Kuna jamaa mwenzetu alikuwa anaenda kufunga ndoa, akaomba ruhusa ya wiki mbili. Walimu wenzake tulitoa michango yetu kama kawaida. Baada ya wiki mbili yule jamaa akarudi na mke wake. Washikakaji zake tulikuwa na hamu ya kumuona bib harusi,tukaenda kuona kiwango. Tulipotoka pale jamaa mmoja akaniambia "Yaani bwana Idako huyu ndiyo mke wa kuoa?! Ingekuwa rahisi huyu alikuwa ni wa kucharaza bakora huku anaulizwa, 'tulikutuma mke wa hivi? Ee, huyu ni mke wa kuoa? Si tunakuuliza?'"
Hii ya Magufuli inanikumbusha maneno ya mshikaji yule.Ingekuwa rahisi, Magufuli alikuwa ni wa kucharaza bakora huku anaulizwa, tulikutuma mawaziri wa hivi? Akina Prof Maghembe? Si tunakuuliza?