Rais Magufuli, akiharibu kwa Lissu na Zanzibar basi Serikali yake itapata tabu sana

Rais Magufuli, akiharibu kwa Lissu na Zanzibar basi Serikali yake itapata tabu sana

Missile of the Nation

JF-Expert Member
Joined
May 24, 2018
Posts
17,047
Reaction score
63,206
Kuna hofu kubwa huko Lumumba kuhusu upepo wa Lissu. Hawakuutegemea, walijua Lissu ataufyata kama walivyoufyata wapinzani wengine kutokana na kashkash waliyowatia ndani ya miaka hii mitano, lakini wamekuta ndiyo kwanza Lissu hapepesi macho, ndiyo kwanza anakamua tu bila wasiwasi wowote.

Imefikia hatua wanatamani wamtoe uwanjani ili wafunge magoli bila timu pinzani. Ila sasa tatizo ni moja. Wakimtoa Lissu kwenye kinyang'anyiro kwa staili waliyotumia kwenye uchaguzi wa Serikali za mitaa, dunia nzima inaona!. Lissu ametengeneza marafiki wengi duniani, tena wale ambao ni wa muhimu kwetu kama Taifa. Nchi za umoja wa Ulaya zinafuatilia kwa makini kila hatua katika uchaguzi huu. Iwapo zitafanyika njama za kumuengua Lissu kimagumashi basi Rais Magufuli kama atakuwa yeye ndiye rais kuanzia mwaka 2021 ajiandae kuendesha serikali yenye hali ngumu sana ya kiuchumi kwa sababu wahisani wataondoa mikopo na misaada yao na huenda wakaenda mbali hadi kuwawekea vikwazo baadhi ya viongozi wasisafiri kwenda kwenye nchi zao!

Lakini pia italeta jambo moja ndani ya nchi, wananchi wataichukia na kuipuuza serikali itakayoingia madarakani kwa kucheza faulo kwenye uchaguzi. Zitatumika nguvu nyingi kuipamba serikali hiyo lakini wananchi wataipuuza na huyo mtawala atachukiwa sana na wananchi hata baada ya kumaliza miaka yake mitano!

Ifahamike Lissu anapendwa ndani na nje ya nchi, kwanza ni kielelezo cha maajabu ya kusurvive risasi nyingi, hiyo inampa sympathy kwa wananchi na dunia. Na yeyote atakayejaribu kumdhuru kwa kumchezea hata rafu za kisiasa anaweza kuamsha ghadhabu kali za hawa marafiki wa Lissu!

Lakini pia, Serikali ya awamu hii inajinasibu na kumtegemea Mungu, na imekuwa ikilitumia Jina la Mungu kisiasa na kipropaganda, Hata hivyo Lissu anawanyang'anya karata hii kwa sababu Kusurvive kwake kunanasibishwa na Uweza wa Mungu. Kwa Lissu yeye ni Ushahidi wa Utendaji wa Mungu na hata akisimama jukwaani akataja Muujiza wa Mungu juu ya kusurvive kwake basi watu wa dini wanamsikiliza yeye zaidi kuliko wale wanaopenda kutaja jina la Mungu kisiasa tu!. Yaani Lissu akimtaja Mungu inaclick kwa wananchi zaidi kuliko hawa wanaopenda kulitumia jina la Mungu kisiasa!. Kwa hiyo kumuengua Lissu pia kutawachukiza wapenda Mungu nchini maana itatafsirika kama muendelezo wa shetani kutaka kumuangamiza Lissu!

Kwa upande wa Zanzibar pia hali ni hiyo, Iwapo Maalim Seif atafanyiwa dhulma tena, basi Umma wa Zanzibar utauchukia muungano zaidi na Utaidharau serikali ya Muungano na ya Zanzibar zitakazoundwa. Lakini pia Wahisani hawatatia ushirikiano mzuri kwa serikali ya Muungano ambayo ndiyo lazima iwezeshe figisu huko Zanzibar ili zifanikiwe!.

Lakini Maalim amepata heshima kubwa nchini na kimataifa kutokana na uvumilivu wake, na kupenda kwake amani na kujaribu mara zote kutumia njia za kisiasa kutatua migogoro aliyonayo.
Ifahamike kuwa iwapo serikali itamessup na Zanzibar, ikapelekea wananchi wa Zanzibar kuingia mabarabarani, kutatokea umwagaji wa damu wa kutisha huko Zanzibar, na hii itapelekea wahusika kuingia katika mkono wa sheria huko ICC.

Kibaya zaidi, Misaada na Mikopo kwa serikali inaweza kusitishwa na hata kupelekea vikwazo.

Kwa hiyo, Rais Magufuli ana uchaguzi, ama akubali uchaguzi uendeshwe kimagumashi na yeye ashinde kwa asilimia atakazozitaka yeye, lakini serikali atakayoiunda imdodee kutokana na hali ngumu ya uchumi itakayofuata kutokana na kususwa kimataifa na pia kuacha Legacy ya kuchukiwa na kubezwa na watanzania baada ya kustaafu au akubali kuendesha uchaguzi huru na haki ili apate heshima na kuinusuru nchi isitokee umwagaji damu wa kutisha huko Zanzibar na pia isipate mdororo wa kutisha wa kiuchumi.

Safari hii hakuna choice, bila uchaguzi huru na wa haki kwa pande zote za muungano serikali itakayofuata itapata tabu sana!
 
Lissu mbele kwa mbele

Kivyovyote vile, Nchi hii inabidi ipigwe vikwazo sanaaaaa.

Ili hawa wanaojiita Masikin na wanyonge akili iwakae vzurii maana wamesahau yalotokea wakati wa JN.

Ulaya na Marekan, wakifanikiwa kuwagombanisha CCM wenyewe kwa wenyewe yaan kamata Mali za JK, kamata mali za Mwinyi, kamata kamata kamataa...piga vikwazo kwanzia wao wenyewe na watoto waooo... .. NA HILI NDIO TUNAOMBA WATUSAIDIE, KUISAMBARATISHA CCM, NI LAZIMA UWAGOMBANISHE WALE WAKUBWA WAKUBWA ....haiwezekan Mwinyi na JK wakae kimyaa kwa haya yanayoendelea alafu tuwaone ni wema kwetu..BIG NO.

Hawa CCM asubuhi kweupeeee na uzuri Jamaa saizi hana Rafiki wa Kufa na kuzikana maana yale mavyama ya enzi za 1950 asilimia kubwa yameondoshwaaaa madarakani.

Tunaenda na Lissu... Tunaenda na Marafiki zetu wa Ulaya na Marekani .
 
Tunataka nchi inayojali Haki na utu wa mtu.

Hawa CCM wanajifanya binadamu wote ni sawa bila kujali rangi, chama n.k...

Lakini tunashudia mambo ya ajabu ajabu kuwahi kutokea.
 
Tunataka nchi inayoheshimu na isiyoingilia uhuru wa vyombo vya habari.

Kwan ulisikia wapi, Eti Huwezi leta maendeleo kama upinzan unanguv?? Et km unakosolewa huwezi leta maendeleo..

Ulisikia wapi?

Leta maendeleo yako, bila kuingia uhuru, bila kuumiza, bila kutesa.

Dunia imeshahamaaa Ujamaa , HAIWEZEKANI NA HAITATOKEA JIWE KUIRUDISHA NCHI HII KTK MFUMO WA CHAMA KIMOJA. HAIWEZEKANI NA HAITATOKEA.
 
Aii.
Nimeishia eti sympathy.

Yaani nyie upinzani ni kitu kinachowapa proof ya hundred percent kwamba mgombea wenu atapita.

Ni kwamba CCM imekosa kabisa watu.
 
Lissu mbele kwa mbele


Kivyovyote vile, Nchi hii inabidi ipigwe vikwazo sanaaaaa.

Ili hawa wanaojiita Masikin na wanyonge akili iwakae vzurii maana wamesahau yalotokea wakati wa JN.

Ulaya na Marekan, wakifanikiwa kuwagombanisha CCM wenyewe kwa wenyewe yaan kamata Mali za JK, kamata mali za Mwinyi, kamata kamata kamataa...piga vikwazo kwanzia wao wenyewe na watoto waooo... .. NA HILI NDIO TUNAOMBA WATUSAIDIE, KUISAMBARATISHA CCM, NI LAZIMA UWAGOMBANISHE WALE WAKUBWA WAKUBWA ....haiwezekan Mwinyi na JK wakae kimyaa kwa haya yanayoendelea alafu tuwaone ni wema kwetu..BIG NO.


Hawa CCM asubuhi kweupeeee na uzuri Jamaa saizi hana Rafiki wa Kufa na kuzikana maana yale mavyama ya enzi za 1950 asilimia kubwa yameondoshwaaaa madarakani.


Tunaenda na Lissu... Tunaenda na Marafiki zetu wa Ulaya na Marekani .

Aisee hizi ndoto zingine ni balaa!
 
Naona umempa options kama 4 hivi na zote conclusion yake ni moja tuu..asishinde uchaguzi na kuunda serikali ijayo...KAZI kwake SASA.
 
Hakuna kitu kizuri kama kukaa na wapinzani na kuona mambo yapi yarekebishwe kuondoa migogoro kwa siku zijazo.

Ni wazi kwa sasa ccm inahitaji kukaa na wapinzani na kiukweli ccm haiwezi kulikwepa hilo. Na kwa sasa wasiamini kwamba wanaweza kutawala peke yao
 
Mi nimekuelewa saana sijui wengine kama wamekuelewa kama mimi?
 
Uchambuzi mzuri wa hali ya kisiasa nchini Tanzania na hatma ya viongozi wa CCM Mpya, bora wakubali matokeo na kujipa heshima ndani na nje kwa CCM kuwa chama cha upinzani kuliko kuharibu zaidi ya hapa tulipofikia.

Wasiwe na hofu, serikali Mpya kutoka upande mbadala inayoingia madarakani 2020 itakuwa tofauti na ya CCM Mpya kwa kufuata utawala wa sheria na haki.
Hata hivyo Lissu anawanyang'anya karata zote CCM huku chama kongwe kikiwa muflisi kwa kukosa karata za hoja na propaganda zisizo na ushawishi
basi Umma wa Zanzibar utauchukia muungano zaidi na Utaidharau serikali ya Muungano na ya Zanzibar
 
Namba ya votes.. ndiwo zitawamua.. ya sherehe zenu za kuzurura na kukaribisha watu.. kuwatizama mukiropoka.. hazina tija..

Magufuli 2020 💯
 
Pia yawezekana Tanzania kuwa ya kwanza kwa ukanda huu kutoa kiongozi aliyepata kuwa madarakani kunyea ndoo huko The Hague
Hivi kwa nini SMS zako zote zinaonyesha kuiombea nchi na viongozi wake mabaya, utafikiri machafuko yakitokea wewe utabaki salama?
 
Back
Top Bottom