Rais Magufuli aamuru Kikokotoo kilichokuwa kinatumiwa awali kiendelee hadi 2023 (kulingana na mfuko husika)

Rais Magufuli aamuru Kikokotoo kilichokuwa kinatumiwa awali kiendelee hadi 2023 (kulingana na mfuko husika)

UPDATES:



Viongozi wa Vyama vya wafanyakazi wametoa historia ya walikotoka hadi walikofika. Aidha, wamedokeza kuwa wapo waliozimia kwenye ofisi za Mifuko ya Hifadhi ya Jamii.

Rais Magufuli anawasikiliza na anataka kila mtu aongee na kutoa dukuduku ili aweze kuongea.

Viongozi wa vyama vya wafanyakazi (upande wa walimu) wanadai kikokotoo kimekuwa ni suala kubwa na Rais Magufuli kama mwalimu anatambua changamoto za walimu. Wanamwomba Rais aliangalie suala la kikokotoo kwa jinsi atakavyoweza kwakuwa wanajua anaweza na kwa wanavyomsaidia Mungu atamsaidia alitatue hili.

TUGHE: Tunakupongeza Mhe. Rais, lakini tunapenda ufahamu kuwa wastaafu wengi hawakuwa wameandaliwa na mabadiliko haya yametokea ghafla na kusababisha negative impact. Morali ya kazi imeshuka!

Waziri Mhagama
Hoja na kuunganisha mifuko ilikuwa ni hoja ya wafanyakazi.

Hapa tunazungumza tu kikokotoo, ili tupate kikokotoo lazima turudi kwenye contribution rate, tukitaka tuendelee na kikokotoo cha 50% contribution itabidi itoke kwenye 20% hadi 25%.

TUCTA: Tunafahamu kwa moyo wako na unavyowasaida wanyonge. Tunaamini utasaidia kutatua

Mwanzo Wastaafu walikuwa wanapata 50% kwa mkupuo na 50% kidogo kidogo kila mwaka

Tulipendekeza mkupuo uwe 40% na si 25%


CHAMA CHA WALIMU: Suala la kikokotoo ni shida, hakuna asiyejua shida za waalimu. Uzuri ni kwamba hata wewe Rais ni Mwalimu

Kwasasa hata mishahara ya mwisho wa mwezi haitoshi. Kwa namna unavyofanya mambo makubwa najua hata hili unaliweza


TUGHE: Wastaafu wengi hatukuwaandaa kisaikolojia. Mabadiliko haya ya kikokotoo cha mafao yametokea kwa ghafla sana.

Wafanyakazi wa umma waliowengi wanalalamika nakuomba mheshimiwa Rais uongee chochote ili Wafanyakazi warudi kwenye morali ya kazi

TUICO: Watu wa sekta binafsi kima chao cha chini ni 100,000. Ili kwenda vizuri kamati itakayoundwa ikachunguze hii mishahara

Pia kuna fao la kupoteza ajira hawalipwi na makampuni mengi yanaondoka bila ya kuwalipa


WAFANYAKAZI WA RELI: Tumepitia misukosuko sana ikiwemo mishahara kuwa kidogo na ulipwaji wake ni wa kusuasua sana

Tulitegemea mafao ya kustaafu yatusaidie kujenga nyumba ili hata tukifa tufe vizuri.

Ile 50% ya awali kama haiwezekani basi tunakubali iwe 40%


TAMICO: Kwenye suala la kikokotoo kuna shida hasa kwenye fao la kujitoa ambalo mbadala wake ni fao la kukosa ajira

Sekta binafsi tunapata shida kwasababu kazi zetu si za muendelezo. Tunaomba iwepo tofauti kwa watu wa sekta ya migodi na ujenzi kwenye fao la kukosa ajira


SERIKALI ZA MITAA: Tunapenda mifuko iwe imara lakini kwa mishahara yetu hii midogo kwa kweli inaumiza

Rais kelele ni nyingi sana, na kwa kikokotoo hiki mfanyakazi akistaafu atashindwa hata kujenga


CHAMA CHA WAAJIRI: Sheria hii ya mifuko ya jamii, ililenga kuiweka mifuko hii kuwa katika hali ya usawa

Baada ya mifuko kuunganishwa uchangiaji umekuwa ukitofautiana kutoka mfanyakazi mmoja hadi mwingine.

Kila mfuko una tafsiri yake ya mchango wa mwanachama


HOTUBA YA RAIS MAGUFULI

Nimeamua niwaite wote ili niwe referee na inawezekana nikawa refaree mbaya

Nisingeweza kuwaita Wafanyakazi wote na tatizo hili naona litafikia mwisho.

Rais Magufuli: Kwenye baraza la Mawaziri tulikubaliana kuinganisha mifuko ya jamii

Hatua hii ilitokana na maombi ya muda mrefu ya vyama vya Wafanyakazi kutaka mifuko iiunganishwe

Watu walijua inaelekea kufa na kweli ilikuwa inaelekea huko

Nimewasikiliza, hapa tunaweza kuongea ikafika jioni. Tunaweza kunaliza yakaletwa mengine na ndio maana nataka tu concentrate sehemu moja. Ndio maana nimeleta regulator ili watoe mawazo yaliyo academic.

Nilipokuwa mwalimu nilianza na mshahara wa 1045, ninapofanya kazi nikataka kustaafu nianze kupata usumbufu naomba sio vizuri ndio maana nimewaita hapa tuzungumze.

Mtakumbuka tarehe 20 Oktoba 2017 baraza la mawaziri tulipitisha kuunganisha mifuko ya kijamii iwe mmoja kwabajili ya watumishi wa umma na NSSF ifanyiwe marekebisho ili iwe kwa ajili ya wafanyakazi wa sekta binafsi.

Sababu ya kuunganisha mifuko hii ni kwamba watu walijua inakwenda kufa na kweli ilikuwa inakwenda kufa.

Kabla ya mifuko kuunganishwa kila mfuko ulikuwa na wanachama wake. Jumla ya wanachama wote ilikuwa milioni 1.2.

Awamu ya tano mifuko ilikuwa hali mbaya na walikuwa wanapigana vita na kugombania wanachama.

Hii mifuko pengine ilikuwa inaendesha kiajabu ajabu. Miradi mingi ikawa inaanzishwa hasa ya majengo. Nenda Dege Eco Village, Kigamboni uangalie majengo yale sasa mwekezaji alikuwa anategemea return gani?

Tulipoingia madarakan tulikuwa deni kubwa la trilioni 1.2, ikabidi tutafuta pesa Serikalini tukaanza kulipa madeni haya na tumelipa yote mpaka March 2017.

Rais Magufuli: Sheria inawataka wapewe kidogokidogo si bora unipe zote nikafe vizuri

Mtu anafanyakazi yake kwa muda wote, halafu anamaliza unamwambia apewe asilimia 25, haiingii akilini. utanipa kidogokidogo? hata Waziri akimaliza Ubunge wake ukimwambia utampa 25% kisha nyingine kidogo kidogo hawezi kukubali

Kuna challanges ambazo hatuwezi kuzikwepa kwenye mifuko hii na ninyi wenyewe mmesema kuwa matatizo yapo

Ni lazima kuzitatua changamoto hizi, mmesema watu wanapenda #Kikokotoo kitoe angalau 50% ya mafao kama ilivyokuwa hapo awali

Wakati wa kuunganisha mifuko wastaafu walikuwa wanadai bilioni 700 na zaidi ya bilioni 500 zimelipwa.

Hii fomula iliyotumiwa na PSPF na NSSF haipo duniani.

Walioiweka ni makatibu wakuu wa wakati ule, sio wakati wangu

Rais Magufuli: Niombe kwenye mifuko waboreshe daftari la wastaafu ili kuondoa wastaafu hewa

Kama tulikuwa na wanafunzi hewa, watumishi hewa, pembejeo hewa hatuwezi kukosa wastaafu hewa

Rais Magufuli: Hifadhi za Jamii zipunguze matumizi ya hovyo, zikiwa fedha za Wastaafu zinatakiwa kulipwa kwa mkupuo hata wa 60% haitawezekana kwasababu hakutakuwa na hizo fedha

Yawezekana tatizo halianzi kwenye kikokotoo bali hata uendeshwaji wa mashirika haya

Nafahamu shirika moja linalotumia bilioni 1.3 kuchapisha kaenda na matangazo. Wanachama hamuwezi kujua kama fedha zenu zinatumika hovyo

Limeajiri walinzi na kuwalipa bilioni 2 kwa mwaka, kama wangeajiri SUMA JKT wangelipa bilioni 1

Nitoe wito kwa watendaji wakuu, tupunguze gharama za uendeshaji wa mifuko. Sasa imebaki mifuko 2 hakuna sababu za kushindana

Wafanyakazi wa Serikali ambao ni wanachama wa NSSF wahamishiwe PSSSF na wale wa sekta binafsi vivyo hivyo

Mashirika yaanze kuangalia namna ya kuongeza wanachama sioni sababu ya NSSF kuwa na wanachama laki nne nchi nzima wakati sekta binafsi inakuwa kila siku

Wale wafanyakazi wa migodi na ujenzi kuna sababu gani ya wao kusubiri hadi miaka 60 wakati kazi zao ni za kipindi kifupi.

Tuongeze option za wanachama. Kustaafu sio dhambi, kustaafu ni heshima lazima mstaafu awe respected

Mwalimu aliyefundisha kwa uaminifu miaka 40 hadi chaki zimemharibia macho na aliowafundisha wamekuwa na mishahara mikubwa na wengine ndio wakurugenzi wa NSSF

Ukitaka kuchukua mafao yake unamwambia nitakupa kidogo ili ukaishi, aliyekwambia nani ataishi?

Nimeamua tuwe na kipindi cha mpito, nimeamua kikokotoo kilichokuwa kinatumika kabla ya mifuko kuunganishwa kiendelee katika kipindi cha miaka yote ya mpito

Kipindi cha mpito ni hadi mwaka 2023 ambapo wanachama wa mfuko 58,000 ndio watastaafu kipindi hicho.

Wanachama watakaokuwa wanastaafu wataendelea na kikokotoo cha 50%

Rais Magufuli: Mimi nitaichungulia hiyo mifuko na nina uhakika Waziri na Katibu Mkuu wa wizara zinazohusika wafuatilie mifuko isitumike hovyo

Katika kipindi hicho watawalipa watu mafao vizuri na kwasababu hali itakuwa imeimarika tutafanya mazungumzo ya mfumo bora

Niakubaliana kuwa si kweli lengo langu mifuko, ndani ya Serikali na vyama vya wafanyakazi mkae mjadili njia bora ya kukokotoa mafao

Mifuko itakuwa imeimarika na itaweza kulipa, hata mkikubaliana kupeana 70% mimi sina neno

Si kweli kwamba lengo langu mifuko ife, ndani ya Serikali na vyama vya wafanyakazi mkae pamoja mjadili njia bora ya kukokotoa mafao

Mifuko itakuwa imeimarika na itaweza kulipa, hata mkikubaliana kupeana 70% mimi sina neno

Viongozi wa wafanyakazi muache kutumiwa na wanasiasa, watakaotumiwa na wanasiasa wataondoka

Mafao yakiwa bora hata wizi na ufisadi utapungua, kwasababu kila mmoja atakuwa anajua kuwa akistaafu atapata fungu lake
Hii NAYO mnaiita hoy poloy!
 
Silaha ndio hizi ...kila kinachosemwa ...Mtukufu Rais anatekeleza!
 
mods naomba msiunganishe uzi huu ili nipate majibu sahihi maana hotuba ya Mhe Rais imenichanganya hapa, nachotaka kujua mimi ni je Fao la kujitoa kwa wafanyakazi wa miakataba mifupi hasa wale wa sekta binafsi ambao wana mikataba mifupi

Je fao hili limerudishwa?

Maana naona watu wanashangilia tu pasipo kujua kuhusu fao hili.
Mbona limeeleweka hilo
Sent using Jamii Forums mobile app
 
mods naomba msiunganishe uzi huu ili nipate majibu sahihi maana hotuba ya Mhe Rais imenichanganya hapa, nachotaka kujua mimi ni je Fao la kujitoa kwa wafanyakazi wa miakataba mifupi hasa wale wa sekta binafsi ambao wana mikataba mifupi

Je fao hili limerudishwa?

Maana naona watu wanashangilia tu pasipo kujua kuhusu fao hili.

Sent using Jamii Forums mobile app
I'm still contemplating[emoji2822][emoji2822][emoji2822]

Sent using Jamii Forums mobile app
 
hakuna fao la kujitoa ila kuna kujitoa uanachama na kuchukua michango yako ndio hiyo itaendelea untill 2023 kwa hiyo ni kucheza na hii ngoma tu kabla 2023 😛😛😀😀
Hilo limezungumzwa wapi!??

Au wewe una Rais wako!??
 
Kikokoto Cha ZZK ni lekudute , Cha Sumaye kujikopesha yeye Mwenyewe, kikokoto Cha mwenyekiti wa saccos ni kujikopesha kwa ajili ya Biashara zake.
 
Bwanamkubwa kapata la kufungia mwaka. anamaliza mwaka akiwa shujaa anasifiwa. makofi na vigeregere kwake. kama ilivyo kawaida yake anatengeneza tatizo kisha analaumu watangulizi . anatufanya fyatu hatuna akili. kwakuwa tumezoea kusifia tutasifia .... haijawahi kutokea? .... ni raisi wa pekee... hamnazo.
kama nilimsikia vizuri bwana haambiliki alisema kikotoo kimeahirishwa hadi 2020 nasi twashangilia kama kumeza panadol kupunguza maumivu mnashangilia nini?
Mwaka wa tatu baada ya raisi kuingia madarakani 2015 hakuna nyongeza ya mishahara wala maslahi mengine huku hali na gharama za maisha zikiwa zimepanda sana kuanzia kodi ya pango mpaka nauli za kwenda kazini. watumishi wananyanyaswa wanaitwa majina mabaya kila uchao.
swali langu kwa viongozi wa vyama MLIKUWA MNASHANGILIA NINI PALE IKULU?
watumishi wa umma wa Tanzania amkeni hakuna viongozi wanaowajali ni waigizaji tuu
Hakuna alichofanya cha maana kwa sababu hicho kikokotoo alikipitisha yeye, alichofanya leo ni Kampeni ya Uchaguzi wa Serikali za Mitaa na ule wa Rais, Wabunge na Madiwani. Mnadanganywa kweli mnadanganyika.
 
Mheshimiwa Rais wetu;

Mimi ni moja kati ya Watanzania wengi tunaounga mkono jitihada zako za kuleta mabadiliko Tanzania. Nakupongeza kwa ujasiri, kutomwonea mtu aibu, kuthubutu, na kukiri hadharani kwamba Tanzania haina sababu ya kuendelea kuwa masikini... bravooo!!

Kwa upande mwingine, naona kuwa namna yako ya kufanya maamuzi na utendaji unawadhoofisha wateule wako kama Mawaziri, Makatibu Wakuu, Na Wakurugenzi. Kwa mfano, maamuzi kuhusu MAFAO Na KIKOKOTOZI cha mifuko ya Pensheni; ni maamuzi mazuri lakini ungeacha wateuzi wako; ususani Waziri husika alishughulikie hilo. Kwa wewe kutoa kauli ya mwisho inawafanya wateuzi wako kuonekana hawafanyi wajibu wao ipasavyo Na pia unawaondolea ujasiri wa kufanya maamuzi makubwa.

Mheshimiwa naomba uangalie namna bora ya kutimiza ndoto zote nzuri ulizonazo kwa ajili ya Taifa letu.

Mungu mbariki Rais JPM, Mungu ibariki Tanzania.

Asante.
 
Leo nimemsikiliza Rais Magufuli wakati wa mkutano na viongozi wa wafanyakazi ameongea vitu vingi ikiwemo kukosoa miradi mingi iliyofanywa na hii mifuko ya hifadhi ya jamii ambayo haina tija kwa hilo nampongeza.

lakini kilichonishangaza ni yeye leo hii kujitenga na maamuzi ya serikali kuhusu kikokotoo cha wastaafu akisema yeye leo alikuwa refalii kati ya serikali na wafanyakazi, swali la kujiuliza hicho kitendo alimtuma waziri kupima upepo? na kama ni hivyo baada ya kuona upepo siyo mzuri na kuwafanya wapinzani waonekane wanapigania maslahi ya wananchi akaamua kujitenga na maamuzi yaliyofanywa na waziri wake?


My take, wale wenye upeo mdogo ndiyo watamshangilia lakini ukweli ni kwamba tatizo amelitengeneza yeye na wabunge wake wa ccm sasa leo anajificha kwenye kivuli cha waziri as if yeye alikuwa likizo.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kwa kweli hapa wapinzani Magufuli katupiga bao
Sijui wewe ni Malay wa aina gani. Wapinzani ndo walistukia hiki kikokotoo kibovu na wakakipinga kwa nguvu leo hii mmetatua tatizo mlilotengeneza wenyewe then unakuja hapa unashangilia Kama zuzu
 
Safi hawa viwavi wamezoea kula pesa za wafanyakazi.
Yaani kutengeneza Kalenda tu wanatumia Bil. 1.5
Na nina uhakika hao ni NSSF, hawa wanaongoza kwa miradi hewa na ili isiyo na tija.
Dawa yao iko jikoni


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Safi jembe langu, msikivu na mtetezi wa wanyonge
Watu kama wewe ndio wapumbavu wa kwanza, ambao hamna tofauti na viongozi wa vyama vya wafanyakazi Rais anaosema wanatumika kisiasa.
Kila kukicha ni kusifia tu jembe lako hata kama kafanya upuuzi, walipo leta 25% ulisifia wenye akili wakakosoa leo rais kusema 25% iwe suspended baada ya kuwaelewa wenye akili unasifia tena.
Bora ungekuwa nyama uwe kitoweo


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom