Rais Magufuli aidha amedanganywa kuhusu Barakoa au kuna tatizo sehemu (kwa alichoongea leo Feb 21, 2021)

cha msingi wasiwe wanapewa nafasi ya kuongea kwenye nyumba za ibada
 
Ninavyomjua Magufuli hili suala la kutilia shaka usalama wa barakoa lazima atalithibitisha kwa vitendo.

Ninamaanisha ataanzisha "movie" kuonesha kuwa imported masks si salama kama alivyotuonesha mwaka jana kuwa mfumo na teknolojia zinazotumiwa na maabara ya taifa kupima korona hazitoi majibu ya kuaminika ili abaki kuwa mkweli. Tusubiri na tutaona!
 
Inaelekea mheshimiwa saaana rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Muinjilisti John Pombe Magufuli ana ugomvi binafsi na barakoa.

Tatizo ni kuwa ugomvi huo ni ugomvi binafis, na siye wananchi tunasema hivi sisi binafsi hatuna ugomv na barakoa na wala hatuna haja ya kurithi maadui.

Mheshimiwa raisi kama anahisi barakoa ni adui, basi ni adui yake yeye binafsi sisi ni rafiki yetu.

Sasa kwa mfano atatushauri vipi tuone barakoa siyo Issue wakati juzi hapa tumeona walinzi wanamlinda raisi Kikwete wamezivaa, tumemuona makamu wa raisi mstaafu amezivaa, na hata wanajeshi waliobeba jeneza la Maalim wamezivaa?

Huo ushauri wa barakoa za nje kuwa hazifai ni kwa ajili yetu sisi tu malaymen au hata Madaktari wanaotutibia nao waache kuzivaa pindi wawapo theatre?.

Je mheshimiwa raisi pindi akiona madaktari wamevaa barakoa wakati wa kuwatibu wagonjwa kimoyomoyo anawaona kama watu wasio na imani timilifu kwa Mungu ambaye anadhani atawalinda tu bila hata kuvaa hizo barakoa?

Ndiyo maana wananchi mitandaoni wanapendekeza mheshimiwa rais akutanishwe na barokoa ili wamalize tofauti zao.

Wazungu wanasema, We don't have a dog in this fight, kwa maana kwamba ugomvi huu siye wala hautuhusu!

Mheshimiwa raisi, anasema tusiamini barakoa za nje, wakati hizo barakoa zimejaa tele kwenye maduka ya dawa na serikali iishachukua kodi yake kwa walioziagiza, Je vyombo vya uthibiti ubora na forodha havikuwa na taarifa kuwa hizo bidhaa zinaingia nchini?, Kama hilo linajulikanabona hatujaona operesheni ya kufika kwenye maduka hayo kuzikusanya na kuziharibu?

Kwenye ugomvi huu wa mheshiiwa raisi na Barakoa, wananchi tumegoma, tumekataa, hatutaki Sisi hatununui ugomvi binafsi.

Unasema tuchukue tahadhari halafu wakati huohuo unatwambia aulindaye uhai wake ataupoteza!. Mheshimiwa rais unatuconfuse totally!

Mheshimiwa rais kwenye hili jipange wewe na timu yako mje upya, kwa heshima na taadhima kubwa kwa mamlaka uliyonayo napenda kusema kuwa hii double talk ya kudunisha, kudiscredit barakoa wananchi tumeikataa na badala yake tunakushauri umalize tofauti zako na barakoa, na uanze kuivaa ili ujilinde!

Mheshimiwa rais Corona ni hatari jihadhari, wasikilize wataalamu!
 
Kama anasema kuwa tutakufa tu kwa nini yeye amejipiga chanjo and his concubines .
 

Aisee. Inawezekana Rais anapodai “anayajua mengi” basi ni huku ndiko anakopatia hizo “alternative facts” anazoziamini sana? This is utter trash.

Kama kweli haya ndiyo aina ya maandiko yanayotumika na mkulu katika maamuzi kuhusu masuala muhimu ya kitaifa basi tumepata hasara isiyomithilika. Tusubiri rehema ya Mwenyenzi Mungu tu.
 
Sasa mtu kama huyu anataka Raisi amkalie kimya.

Ujinga tu. Unafanya mambo ya kisiasa kwenye dini,
Raisi akitumia kanisa kuwashambulia nyinyi wenye imani haba mnalalamika eti kachafua madhabahu. Acheni kumchokoza[emoji57][emoji52]
yeye kasema madhabauni kwan??
 
Natamani kumuuliza kwanini ulipokuwa France ulikuwa ukivaa barakoa lakini umerudi nchini huvai? Covid iliyopo France ndiyo hiyo hiyo iliyopo Tanzania kwanini unachezea uhai wako? Unamfurahisha/unamuogopa nani kwa kutovaa barakoa?
Kabudi akirudi atavua barakoa kumfurahisha bosi wake ingawa kwa umri wake yupo kwenye target ya corona virus.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…