Rais Magufuli aamuru Kikokotoo kilichokuwa kinatumiwa awali kiendelee hadi 2023 (kulingana na mfuko husika)

Rais Magufuli aamuru Kikokotoo kilichokuwa kinatumiwa awali kiendelee hadi 2023 (kulingana na mfuko husika)

CCM ni watu wa jabu sana, Inasikitisha sana kuona jinsi ambavyo wanatengeneza tatizo halafu wanalitatua ili kujitafutia KIKI hasa ktk kipindi hiki cha kuelekea uchaguzi wa serikali za mitaa (2019) na uchaguzi mkuu (2020). Janga yenu tumeing’amua. Huwezi kuwa na wasaidizi wako unawatuma waje waharibu halafu wewe ujitokeze kusawazisha mambo. Ni aibu kubwa sana. Mtu mzima ukijivua nguo kwa makusudi huna sababu ya kuchutama. Tembea wima watu waone uchi wako.
 
"Hivi yeye hakuwa sehemu ya walioipendekeza hiyo sheria? Je, aliyeisaini na kuruhusu ianze kutumika ni nani?"

Create a problem, then solve it....

Halafu mnatuona wafanyakazi kama hatuna akili vile. Tunajua tu, na 2019 ngonjera za mishahara mizuri zitaanza.
 
m nipo tofauti kidogo ...napata mashaka kilichoangaliwa hapa ni uchaguzi serikali za mitaa na uchaguzi wa mwaka 2020...halafu watakuja na kauli kwamba wameshindwa kuelewana so sheria ibaki palepale.....cha muhimu wafanyakazi waendelee kukaza mpaka sheria ifutwe kwanza ...hiyo 2023 waje na muswada mpya.......je 2023 akisema iwe 15% na atakua anaondoka zake madarakani......msiseme hamkukumbushwa........
 
Kama wafanyakazi wenyewe ndo hawa wanaopongeza basi ni halali kupewa 25%.

Ujinga umeshamiri sana Tz kwakweli
 
HONGERA KWA ZAWADI NZURI KWA WAFANYAKAZI MH.RAIS.

By Mwl.Osunga Jr.

Mwaka 1949 bada ya muda mrefu wa vita na hatimaye mapinduzi ya CHINA yaliyochochewa na Communist party kilichoongozwa na Mao Tse Tung dhidi ya chama cha mabeberu cha Kumunitang kilichoonzwa na Kaishek Isen.
Mao aliweza kuutangazia umma wa wachina waliokuwa wakulima na wafanyakazi zaidi ya asilimia 80 kuwa China itakuwa nchi ya wakulima na wafanyakazi.
Kwa nukta hiyo mitaala ya Elimu ilibadilishwa na vitabu vikaandikwa upya vilivyokuwa vinazungumzia umuhimu wa wafanyakazi pamoja na wakulima.

Mapinduzi haya yalitanguliwa na Yale ya Urusi (Russian Revolution) ya mwaka 1917,October.yaliyochochewa na Bolshevik party kilichoongozwa na V.I.Lenin baada ya kupata uungwaji mkono kutoka kwa wakulima na wafanyakazi waliokuwa wakipata mateso na manyanyaso kutoka kwa Tanaka tawala
Hivyo Lenin akaitangaza Urusi kuwa nchi ya kijamaa.

Sera za kijaamaa ziliendelea kuingia katika nchi nyingi za Kiafrika kwa majina yao mfano, Humanism pale Zambia, Common Man's Charter pale Uganda, Harambee pale Kenya na hapa kwetu tulikiuwa na Ujamaa na kujitegemea.

Mwaka 1962 mpango mkakati wa uchumi wa 1962-1966 ulionesha sisi lazima tuachane na Sera za kibebari na kufuata Sera za kijamaa, ilichukua muda hadi 1967 ambapo kwenye mkutano wa pale Arusha ulipitisha Azimio la Arusha lililoonesha sasa mlengo wetu kiuchumi, tukiwa tunaendelea kutambua mchango wa wakulima na wafanyakazi.

Mwaka 1977 kiliundwa chama cha mapinduzi ambacho ni muunganiko wa TANU na ASP chama hiki kipya kilikuwa na nembo inayoonesha jembe na nyundo.Ikiashiria tutaendelea kuwajali wafanyakazi.

Alichokifanya Rais Leo ndo maana halisi ya CCM, na ndo maana ya Ujamaa lazima tuendelee kuwajali na kuwaathamini watu hawa.

Baaada ya zawadi hii nzuri ya Rais kwa wafanyakazi naomba pia Rais chetu kipenz afanye pia haya.
a)Awaongeze wafanyakazi hawa mishahara kwa kazi kubwa wanayoifanya.
b)Afungulie ajira kwa kada mbalimbali ikiwemo Ualimu kwani Sera ya Elimu bure imefanya kuwepo kwa ongezeko kubwa la wanafunzi na kuchochea upungufu wa walimu.
Kwa wanaokwambia walimu wametosha wanataka uteuzi Mh. Walimu hawapo.
c) Pitia tena ruzuku za wakulima na kuhimiza wakurugenzi wawapeleke maafisa kilimo vijijini kutoka semina za kilimo na si kukaa tuu ofisi.

Baada ya ushahuri huo kama taifa bado tuko vizuri, tunapaswa tena kujipanga na kufika wenzetu.

Hakika Rais naona moyo wa Mao, Lenini, Bismarck na Roosevelt ndani yako.
Nawaomba watanzania tuunge mkono jitihada hizo.l

0756231744
BASAM..
Hapa kwenye heading sijakuelewa unaposema zawadi una maanisha nini.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Huyu mtu wa hovyo sana. Anatengua kitu kwa utaratibu wake badala ya kupeleka hoja bungeni sheria irekebishwe. Ndiyo hivyo tena ukiwa na kikojozi subiri watu washuhudie godoro likianikwa.
 
Full umakaveli. Mchiavelli anasema kuwa mtu akitaka kudannganya hawezi kosa watu wa kuwadanganya.

Pia anasema ki9ngozi mnjanja akipata nafasi anatengeneza tatizo, kisha analitatua na kupata sifa kemkem.
 
TUNDU LISSU anajua kuzipanga vizuri Karata zake
 
UPDATES:



Viongozi wa Vyama vya wafanyakazi wametoa historia ya walikotoka hadi walikofika. Aidha, wamedokeza kuwa wapo waliozimia kwenye ofisi za Mifuko ya Hifadhi ya Jamii.

Rais Magufuli anawasikiliza na anataka kila mtu aongee na kutoa dukuduku ili aweze kuongea.

Viongozi wa vyama vya wafanyakazi (upande wa walimu) wanadai kikokotoo kimekuwa ni suala kubwa na Rais Magufuli kama mwalimu anatambua changamoto za walimu. Wanamwomba Rais aliangalie suala la kikokotoo kwa jinsi atakavyoweza kwakuwa wanajua anaweza na kwa wanavyomsaidia Mungu atamsaidia alitatue hili.

TUGHE: Tunakupongeza Mhe. Rais, lakini tunapenda ufahamu kuwa wastaafu wengi hawakuwa wameandaliwa na mabadiliko haya yametokea ghafla na kusababisha negative impact. Morali ya kazi imeshuka!

Waziri Mhagama
Hoja na kuunganisha mifuko ilikuwa ni hoja ya wafanyakazi.

Hapa tunazungumza tu kikokotoo, ili tupate kikokotoo lazima turudi kwenye contribution rate, tukitaka tuendelee na kikokotoo cha 50% contribution itabidi itoke kwenye 20% hadi 25%.

TUCTA: Tunafahamu kwa moyo wako na unavyowasaida wanyonge. Tunaamini utasaidia kutatua

Mwanzo Wastaafu walikuwa wanapata 50% kwa mkupuo na 50% kidogo kidogo kila mwaka

Tulipendekeza mkupuo uwe 40% na si 25%


CHAMA CHA WALIMU: Suala la kikokotoo ni shida, hakuna asiyejua shida za waalimu. Uzuri ni kwamba hata wewe Rais ni Mwalimu

Kwasasa hata mishahara ya mwisho wa mwezi haitoshi. Kwa namna unavyofanya mambo makubwa najua hata hili unaliweza


TUGHE: Wastaafu wengi hatukuwaandaa kisaikolojia. Mabadiliko haya ya kikokotoo cha mafao yametokea kwa ghafla sana.

Wafanyakazi wa umma waliowengi wanalalamika nakuomba mheshimiwa Rais uongee chochote ili Wafanyakazi warudi kwenye morali ya kazi

TUICO: Watu wa sekta binafsi kima chao cha chini ni 100,000. Ili kwenda vizuri kamati itakayoundwa ikachunguze hii mishahara

Pia kuna fao la kupoteza ajira hawalipwi na makampuni mengi yanaondoka bila ya kuwalipa


WAFANYAKAZI WA RELI: Tumepitia misukosuko sana ikiwemo mishahara kuwa kidogo na ulipwaji wake ni wa kusuasua sana

Tulitegemea mafao ya kustaafu yatusaidie kujenga nyumba ili hata tukifa tufe vizuri.

Ile 50% ya awali kama haiwezekani basi tunakubali iwe 40%


TAMICO: Kwenye suala la kikokotoo kuna shida hasa kwenye fao la kujitoa ambalo mbadala wake ni fao la kukosa ajira

Sekta binafsi tunapata shida kwasababu kazi zetu si za muendelezo. Tunaomba iwepo tofauti kwa watu wa sekta ya migodi na ujenzi kwenye fao la kukosa ajira


SERIKALI ZA MITAA: Tunapenda mifuko iwe imara lakini kwa mishahara yetu hii midogo kwa kweli inaumiza

Rais kelele ni nyingi sana, na kwa kikokotoo hiki mfanyakazi akistaafu atashindwa hata kujenga


CHAMA CHA WAAJIRI: Sheria hii ya mifuko ya jamii, ililenga kuiweka mifuko hii kuwa katika hali ya usawa

Baada ya mifuko kuunganishwa uchangiaji umekuwa ukitofautiana kutoka mfanyakazi mmoja hadi mwingine.

Kila mfuko una tafsiri yake ya mchango wa mwanachama


HOTUBA YA RAIS MAGUFULI

Nimeamua niwaite wote ili niwe referee na inawezekana nikawa refaree mbaya

Nisingeweza kuwaita Wafanyakazi wote na tatizo hili naona litafikia mwisho.

Rais Magufuli: Kwenye baraza la Mawaziri tulikubaliana kuinganisha mifuko ya jamii

Hatua hii ilitokana na maombi ya muda mrefu ya vyama vya Wafanyakazi kutaka mifuko iiunganishwe

Watu walijua inaelekea kufa na kweli ilikuwa inaelekea huko

Nimewasikiliza, hapa tunaweza kuongea ikafika jioni. Tunaweza kunaliza yakaletwa mengine na ndio maana nataka tu concentrate sehemu moja. Ndio maana nimeleta regulator ili watoe mawazo yaliyo academic.

Nilipokuwa mwalimu nilianza na mshahara wa 1045, ninapofanya kazi nikataka kustaafu nianze kupata usumbufu naomba sio vizuri ndio maana nimewaita hapa tuzungumze.

Mtakumbuka tarehe 20 Oktoba 2017 baraza la mawaziri tulipitisha kuunganisha mifuko ya kijamii iwe mmoja kwabajili ya watumishi wa umma na NSSF ifanyiwe marekebisho ili iwe kwa ajili ya wafanyakazi wa sekta binafsi.

Sababu ya kuunganisha mifuko hii ni kwamba watu walijua inakwenda kufa na kweli ilikuwa inakwenda kufa.

Kabla ya mifuko kuunganishwa kila mfuko ulikuwa na wanachama wake. Jumla ya wanachama wote ilikuwa milioni 1.2.

Awamu ya tano mifuko ilikuwa hali mbaya na walikuwa wanapigana vita na kugombania wanachama.

Hii mifuko pengine ilikuwa inaendesha kiajabu ajabu. Miradi mingi ikawa inaanzishwa hasa ya majengo. Nenda Dege Eco Village, Kigamboni uangalie majengo yale sasa mwekezaji alikuwa anategemea return gani?

Tulipoingia madarakan tulikuwa deni kubwa la trilioni 1.2, ikabidi tutafuta pesa Serikalini tukaanza kulipa madeni haya na tumelipa yote mpaka March 2017.

Rais Magufuli: Sheria inawataka wapewe kidogokidogo si bora unipe zote nikafe vizuri

Mtu anafanyakazi yake kwa muda wote, halafu anamaliza unamwambia apewe asilimia 25, haiingii akilini. utanipa kidogokidogo? hata Waziri akimaliza Ubunge wake ukimwambia utampa 25% kisha nyingine kidogo kidogo hawezi kukubali

Kuna challanges ambazo hatuwezi kuzikwepa kwenye mifuko hii na ninyi wenyewe mmesema kuwa matatizo yapo

Ni lazima kuzitatua changamoto hizi, mmesema watu wanapenda #Kikokotoo kitoe angalau 50% ya mafao kama ilivyokuwa hapo awali

Wakati wa kuunganisha mifuko wastaafu walikuwa wanadai bilioni 700 na zaidi ya bilioni 500 zimelipwa.

Hii fomula iliyotumiwa na PSPF na NSSF haipo duniani.

Walioiweka ni makatibu wakuu wa wakati ule, sio wakati wangu

Rais Magufuli: Niombe kwenye mifuko waboreshe daftari la wastaafu ili kuondoa wastaafu hewa

Kama tulikuwa na wanafunzi hewa, watumishi hewa, pembejeo hewa hatuwezi kukosa wastaafu hewa

Rais Magufuli: Hifadhi za Jamii zipunguze matumizi ya hovyo, zikiwa fedha za Wastaafu zinatakiwa kulipwa kwa mkupuo hata wa 60% haitawezekana kwasababu hakutakuwa na hizo fedha

Yawezekana tatizo halianzi kwenye kikokotoo bali hata uendeshwaji wa mashirika haya

Nafahamu shirika moja linalotumia bilioni 1.3 kuchapisha kaenda na matangazo. Wanachama hamuwezi kujua kama fedha zenu zinatumika hovyo

Limeajiri walinzi na kuwalipa bilioni 2 kwa mwaka, kama wangeajiri SUMA JKT wangelipa bilioni 1

Nitoe wito kwa watendaji wakuu, tupunguze gharama za uendeshaji wa mifuko. Sasa imebaki mifuko 2 hakuna sababu za kushindana

Wafanyakazi wa Serikali ambao ni wanachama wa NSSF wahamishiwe PSSSF na wale wa sekta binafsi vivyo hivyo

Mashirika yaanze kuangalia namna ya kuongeza wanachama sioni sababu ya NSSF kuwa na wanachama laki nne nchi nzima wakati sekta binafsi inakuwa kila siku

Wale wafanyakazi wa migodi na ujenzi kuna sababu gani ya wao kusubiri hadi miaka 60 wakati kazi zao ni za kipindi kifupi.

Tuongeze option za wanachama. Kustaafu sio dhambi, kustaafu ni heshima lazima mstaafu awe respected

Mwalimu aliyefundisha kwa uaminifu miaka 40 hadi chaki zimemharibia macho na aliowafundisha wamekuwa na mishahara mikubwa na wengine ndio wakurugenzi wa NSSF

Ukitaka kuchukua mafao yake unamwambia nitakupa kidogo ili ukaishi, aliyekwambia nani ataishi?

Nimeamua tuwe na kipindi cha mpito, nimeamua kikokotoo kilichokuwa kinatumika kabla ya mifuko kuunganishwa kiendelee katika kipindi cha miaka yote ya mpito

Kipindi cha mpito ni hadi mwaka 2023 ambapo wanachama wa mfuko 58,000 ndio watastaafu kipindi hicho.

Wanachama watakaokuwa wanastaafu wataendelea na kikokotoo cha 50%

Rais Magufuli: Mimi nitaichungulia hiyo mifuko na nina uhakika Waziri na Katibu Mkuu wa wizara zinazohusika wafuatilie mifuko isitumike hovyo

Katika kipindi hicho watawalipa watu mafao vizuri na kwasababu hali itakuwa imeimarika tutafanya mazungumzo ya mfumo bora

Niakubaliana kuwa si kweli lengo langu mifuko, ndani ya Serikali na vyama vya wafanyakazi mkae mjadili njia bora ya kukokotoa mafao

Mifuko itakuwa imeimarika na itaweza kulipa, hata mkikubaliana kupeana 70% mimi sina neno

Si kweli kwamba lengo langu mifuko ife, ndani ya Serikali na vyama vya wafanyakazi mkae pamoja mjadili njia bora ya kukokotoa mafao

Mifuko itakuwa imeimarika na itaweza kulipa, hata mkikubaliana kupeana 70% mimi sina neno

Viongozi wa wafanyakazi muache kutumiwa na wanasiasa, watakaotumiwa na wanasiasa wataondoka

Mafao yakiwa bora hata wizi na ufisadi utapungua, kwasababu kila mmoja atakuwa anajua kuwa akistaafu atapata fungu lake

Du sasa Zitto sijui ataongea nini ,maana yeye na wenzake walitaka kuifanya issue ya mafao mtaji wa kisiasa kama ilivyo kawaida yao,sasa watabaki kuhangaika na katuni za mwenzao Kipanya za FastJet
 
alizungumzia vizuri sana. Amesema migodini na kwenye contractors, ajira ni za muda wa miaka miwili mitatu, haingii akilini kuambiwa usubiri mafao yako hadi ufikishe umri wa miaka 60!.
P.
Yaaap, basi hapo kalipangua , ina maana lipo Tena
Guuud president
 
Mpaka 2023? ? Baada ya hapo inakuwaje? ? Nyie shangilieni tu kama mazuzu
 
Back
Top Bottom