Rais Magufuli akutana na Viongozi wa vyama vya Siasa nchini, Maalim Seif(ACT-Wazalendo), Prof. Lipumba (CUF) na James Mbatia (NCCR-Mageuzi)

Rais Magufuli akutana na Viongozi wa vyama vya Siasa nchini, Maalim Seif(ACT-Wazalendo), Prof. Lipumba (CUF) na James Mbatia (NCCR-Mageuzi)

digba sowey

JF-Expert Member
Joined
Mar 1, 2017
Posts
8,926
Reaction score
17,880
Rais wa Tanzania John Pombe Magufuli akiagana na Mwanasiasa Mkongwe ambaye ni Mwanachama wa Chama cha ACT Wazalendo Maalim Seif Sharif Hamad mara baada ya kumaliza mazungumzo yao Ikulu Jijini Dar es Salaam.

My take,hizi ndo siasa safi.

=====

seif3.jpg

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiwa katika mazungumzo ya faragha na Mwanasiasa Mkongwe ambaye ni Mwanachama wa Chama cha ACT Wazalendo Maalim Seif Sharif Hamad, Ikulu Jijini Dar es Salaam.

FB_IMG_1583230410700.jpeg

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiagana Mwanasiasa Mkongwe ambaye ni Mwanachama wa Chama cha ACT Wazalendo Maalim Seif Sharif Hamad kwa kutokugusana mikono, Ikulu Jijini Dar es Salaam. Salamu hiyo ya kutokugusana mikono ni kutekeleza ushauri ya Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Ummy Mwalimu wenye lengo kujihadhari dhidi ya virusi vya ugonjwa wa Corona.

seif2.jpg

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akifurahia jambo na Mwanasiasa Mkongwe ambaye ni Mwanachama wa Chama cha ACT Wazalendo Maalim Seif Sharif Hamad mara baada ya mazungumzo yao Ikulu jijini Dar es Salaam.

1583233680079.png

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiwa katika mazungumzo ya faragha na Mwanasiasa Mkongwe ambaye ni Mwenyekiti wa Chama cha Wananchi CUF Profesa Ibrahim Lipumba, Ikulu Jijini Dar es Salaam.

1583233781339.png

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiwa katika Picha na Mwenyekiti wa Chama cha Wananchi CUF Profesa Ibrahim Lipumba mara baada ya kumaliza mazungumzo yao Ikulu Jijini Dar es Salaam.
1583233836110.png

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiwa katika mazungumzo na Mwenyekiti wa Chama cha NCCR Mageuzi James Mbatia Ikulu jijini Dar es Salaam.

Mbatia.jpg

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza jambo na Mwenyekiti wa Chama cha NCCR Mageuzi James Mbatia Ikulu jijini Dar es Salaam.
 
Zitto karibu huku ushuhudie wanasiasa nguli wanaojua siasa. Wenzako matatizo ya nchi wanakaa chini na kuzungumza, wewe unaenda ugenini kuzungumza halafu unajiona mwamba wa siasa. Rudi darasani ukajifunze uzalendo.
 
Back
Top Bottom