Rais Magufuli ahudhuria maadhimisho ya miaka 100 ya mahakama kuu

Rais Magufuli ahudhuria maadhimisho ya miaka 100 ya mahakama kuu

Analogia Malenga

JF-Expert Member
Joined
Feb 24, 2012
Posts
5,108
Reaction score
10,191
Rais John Magufuli amehudhuria maadhimisho ya miaka 10 ya Mahakama Kuu nchini.

Magufuli amesema mahakama kuu ilianzishwa Januari 3, 1921 wakati Tanganyika ikiwa koloni la uingereza.

Rais ametoa pole kwa watumishi wamahakama ambao wamefariki dunia.

Pia Rais amesisitiza kwa somo la Historia kuwa somo la lazima kuwa kuna baadhi ya watu wanabeza maendeleo yaliyotokana na uhuru.

====
RAIS MAGUFULI: KASI YA USIKILIZAJI KESI IMEONGEZEKA

Akizungumza katika Maadhimisho ya Siku ya Sheria na Miaka 100 ya Mahakama Kuu, Rais wa Tanzania, Dkt. John Magufuli amesema katika miaka ya hivi karibuni, kasi ya kusikiliza kesi imeongezeka na tatizo la mrundikano wa kesi/mashauri limepungua kwa kiasi kikubwa

Amesema, katika miaka mitano iliyopita Serikali imeanzisha Mahakama Kuu Divisheni ya Uhujumu Uchumi na kufanya Divisheni kuwa nne ikiwa ni pamoja na Biashara, Ardhi na Kazi

Amesema, "Kama mnavyofahamu mwaka jana Nchi yetu imeingia Uchumi wa Kati, hivyo tutahakikisha mambo yetu yanafanana na Nchi yenye Uchumi wa Kati, sio tu kwenye Mahakama bali kwenye Taasisi zote za Serikali

Hata hivyo, Rais Magufuli ameeleza kuwa, bado kuna changamoto zinazoukabili mfumo wa utoaji Haki na Sheria Nchini, ikiwemo mrundikano wa wafungwa na mahabusu magerezani

 
Nampenda sana Rais wangu Magufuli kwa uwazi wake na ukweli, hana unafiki wa kumun'unya maneno anapo ona ukweli, sio mnafiki. wakuu wa mihimili mingine waige tabia ya Mh. Rais.

matumizi ya Kiswahili ni kwa manufaa ya Watanzania. hongera sana kwa Jiji aliye pandishwa kwa kutumia kiswahili kuandika hukumu, hakika Jaji huyu ni mzalendo wa kuigwa, Mungu amjaalie siku moja awe Jaji Mkuu.
 
Mbona wakati inaanzisjwa hiyo Mahakama kuu,jina Tanzania halikuwepo.
 
Leo Magu kampandisha cheo jaji kwa kuwa tuu ameandika hukumu moja kwa Kiswahili, ule utaratibu wa kupandisha vyeo mahakamani hauna maana tena mbele ya "the rock"
Pia kwa mara ya kwanza amezungumzia watu kumsema hajui kiingereza
Sema Mahakama na sio Mahakamani.
 
Kauli na maelekezo ya Rais kwa Mahakama zote nchini kuendesha kesi na kutoa maelezo ya hukumu ni jambo la msingi sana. Mahakama ndiyo mahala pekee ambapo haki inapaswa kuonekana kutendeka kwa ukamilifu wake. Hivyo pamoja na ushahidi na uendeshaji wa mashauri na misingi mingineyo ya kisheria ni muhimu katika kufikia uamizi wa haki.

Kwangu mimi suala la lugha, desturi na mila ni vitu muhimu sana katika uendeshaji wa mashauri mahakamani. Hivyo msisitizo wa Rais John Pombe Magufuli kuhusu matumizi ya kiswahili ni jambo la muhimu sana katika kufikia uamuzi wa haki.

Kiswahili kinaeleweka na kila mtu na lugha iliyoleta uhuru nchini na ukombozi katika Afrika na kwa sasa ni lugha inayotumika katika mahusiano ya kimataifa na biashara duniani. Hivyo hakuna sababu ya kuibeza.

Lakini pia ni lugha ya Taifa kwa muda mrefu sasa ikiunganisha Taifa la Tanzania na hata na majirani yetu. Mahakama zingatieni sana wito huu ili kuanzia sasa mashauri yote yaendeshwe kwa kiswahili pamoja na hukumu zake. Hiki kitakuwa ni kielelezo cha taifa huru linalojitambua.

Ni mahakama pekee imebakia kutumia kiingereza katika maandiko yake tena maneno mengine ya kilatini na kigriki hali ambayo hata sisi wengine tunaojua kiingereza hutukwaza.Aidha, maandiko ya kimahakama yafanyiwe tafsri na BAKITA kurahisisha kazi hii.
 
Jaji Warioba ni mtu muhimu sana kwa historia ya Tanzania - Rasimu yake ya Katiba ndiyo imebeba HAKI za watanzania hawa - ila ipo kabatini hadi muda huu!! sasa ukitaka kuwaudhi CCM we watajie "katiba mpya"

Na mtu wa tatu atakayekuwa maarufu katika historia a Tanzania baada a Mwalimu na Jaji Warioba ni Rais atayewapatia watanzania Katiba Mpya

Watu muhimu kwa sasa kwa historia ya Tanzania
1 Mwalimu Julias Kambarage Nyerere (Mkombozi / Baba wa Taifa)
2 Jaji Joseph Sinde Warioba ( Rasmu yake ya katiba)
3 Rais atakayewapatia watanzania Katiba mpya itokanayo na Rasimu ya Jaji warioba (Rais mwana mageuzi)
 
Niliwahi andika siku za karibuni humu kwamba hakuna fani iliyokua rahisi kuwekwa kwenye kiswahili kutoka kingereza kama sheria na nikasema imechukua miaka karibu 60 watu wetu wakisikilizwa mashauri kwa kingereza kwenye mahakama zetu kutokana na kasumba ya kuenzi kizungu kwa wanasheria wetu.

Leo rais alivyokua anaelekeza wanasheria kwamba lazima sasa kesi ngazi zote zisikilizwe kwa kiswahili na taarifa za hukumu kutolewa kwa kiswahili mtu aliyeangalia matangazo ya moja kwa moja leo angeona jinsi wanasheria walivyoshindwa kushangilia kwa moyo agizo hilo na kuna mama mmoja alionekana anasikitika.

Wanasheria wetu wengi wako kwenye fani hiyo kama kazi tu kupata riziki na sio wenye moyo wa kutoa haki kwa wenye kustahili. Wanaona kingereza ni moja ya mikogo na mizungu ya kumfanya mteja kupata butwa na kuacha hakimu au jaji kuamua atakavyo.

Sasa ni amri tunataka haki iwe inasimamiwa na kutolewa kwa lugha kila mwananchi anaelewa. Pia binafsi nampongeza rais wetu kwa kumsifia na kumpongeza jaji wa mahakama kuu aliyesikiliza kesi na kuitolea hukumu kwa kiswahili kwa mara ya kwanza. Isitoshe rais akampandisha cheo jaji huyo kua jaji wa mahakama ya rufaa. Hii kwa kweli inadhihirisha jinsi magufuli alivyokua rais bora kabisa kwa maslahi ya wananchi wa kawaida.
 
Niliwahi andika siku za karibuni humu kwamba hakuna fani iliyokua rahisi kuwekwa kwenye kiswahili kutoka kingereza kama sheria na nikasema imechukua miaka karibu 60 watu wetu wakisikilizwa mashauri kwa kingereza kwenye mahakama zetu kutokana na kasumba ya kuenzi kizungu kwa wanasheria wetu...
[emoji1656][emoji1656][emoji1656][emoji1656][emoji1656]
 
Kwani sheria zikiandikwa kwa kiswahili zitabadili nini kama msingi wake wa awali katika lugha chanzi niwa kunyima haki za watu.
 
Tatizo sio lugha bali utoaji wa haki. Lugha ni sehemu ndogo sana ya tatizo halisi la hizo mahakama.
 
Back
Top Bottom