viongozi wa wafanyakazi muache kutumiwa na wanasiasa, watakaotumiwa na wanasiasa wataondoka

Mafao yakiwa bora hata wizi na ufisadi utapungua, kwasababu kila mmoja atakuwa anajua kuwa akistaafu atapata fungu lake

Rais J.P.M mtu wa watu. Wafanyakazi Mna kila sababu ya Kuendelea Kumuombea.Live long Mr President.Tanzania Tulikuwa tunahitaji Kiongozi wa nchi wa namna hii.Kiongozi/Rais wa wanyonge.Hakika tumepata Baba.
 
Hongera sana Rais J.P. Magufuli kwa uamuzi wa kuwajali na kuwatetea wafanyakazi, hakika wewe ni Rais wa watanzania wote. Asiyekubali hilo anywe dawa ya usingizi alale . Live long mr President tunakuhitaji sana watanzania.
 
Mbona zipo baadhi ya sekta binafsi zina mishahara mikubwa zaidi ya iyo ya serikali
ni kweli lakini nyingi ni vurugu tu ndugu yangu binafsi nimefanya kampuni moja zaidi ya miaka 10 lakini nilichopata hakilingani na kazi ya miaka 3 wengi wanaumia kwa kweli labda uwe NGO
 
wadau mfano umefanya kazi kwa miaka 10,na ukaachishwa kazi ukiwa na umri wa miaka 40,je kwa mujibu wa hotuba ya rais ya jana,naweza pewa hela yangu yote niliyochangia nssf?kama zamani?
 
wadau mfano umefanya kazi kwa miaka 10,na ukaachishwa kazi ukiwa na umri wa miaka 40,je kwa mujibu wa hotuba ya rais ya jana,naweza pewa hela yangu yote niliyochangia nssf?kama zamani?
Amesema mambo yarudi kama zamani hadi 2023. Ametolea mfano kadhia ya watu wanaofanya kazi za mikataba ya muda mfupi kama miaka 3 hakuna sababu ya kusubiria chao mpaka sijui afikishe miaka 60, wapewe chao wakafie mbele. So fao la kujitoa limerudi.
 
Amesema mambo yarudi kama zamani hadi 2023. Ametolea mfano kadhia ya watu wanaofanya kazi za mikataba ya muda mfupi kama miaka 3 hakuna sababu ya kusubiria chao mpaka sijui afikishe miaka 60, wapewe chao wakafie mbele. So fao la kujitoa limerudi.
asnte mdau,tusubiri wengine
 
Hapana, kilichofutwa ni kanuni ya kikokotoo kipya cha 25% na siyo sheria mpya (iliyofuta fao la kujitoa).

Sent using Jamii Forums mobile app
Watanzania mbona mnakuwa wagumu sana kuelewa? Au hukumsikiliza rais bali umesimuliwa? Kuna vitu vingine sio lazima aviseme kwa kuvirudiarudia. Swala la ajira za muda mfupi kaliongelea tena kwa kutoa na mifano kabisa ya mikataba ya muda mfupi. Sasa sijui mpaka atamke kabisa "fao la kujitoa limerudi" ndio uelewe? Achilia mbali mifano aliyoitoa kuhusu ajira za muda mfupi amesema mambo yarudi kama zamani mpaka 2023. Aisee watanzania bhana!
 
nikopeeni nauli niende arusha nikadai pesa zangu nssf, npo moro wajameni. Ole waniambie utumbo wao mle ndani nitawaua kabisa
 
Duuuu sio poa kujumuisha.kwan ww mrundi
Watanzania mbona mnakuwa wagumu sana kuelewa? Au hukumsikiliza rais bali umesimuliwa? Kuna vitu vingine sio lazima aviseme kwa kuvirudiarudia. Swala la ajira za muda mfupi kaliongelea tena kwa kutoa na mifano kabisa ya mikataba ya muda mfupi. Sasa sijui mpaka atamke kabisa "fao la kujitoa limerudi" ndio uelewe? Achilia mbali mifano aliyoitoa kuhusu ajira za muda mfupi amesema mambo yarudi kama zamani mpaka 2023. Aisee watanzania bhana!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Duuuu sio poa kujumuisha.kwan ww mrundi

Sent using Jamii Forums mobile app
Samahani mkuu. Acha na mimi niji-include, "sisi watanzania ni wagumu sana kuelewa". Rais kaongea tena kwa kutolea mfano "kwenye hizi miradi ya serikali ambayo mkandarasi anajenga kwa muda wa miezi 36, unamwambia mtu asubirie mafao yake mpaka afikishe miaka 60, si umpe hela yake akafie mbele, akifikisha miaka 60 hata mkandarasi mwenyewe anakuwa kesha ondoka, hata nyinyi mifuko ya kijamii hata hamumkumbuki huyu mfanyakazi" mwisho wa kunukuu. Sasa mtu anakuja kusema fao la kujitoa hajaliongelea, aisee! Kweli sisi watanzania ni wagumu wa kuelewa.
 
Back
Top Bottom