Rais Magufuli afanya uteuzi wa viongozi watatu wa Tume ya Maendeleo ya Ushirika (TCDC)

Rais Magufuli afanya uteuzi wa viongozi watatu wa Tume ya Maendeleo ya Ushirika (TCDC)

beth

JF-Expert Member
Joined
Aug 19, 2012
Posts
3,881
Reaction score
6,377
Rais John Magufuli amefanya uteuzi wa viongozi watatu wa Tume ya Maendeleo ya Ushirika, uteuzi ambao ulianza rasmi Januari 30 mwaka huu.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Katibu Mkuu wa Wizara ya Kilimo walioteuliwa ni Dkt. Benson Otieno Ndiege ambaye amekuwa Mrajis wa Vyama vya Ushirika Tanzania na Mtendaji Mkuu wa Tume ya Maendeleo ya Ushirika.

Wengine walioteuliwa ni, Mulande Charles Msolwa, ambaye amekuwa Naibu Mrajis wa Vyama vya Ushirika Tanzania-Uhamasishaji na Uratibu, na Nyakunga Collins Bernedict ambaye amekuwa Naibu Mrajis wa Vyama vya Ushirika Tanzania-Ukaguzi na Usimamizi.

1582007987859.png
 
Back
Top Bottom