Rais Magufuli aamuru Kikokotoo kilichokuwa kinatumiwa awali kiendelee hadi 2023 (kulingana na mfuko husika)

Rais Magufuli aamuru Kikokotoo kilichokuwa kinatumiwa awali kiendelee hadi 2023 (kulingana na mfuko husika)

nimeanzisha uzi huu kabisa kumpongeza rais wetu kwa maamuzi yake ya leo.
tunahitaji Rais msikivu na anayejali maslahi ya Taifa na ustawi wa wananchi wake. Hili rais wangu umelionyesha bila kusita.

pia umegusia hata fao muda maalum kama wafanyakazi wa migodi au kazi za muda

niseme ukweli kabisa napenda upinzani sutawi lakini utendaji wako hauna shaka kabisa.
sisemi hatuhitaji upinzani ila tunahitaji upinzani wa mawazo mbadala na kuboresha zaidi

pi a natumia nafasi hii kumpongeza mbunge wa chadema aliyesimamia swala la kanuni ya kikokotoo kuingia kwenye sheria.

Tanzania yetu ni moja na sisi sote ni wamoja. hongera wapinzani na hongera Rais wetu

pia hongera wa elimu bur watoto wa masikini kule kijiji umefanya difference kubwa sana, pia hongera kwa mradi wa kimara to kibaha na pia hongera kwa stand ya ubungo.

maamuzi ya leo umegusa wengi na umeonyesha namna gani unaelewa haki


kama umeguswa na maamuzi ya leo ema kitu hapa
Ina maana huyu Rais ni tofauti na yule aliyesaini hiyo Sheria ? Ninachofahamu ni kwamba Rais kabla ya kusaini alipewa taarifa ya kutosha kuhsu hiyo Sheria na matokeo yake, kwa hiyo siwezi kutoa Pongezi kwake kwa sababu yeye ndiye aliyeanzisha hilo tatizo, hivyo ni wajibu wake kuliondoa> Aidha, hakukuwa na sababu yoyote ya kuwaita Viongozi wa Vyama vya Siasa na kuutangazia umma, alipaswa kuwagiza Waziri aliyeandaandaa hicho kukokotoo akifute kama liavyokiandaa, vinginevyo, acheni kufanya siasa katika maisha ya watu. Fanya kazi kwa bidii, uonekane na kuteliuwa kuwa DC lakini sio kutafuta sifa kwa kusifu haya maigizo.
 
Yaani magu anapenda matukio+Kiki.
tatizo alilianzisha mwenyewe ili limjengee ki siasa huko mbeleni. akajifanya kama haelewi kinachoendelea;
akawaacha wapinzani walipigieh kelele ili lizidi kupata kiki....
baada ya muda

[emoji23] [emoji23] [emoji23]
kajifanya kuita makamera na kulisolve .
daaah ngoja tusubiri episode zingine.

AMINI NA WAAMBIA 2019 NDIYO MTAONA KILA AINA YA MUVI.
kwa ajili ya kupata Mtaji wa kisiasa

Sent using Jamii Forums mobile app
 
lumumba inaingiaje hapa. au wewe hujui mzigo waliokuwa nao ndugu zetu sababu ya kikokotoo
lumumba inaingiaje hapa. au wewe hujui mzigo waliokuwa nao ndugu zetu sababu ya kikokotoo
Okay, nijibu kwanza sasa ili swali,hicho kikokotoo wakina nani walikibadirisha kama sio CCM walioshika dola, baada ya kuona kelele za watumishi ni nyingi jiwe ndo anazuga kuita mkutano ikulu na kutengua,wauaji wakubwa nyie!
 
Si kawaida yangu kupongeza pasipostahili kupongeza au kukosoa pasipostahili kukosoa, ila leo kwa dhati ya moyo wangu, nakupongeza Rais wangu John Pombe Magufuli au JPM kwa hili la Kikokotoo, kwa kurejesha 50% kwa mifuko iliyokuwa ikitoa 50 na ile ya iliyokuwa ikitoa 25% ibaki hivyo hivyo na 25% katika kipindi cha mpito hadi mwaka 2023.
Nimekusikiliza hatua kwa hatua, na kusoma lugha ya mwili wako, hakika umejiweka kwenye nafasi ya mfanyakazi, na kuyabeba machungu na maumivu ya kiakili na kisaikolojia waliyopitia tangu kutangazwa kwa kanuni mpya ya mifuko ya Hifadhi ya Jamii.

Nasema asante Rais wangi. Nimefurahi zaidi ulipowaeleza wabunge wetu ukweli mchungu kuwa kama sheria hii ya 25% ingepelekwa Bungeni kuwahusu wao, hakika wasingeipitisha. Rais umesimama katikati ya wafanyakazi wa taifa hili. Umezungumza kama Baba. Ni jambo ambalo lilikuwa haliingii akilini, na wewe umesema halileti logic, kwamba nimetumikia nchi kwa uaminifu mkubwa, ninapostaafu unanipa 25% halafu unaniambia hizo zingine nitakupa kidogo kidogo hadi ufe.
Sielewi wasomi wetu wanafikiri kwa ubongo gani. Ninapostaafu, na pengine kwa uaminifu wangu sijaweza kujenga hata kakibanda, natakiwa nikalipe kodi, nisomeshe watoto, niachane na gari ya umma nipande daladala, sasa nilitaraji hiko nilichojikusanyia kingenisaidia kuweka hata kakibanda au kabiashara, unaniwekea masharti magumu, ambayo wakati najiunga na mifuko hukuniambia. Ndio maana nasema asante sana Rais wangu JPM.

Sasa tutakula mwaka mpya kwa raha mustarehe hadi lile jino la Krismas litaonekana. Asante Rais wangu, ile stress ya miezi kadhaa waliotupa hawa watu wa mifuko ya Hifadhi ya Jamii sasa inaondoka. Lakini baba, usimame hivyo hivyo ili kipindi cha mpito kikimalizika 2023 wasije tena na hadithi za ujanja ujanja au za Alinacha au Abunuasi ambazo hazina maslahi kwa mfanyakazi anapostaafu. Wewe ni Rais wetu, kwa hili nasema asante sana ila mishahara sekta binafsi kwa baadhi ya sekta ni hairidhishi na ndio msingi wa mahesabu. Wakija hiyo 2023, waje pia na fomula ya mishahara na kikokotoa.

Mungu akubariki
Unampongeza mtu aliyesaini sheria mbovu una walakini medulani oblangatan!
 
raha sana! ukiwa umeajiriwa na serikali au shirika la umma wewe ni kama mtoto wa familia bora usipolizika unajiliza kisha baba anakuja kukubembeleza!

sasa njoo huku sekta binafsi ikiwa mshahara 300,000 ni hiyo tu na haitegemei kupanda na hakuna huduma zingine kama matibabu

changamoto ya maisha haya inakuja pale kazi inapokwisha uishi maisha binafsi kama haukujipanga na kwa bahati mbaya ulikuwa na kipato kidogo na nyongeza ulichelewa kuoa na kujenga familia hivyo mtoto wa kwanza yuko form two!

hivyo nawashauri tumieni fursa ya kuajiriwa kukopa na kuwekeza sio kununua vigari kila kukicha hatuoni wivu lakini ndo ukweli tulioko huku tunaona fursa mnazo sana kuzidi mnavyofikiria.

hivi kuna tabu gani ukakopa ukanunua bajaji ukatumia kama 7,000,000/- mpaka 8,000,000 kwa siku ukapata 20,000 ambazo kwa mwaka ukapata 7,200,000/- inayotosha kusimamisha nyumba ndogo ya kupangisha ya vyumba viwili mpaka linta? tutaendelea nina mteja kwanza
Nadhani mteja ameshaondoka, Endeleza somo.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Tulikwambia ukashupaza shingo, haya sasa yako wapi?
Jiuzulu hiyo nafasi ya uwaziri hutufai

Sent using Jamii Forums mobile app
Sio huyo tu mpaka wale wote wa SSRA inapaswa waachie nafasi maana walikuwa wanaongea utumbo mno mpaka jpm akasema wanaongea too theoretical.

Jenista na ssra walikuwa wanaongea mambo ambayo cjui wameyatoa wapi.
 
Ina maana huyu Rais ni tofauti na yule aliyesaini hiyo Sheria ? Ninachofahamu ni kwamba Rais kabla ya kusaini alipewa taarifa ya kutosha kuhsu hiyo Sheria na matokeo yake, kwa hiyo siwezi kutoa Pongezi kwake kwa sababu yeye ndiye aliyeanzisha hilo tatizo, hivyo ni wajibu wake kuliondoa> Aidha, hakukuwa na sababu yoyote ya kuwaita Viongozi wa Vyama vya Siasa na kuutangazia umma, alipaswa kuwagiza Waziri aliyeandaandaa hicho kukokotoo akifute kama liavyokiandaa, vinginevyo, acheni kufanya siasa katika maisha ya watu. Fanya kazi kwa bidii, uonekane na kuteliuwa kuwa DC lakini sio kutafuta sifa kwa kusifu haya maigizo.
Sheria vs Kanuni
 
Wanaomchukia naona wako kimyaaa? Nachojilaumu mimi sikumpigia kura ile octoba 25,huwa najiona sikumtendea haki.hakika huyu ni Rais wa wanyonge.bado bomu la ajira baba.. Achia japo kidogo tu..
Screenshot_20181210-131135.jpeg


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mtu anatengeneza tatizo mwenyewe halafu kesho anakuja kulitatua,unampongeza?Kesho serikali ikisema mtalipa kodi ya kichwa,mtalalamika!Kesho kutwa yake ikaja serikali kusema inaondoa kodi hiyo mtashangilia na kusifu kuwa mmepewa zawadi ya mwaka mpya!
 
Tatizo LA wapinzani ni kupinga hadi mafanikio, ama kweli kwa JPM, wapinzani wataisoma namba, Jamaaa anakandamiza vibayaaa. Big up JPM. Tupo nawe bega kwa bega
Haha sa hv wanaanza kusema rais anaogopa cheche za Lisu wanahamisha magoli tu a.k.a wanatapatapa
 
Unampongeza mtu aliyesaini sheria mbovu una walakini medulani oblangatan!
Yaani Mkuu duniani hapa hakun majitu majinga kama matumishi ya umma! Hili taahira linashangilia nini sasa? Ina maana aliyesaini hakuiona kama sheria haikuwa na aina ya ukandamizaji? Shame on him!!
 
Mleta hoja sikuungi mkono eneo la kuwa-under rate sub-ordinate wake kwani wamefanya vibaya na intervention ilikuwa lazima. Kwa maneno mengine kafanya vyema na ikibidi awaswage wote waliohusika kutengeneza kanuni ile!
 
Back
Top Bottom