Entreprenegro
JF-Expert Member
- Apr 6, 2012
- 601
- 132
Kwa maoni yangu hapa naona Magufuri amekosea. Magufuri alitakiwa kumtoa yule babu (Profesa Mchome) ambae alikuja kuisadia CCM ku-introduce Division V na badala yake nafasi yake ingechukuliwa na Ndalichako. Nafasi ya Katibu Mkuu ambayo ndiyo ya utendaji ndo ilikuwa bora zaidi kwa Ndalichako kuliko nafasi ya waziri ambayo ni ya kisiasa! And trust, wote mnaofurahia hivi sasa; huyu mama atakuja kuwaboa ndani ya mwaka mmoja tu... SAVE THE POST!
Lakini kwa upande mwingine, Magufuri anatakiwa kuwa makini sana na hizi nafasi zake 10 za wabunge manake ni mapema mno kuwa ameshateua takribani wabunge 5 au sita wakati hata miezi 3 bado! Hofu yangu ni kwamba, nafasi zake 10 zinaweza kwisha mapema halafu bado akatakiwa ku-outsource nje ya bunge ili kupata waziri pale waliopo watakaposhindwa kuendelea na nafasi zao kutokana na sababu moja au nyingine! Kwa kuchelea hilo, ndipo watendaji wazuri kama akina Ndalichako walitosha kabisa na kuwa na manufaa makubwa kuwateua kuwa makatibu wakuu kuliko kuwa waziri!
Boss serikali ya sasa waziri lazima uwe mtendaji. Sio kama ulivokalili kwamba waziri ni siasa. Lazima ujue unaends kusimamia nini katika hiyo sekta. Sio unachagua chagua hata vimada katika sekta nyeti unategemea maendeleo kwa sababu ni nafasi ya kisiasa. Na kuhusu kuteuwa ni matakwa yake kikatiba hakuna mtu atakayemshinikiza hata alipoapishwa siku ile ile angeteuwa wote 10, hakuna tatizo.