Rais Magufuli akamilisha uteuzi wa Baraza la Mawaziri, Makame Mbarawa abadilishiwa Wizara

Rais Magufuli akamilisha uteuzi wa Baraza la Mawaziri, Makame Mbarawa abadilishiwa Wizara

Mi nimemwelewa JPM, kwa ajili ya kuharmonize mambo ulikuwa ni lazma apatikane MTU kutoka kaskazni especially Kilimanjaro so hakuwa na namna

Ndo hicho ila bora angemchukua mwanry kuliko huyu ...hana msaada
 
Uwongo siyo kitu kizuri. Huyo Mama mmoja aweze kufelisha waislamu wote?
Aisee tafuta namna ya kujieleza iwe na nafasi kwenye vichwa vya watu, Great thinkers!

Hivi ck hizi kwenye mitihani mnaandika majina au ni index numbers. Maana sijui kuna namba zinazoonyesha kuwa mwanafunzi ni muislam au mkirsto au mpagani. Au mna nia ya kumchafua huyu mama tu
 
...huyo mama analalamikiwa na nani zaidi ya majungu; kama vipi ijumaa andamaneni baada ya sala yenu..

tutaandamana kwenye box la kura,haiwezekani mtu analalamikiwa na watu karibu milioni 20 bado tena unamrudisha
 
Hakyanani kwa Magembe ndio kachemsha, huyo ni jipu


Ati mkoa huo na dini hiyo ipate waziri. Hakai muda na akitaka afanye sherehe mapemaaa ili aifanye na hiyo nyingine siku si nyingi. Kinana alishasema huu ni mzigo
 
Labda kawekwa ili ile kanda yetu isikose mtu katika baraza lake.
 
kweli MAWAZO YANGU kuwa Ndalichako apewe Wizara ya ELIMU yamezingatiwa, Hongera Dr Magufuli KWA hilo japo kuhusu Maghembe ninawasiwasi hiyo NAMBA inavuja KABLA ya mechi kuanza, hapo umeliwa Rais wangu.

Japo wengi uliowateua wako vizuri ila KWA Prof Maghembe umekwenda Mrama, time will tell, bora hata ungempa Ngeleja au Kagasheki hiyo Wizara. Time will tell, pia Ndalichako angefaa zaidi TAMISEMI kuliko Wizara ya ELIMU.
 
prof muhongo ana record nzuri ya utendaji lakini prof maghembe sijui labda niwe nimesahau..

Mhongo anatuhumiwa kwa ufisadi mkubwa ingekuwa nchi nyingine asingepata uwaziri double standard kwa baadhi ya watu. Ccm hakuna msafi ka ni wagonjwa wote mahutihuti tu
 
Akimwondoa Manyanya hapo Elimu itakuwa poa. Kwa kuwa, pamoja na kutoka TAMISEMI, ameonyesha kuboronga mbaya.
Elimu itaongozwa na ma-junior kisiasa. Sina wasiwasi na ushawishi wa Ndalichako kwenye Cabinet. Uchafu wa ma-distinction na pass za GPA ya 0.3 utupwe jalalani.
 
Ndani ya mwezi mmoja Magufuli ameshaanza kupangua Baraza lake alilolitengeneza kwa zaidi ya mwezi mmoja.


Hii ni ishara ya kukurupuka.
 
Kuna jamaa mwenzetu alikuwa anaenda kufunga ndoa, akaomba ruhusa ya wiki mbili. Walimu wenzake tulitoa michango yetu kama kawaida. Baada ya wiki mbili yule jamaa akarudi na mke wake. Washikakaji zake tulikuwa na hamu ya kumuona bib harusi,tukaenda kuona kiwango. Tulipotoka pale jamaa mmoja akaniambia "Yaani bwana Idako huyu ndiyo mke wa kuoa?! Ingekuwa rahisi huyu alikuwa ni wa kucharaza bakora huku anaulizwa, 'tulikutuma mke wa hivi? Ee, huyu ni mke wa kuoa? Si tunakuuliza?'"

Hii ya Magufuli inanikumbusha maneno ya mshikaji yule.Ingekuwa rahisi, Magufuli alikuwa ni wa kucharaza bakora huku anaulizwa, tulikutuma mawaziri wa hivi? Akina Prof Maghembe? Si tunakuuliza?
 
Mhongo anatuhumiwa kwa ufisadi mkubwa ingekuwa nchi nyingine asingepata uwaziri double standard kwa baadhi ya watu. Ccm hakuna msafi ka ni wagonjwa wote mahutihuti tu

afadhali muhongo ni smart kuliko hili zee kilaza hili
 
Back
Top Bottom