stephot
JF-Expert Member
- Mar 1, 2012
- 17,216
- 26,225
Ila wadau naona mnamsifia mama Joisi,lakini kuna mambo lazima tuyaangalie kwa mapana
KWANZA:Joisi anakuja wizarani tayar ameshaingia kwenye siasa,nafasi anayoshika ni ya kisiasa na si ya kiutendaji teeeena,so utendaji wake utakua ni wa kisiasa siasa,ni afadhali angekua Katibu Mkuu wa Wizara.
PILI:Joisi anaingia wizarani tayar kuna sera mbovu kabisa ya elimu ya mwaka 2014,so anakuja kuitekeleza sera mboooovu kabisa ambayo ukweli haina tija kwa mustakabali wa elimu Tanzania,je ataleta maajabu chini ya sera hii?tukukumbuke hii sera imepitishwa mwaka jana tu na hata wadau weengi wa elim bado hawajaijua,hiko ni kisiki kingine.
TATU:Joisi anakuja wizarani tayari viwango vya ufaulu kwa sekondari vimeshapangwa,je atavibadili tena?je mabosi wake watakubali? Ambao ni (CCM na MAMLAKA ZA JUU YAKE).
Nne:Mtihani wa kwanza kwa Joisi ni suala la ada elekezi kwa shule binafsi,sote tunajua hizi shule binafsi nyiiingi ni za hawa tunaowaita vigogo hukohuko kwenye system,je Joisi atafanikiwa hilo?
TAno:Ili Joisi afanikiwe yule profesa pale wizarani aondolewe kwanza (Katibu mkuu wizara ya elimu) maana haendani na spidi ya serikali hii,na ni chanzo cha changamoto kadhaa,lakini poa wizara ya elimu jamani ingepaswa kuwa na manaibu wawili,hilo halikwepeki kabisa,maana kuna.mambo ya shule za awali (nasari na praimari),kuna elim sekondari,kuna vyuo vya ufundi na ualim na kuna vyuo vikuu,pagumu hapo!!!
MWisho,namtakia kila la kheri mama Joisi,lakini namkumbusha now ameshakua mwanasiasa kamili,NEKTA ilikua taasisi ndogo nowana wizara,asije kuharibu hata ya NECTA tukayasahau
Kwa muono wangu wa harakaharaka mawaziri wa JPM wana power sio kama wa awamu iliopita ambapo makatibu wakuu ndio walikuwa na sauti.