Rais Magufuli akamilisha uteuzi wa Baraza la Mawaziri, Makame Mbarawa abadilishiwa Wizara

Rais Magufuli akamilisha uteuzi wa Baraza la Mawaziri, Makame Mbarawa abadilishiwa Wizara

Kwa maoni yangu hapa naona Magufuri amekosea. Magufuri alitakiwa kumtoa yule babu (Profesa Mchome) ambae alikuja kuisadia CCM ku-introduce Division V na badala yake nafasi yake ingechukuliwa na Ndalichako. Nafasi ya Katibu Mkuu ambayo ndiyo ya utendaji ndo ilikuwa bora zaidi kwa Ndalichako kuliko nafasi ya waziri ambayo ni ya kisiasa! And trust, wote mnaofurahia hivi sasa; huyu mama atakuja kuwaboa ndani ya mwaka mmoja tu... SAVE THE POST!

Lakini kwa upande mwingine, Magufuri anatakiwa kuwa makini sana na hizi nafasi zake 10 za wabunge manake ni mapema mno kuwa ameshateua takribani wabunge 5 au sita wakati hata miezi 3 bado! Hofu yangu ni kwamba, nafasi zake 10 zinaweza kwisha mapema halafu bado akatakiwa ku-outsource nje ya bunge ili kupata waziri pale waliopo watakaposhindwa kuendelea na nafasi zao kutokana na sababu moja au nyingine! Kwa kuchelea hilo, ndipo watendaji wazuri kama akina Ndalichako walitosha kabisa na kuwa na manufaa makubwa kuwateua kuwa makatibu wakuu kuliko kuwa waziri!

Boss serikali ya sasa waziri lazima uwe mtendaji. Sio kama ulivokalili kwamba waziri ni siasa. Lazima ujue unaends kusimamia nini katika hiyo sekta. Sio unachagua chagua hata vimada katika sekta nyeti unategemea maendeleo kwa sababu ni nafasi ya kisiasa. Na kuhusu kuteuwa ni matakwa yake kikatiba hakuna mtu atakayemshinikiza hata alipoapishwa siku ile ile angeteuwa wote 10, hakuna tatizo.
 
Dr ndalichako usituangushe sasa wengi tunategemea makubwa kutoka kwako.futa hayo madivision five,brn zinadumaza watoto,mitihani ya dini waachieni mashehe na mapadri watarajiwa.
 
mods acheni tunataka rais akipita apate maoni yetu.
Mimi kama RAIA na kwa mujib wa katiba ya muungano naruhusiwa kutoa maoni yangu, pia Nina haki kuuungwa mkono kwa hoja yangu.

Mimi sikubaliani na uteuzi wa Joyce ndalichako kutokana namna alivofanya katika baraza la mitihani kwa kufelisha baadhi ya wanafunzi waliosoma Islamic knowledge iliopelekea kuundwa tume bayo hadi Leo hatukapata majibu take
" Mimi magufuli nitatenda haki, sitabagua MTU kutokana na chama chake,kabila lake,dini yke,ukanda wake"
sasa mimi kama mwananchi nakuletea malalamiko kwako mh rais juu ya uteuzi wa Joyce Ndalichako

Mm nilidhani amewafelisha physics au math kumbe somo lenu la IS
 
Aisee! Naona unaendeshwa na ushabiki zaidi kuliko uhalisia!Yaani kwa hayo maelezo yenu yanayotawaliwa zaidi na ushabiki ni kana kwamba serikali ya Magufuri itakuwa ndo serikali ya kwanza duniani kutokuwa na wazembe au uzembe katika utendaji! Labda tu nikukumbushe, hata huyo Baba wa Taifa, Mwalimu Nyerere ambae anasifika kwa ukali na kutumuonea mtu haya; bado serikalini alikuwa na watendaji wazembe! Tuache kumjazia Magufuri sifa za as if yeye ni mwanadamu wa kipekee duniani... we support him but we also know yeye bado ni mwanadamu sawa na mwanadamu mwingine yeyote kwahiyo kuonesha kila anachofanya yeye ni perfect wala haisaidii!

Ulitaka ateuliwe bibi yako
 
Tumpe nafasi huyu na tumuunge mkono mama akafanye kazi tuliyokuwa tunataka, na ni mapema sana pia kuanza kukosoa. Nakumbuka wapo watu maarufu humu walimzungumzia Mh. Rais alipokuwa mgombea na kumuita mtu asiyekuwa na maono na wengine walifikia kumuita 'just a mere manager' na watu walifurahia sana, sasa sijui wale walioandika vile wanayakumbuka yale maandishi yao tena. Rais anajua kwanini amemteua na nafas ya katibu mkuu kwa Mchome muda unahesabika tuvute subra.
 
Ila wadau naona mnamsifia mama Joisi,lakini kuna mambo lazima tuyaangalie kwa mapana
KWANZA:Joisi anakuja wizarani tayar ameshaingia kwenye siasa,nafasi anayoshika ni ya kisiasa na si ya kiutendaji teeeena,so utendaji wake utakua ni wa kisiasa siasa,ni afadhali angekua Katibu Mkuu wa Wizara.
PILI:Joisi anaingia wizarani tayar kuna sera mbovu kabisa ya elimu ya mwaka 2014,so anakuja kuitekeleza sera mboooovu kabisa ambayo ukweli haina tija kwa mustakabali wa elimu Tanzania,je ataleta maajabu chini ya sera hii?tukukumbuke hii sera imepitishwa mwaka jana tu na hata wadau weengi wa elim bado hawajaijua,hiko ni kisiki kingine.
TATU:Joisi anakuja wizarani tayari viwango vya ufaulu kwa sekondari vimeshapangwa,je atavibadili tena?je mabosi wake watakubali? Ambao ni (CCM na MAMLAKA ZA JUU YAKE).
Nne:Mtihani wa kwanza kwa Joisi ni suala la ada elekezi kwa shule binafsi,sote tunajua hizi shule binafsi nyiiingi ni za hawa tunaowaita vigogo hukohuko kwenye system,je Joisi atafanikiwa hilo?
TAno:Ili Joisi afanikiwe yule profesa pale wizarani aondolewe kwanza (Katibu mkuu wizara ya elimu) maana haendani na spidi ya serikali hii,na ni chanzo cha changamoto kadhaa,lakini poa wizara ya elimu jamani ingepaswa kuwa na manaibu wawili,hilo halikwepeki kabisa,maana kuna.mambo ya shule za awali (nasari na praimari),kuna elim sekondari,kuna vyuo vya ufundi na ualim na kuna vyuo vikuu,pagumu hapo!!!
MWisho,namtakia kila la kheri mama Joisi,lakini namkumbusha now ameshakua mwanasiasa kamili,NEKTA ilikua taasisi ndogo nowana wizara,asije kuharibu hata ya NECTA tukayasahau

Wewe ni GT, reasoning yako nimeikubali!
 
kote mi namuunga mkono , waliofanya vibaya huenda haikuwa kwa matakwa yao, JPM kawaweka weledi na naamini uadilifu ukitumika kuwaongoza tutafika tunakokuota.

Tugangeni yajayo TUFANYE KAZI!

Nape ana weledi upi wa kuongoza wizara zaidi ya itikadi za lumumba
 
Katika teuzi zote za Magufuli,
Hii ya wizara ya elimu ni bora zaidi,sababu hata wananchi walikua na kiu ya kumpata waziri kama huyu Mama

Hivi huyo ndalichako amefanya nini alipokuwa baraza la mitihani?mitihani kilasiku ilikuwa inavuja na kuwafanya watoto wa wenye noti kupata mtihani kabla ya kuingia ndani ya chumba cha mitihani
 
Watoto wa kikristo wakitoka shule anapumzika kidogo anaenda tuition yule wa kiislam anaenda madrasa kukariri kiarabu na mistari ya quaran mitihani ikija "oooh tumefelishwa" wakati mwingine kuitwa dini ile ni tusi kubwa sana.
 
JF isifungwe, naona mkuu hua anapitia hapa na kuchukua ushauri; Alipitiaga hapa issue ya wizara ya fedha na kesho yake akatia timu pale wizarani na Ndalichako nae pia, tulimpendekeza humu na hatimae rais ametusikia. Big up Magu!
 
Hongera ndalichako. Umepigiwa kampeni sana Jf apa ...nakunote kama mbunge wa jimbo la jf. Fanyia kazi matatizo ya elimu. Mbarawa safi kule ziwani isingekuweza, uku uchukuzi poa, ila sitakusahau kwa kupunguza MB zetu.
 
Walimu wamelipwa stahili zao nyingi,wafanye kazi. Niko Babati,wazazi wameamua kushughulika na waalimu wazembe,watalala nao mbele,kipimo matokeo ya mitihani ya taifa na za ujirani.Wengi wao wanashughulika na biashara zao muda wa serikali(kazi). Kwa huyu mama kitaeleweka,hapa kazi tu.
 
Fuatilia vizuri wakati wa Ndalichako mtihani haukuvuja labda kama wewe ni miongozi wa watumishi wa Necta mliokuwa mnavujisha kwa siri.
 
Ila ccm watu wameisha ..ivi mwezi mzima rais anpekua ...watu hakuna!! Kwa sasa itakuwa nusu ya serikali haitokani na chama. Katiba mpya inatekekezwa kiaina. Safi
 
Back
Top Bottom