Rais Magufuli alikataa kuongeza mikoa kwa kuwa inaongeza gharama, alisema la muhimu wananchi wapatiwe huduma

Rais Magufuli alikataa kuongeza mikoa kwa kuwa inaongeza gharama, alisema la muhimu wananchi wapatiwe huduma

Johnny Sack

JF-Expert Member
Joined
Jan 21, 2017
Posts
8,984
Reaction score
19,288
Magufuli alipoombwa kuugawa mkoa wa Tabora ambao unastahili zaidi kugawanywa kuliko huko Chato alijibu na kusema hawezi kugawa mikoa kwa sababu ni gharama, Pia alishaombwa kuugawa mkoa wa Morogoro na akatoa majibu hayo hayo.

Leo Hoi tunasikia mkoa wa Chato umegawanywa kilazima licha ya wananchi kutohitaji na madiwani wao kukataa, Samia nitamuona rais wa ajabu akitekeleza hili ombi na kuacha mikoa yenye uhitaji zaidi.

Mbona wananchi wamekubali mkoa uwepo, wewe hizo taarifa za wananchi kuukataa umezitoa wapi?

Mimi siungi mkono kwa sababu ule mkoa wa Geita bado ulikua mchanga. Morogoro ilikua haki kabisa kuugawa.
 
Magufuli alipoombwa kuugawa mkoa wa Tabora ambao unastahili zaidi kugawanywa kuliko huko Chato alijibu na kusema hawezi kugawa mikoa kwa sababu ni gharama, Pia alishaombwa kuugawa mkoa wa Morogoro na akatoa majibu hayo hayo...
Madiwani waliokataa ni wa Busanda siyo wa Geita nzima wengine wamekubali mkoa ugawanywe hivyo wengi wape!
 
Madiwani waliokataa ni wa Busanda siyo wa Geita nzima wengine wamekubali mkoa ugawanywe hivyo wengi wape!
Pointi kubwa hapa ni kukataa kugawa mikoa yenye uhutaji zaidi kwa kigezo cha gharama kisha kugawa mkoa wake
 
Pointi kubwa hapa ni kukataa kugawa mikoa yenye uhutaji zaidi kwa kigezo cha gharama kisha kugawa mkoa wake
Yeye amegawa mkoa wake?? Kwani bado yupo? Mbona unamsingizia? Siku ya mazisho yake wanachato walimuomba Mama Samia na yeye ndiyo akawaahidi kuwa kama itakidhi masharti basi Chato itakuwa mkoa na sasa wako kwenye process. Usimsingizie Hayati Magufuli katika hili.
 
[emoji23][emoji23] wszee mnajua sana kujivua akili, yaani hujui kuwa hui mpango ulianzishwa jiwe akiwa hai?
Wewe nafikiri unalako jambo. Kama alianzisha umejuaje mbona hatukuona madiwani wanaijadiri issue hii?
 
😂😂😂😂😂😂😂hiiiiiiiiiiiii
 
Chato region Imepita hiyo hakuna kipingamizi itasaidia uwanja wa ndege wa chato uwe proactive
 
Yeye amegawa mkoa wake?? Kwani bado yupo? Mbona unamsingizia? Siku ya mazisho yake wanachato walimuomba Mama Samia na yeye ndiyo akawaahidi kuwa kama itakidhi masharti basi Chato itakuwa mkoa na sasa wako kwenye process. Usimsingizie Hayati Magufuli katika hili.
Amemsingiziaje kitu alichosema mwenyewe? Cha kumlaumu Mwendazake ni kuwa alikemea wazo la Nzega kuwa mkoa lakini ilipofika Chato akakaa kimya.

Hii dhana ya mikoa mipya imeghubikwa ubinafsi na ukabila. Ili kuondoa tatizo basi wilaya zote ziwe mikoa ili wigo la maRC liongezeke.

Mimi ningeshauri badala ya kuongeza mikoa ipunguzwe. Mkoa wa Dar es Salaam uondolewe na uunganishwe na mkoa wa Pwani kama ilivyokuwa zamani. Dar es Salaam ubaki kuwa jiji. Tuwaige marekani ambako makao makuu ya majimbo sio lazima iwe katika miji mikubwa. Makao makuu ya jimbo la New York ni Albany na sio jiji la New York, Texas ni Austin na sio Houston n.k. Lindi iunganishwe tena na Mtwara, Songwe irudi Mbeya, Manyara Arusha, Katariina irudishwe ilikotoka, Geita vile vile. Pesa zitakazookolewa ziwekezwe kwenye miundo mbinu. Na tuondokane na dhana ya vitu kama hospitali ya mkoa, tupaki na referral hospitals ambazo zitajengwa kutokana na wingi wa watu wanaohudimiwa na sio status ya mkoa.

Amandla...
 
Magufuli alipoombwa kuugawa mkoa wa Tabora ambao unastahili zaidi kugawanywa kuliko huko Chato alijibu na kusema hawezi kugawa mikoa kwa sababu ni gharama, Pia alishaombwa kuugawa mkoa wa Morogoro na akatoa majibu hayo hayo.

Leo Hoi tunasikia mkoa wa Chato umegawanywa kilazima licha ya wananchi kutohitaji na madiwani wao kukataa, Samia nitamuona rais wa ajabu akitekeleza hili ombi na kuacha mikoa yenye uhitaji zaidi.

hilo ni pendekezo la hayati usimsingizie maadam wetu.ona sukumagangs wanavyoshupalia hilo
 
Naunga mkono kabisa kuundwa kwa mkoa wa Chato kwa sababu kuu moja, ... nayo ni kuisogeza serikali karibu zaidi na ukanda huu uliopakana na chanzo kikuu cha migogoro ya nchi za maziwa makuu (TUTSI/HUTU conflict zone)!
👊 😎✌️💥☠️☠️☠️💀
 
Yeye amegawa mkoa wake?? Kwani bado yupo? Mbona unamsingizia? Siku ya mazisho yake wanachato walimuomba Mama Samia na yeye ndiyo akawaahidi kuwa kama itakidhi masharti basi Chato itakuwa mkoa na sasa wako kwenye process. Usimsingizie Hayati Magufuli katika hili.
Sio kweli...

Mama Samia huyu hapa kuanzia dakika ya 1:55

Nigusie kidogo, mambo ambayo ameyasema mzee wetu hapa, Mzee Bigambo... kwanza la Chato kuwa mkoa. Nataka niseme kwamba, nina taarifa mchakato umeanza. Niwaagize kumaliza mchakato huo katika ngazi zenu huku....
Hapo nilipo-bold ni ushahidi tosha kwamba mchakato wa Chato kuwa mkoa ulianza enzi za Magu!!

Na huo ni ushahidi tosha kwamba ambacho alikataza Magu ni kuanzisha mikoa mingine lakini kwa Chato kuwa mkoa, it's okay!!!
 
Back
Top Bottom