Rais Magufuli akutana na Viongozi wa vyama vya Siasa nchini, Maalim Seif(ACT-Wazalendo), Prof. Lipumba (CUF) na James Mbatia (NCCR-Mageuzi)

Huyu Magufuli naona anajipa kazi bila kutaka kwa kumuogopa Membe. Naona ameamua ni heri ajiweke karibu kwa viongozi wa vyama ambavyo ni "likely" Membe kujiunga navyo kwa ajili ya kutimiza "ndoto zake". Bila shaka anajaribu kuwalaghai wasimpe nafasi ili akose pa kutimizia ndoto zake.
 
Hii ndo aina ya siasa inayotakiwa kufanywa na viongozi wetu wa kisiasa na kiserikali kuliko kila upande kuwa wababe kwa upande mwingine.

Haya ni maandalizi mazuri ya uchaguzi mkuu
Kweli unayo sema, lakini kwa upande wangu naona siasa za unafik zinazofanywa na chama tawala,..

Angalia nini kinatokea Pemba, Wabunge wa upinzani wanarubuniwa,..

Angalia nini kinatokea Moshi,mikutano ya Chadema inachafuliwa..

CCM hawana nia safi na siasa za Ukweli na uwazi, wanataka kutawala milele, CCM ni wazuri kwa kilaghai na kuchafua wengine

We got a long way to go, I feel sorry for my people and country, Go bless TZ
 
Kusema ukweli vurugu zilizofanyika kwenye kikao cha mwenyekiti wenu ni vurugu zilizokuwa zimeandaliwa na Mbowe mwenyewe akiwa na mia za kuunyesha umma kuwa Tanzania hakuna siasa safi,bahati mbaya ukweli umebainika mapema chabuso,

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kwahali ilivyo sasa, Membe, Lowasa, Makamba na hata Kinana wangeenda Upinzani hakuna ambacho wangeweza fanikiwa. "Zana za ushindi alizonazo", Magufuli haogopi uchaguzi, anachotafuta ni kuonekana ushiriki kivuli wa upinzani.
 
Kwahali ilivyo sasa, Membe, Lowasa, Makamba na hata Kinana wangeenda Upinzani hakuna ambacho wangeweza fanikiwa. "Zana za ushindi alizonazo", Magufuli haogopi uchaguzi, anachotafuta ni kuonekana ushiriki kivuli wa upinzani.
Sidhani Kinana na Lowasa wana nia ya uraisi. Msiwachanganye kundini

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kwa akili za dikteta uchwara..unaweza kuwa sahihi

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Viongozi wa upinzani walikuwa wawili tu,jingine lilikuwa pandikizi.
 
Nimepitia twitter kuangalia wanazi wa CUF/ACT wamepost kitu gani kuhusu milutano hii ya leo, nimekuta akina Jussa hawajaweka chochote zaidi ya kupost wateuliwa wa kugombea uenyekiti wa ACT.

Pamoja na kwamba Maalim kateuliwa kuwa mmoja wa wagombea nafasi ya Mwenyekiti wa Chama lakini Jussa hajasema hilo zaidi ya kupost picha za akina Maganja na Shilungushella.

Naamini ana maumivu rohoni mwake.
 
Hahahaha
Sent using Jamii Forums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…