Rais Magufuli alishasema hatabadili Katiba ili kusalia madarakani. Kwanini Kabwe, Membe, Tundu Lissu mnamenea mnamnenea uongo ?

Ni Hayati Benjamin William Mkapa ndiye pekee ambaye angalimzuia huyu mtu kutokubadilisha katiba ili apate kuendelea kubaki madarakani. Lazima yeye na wapambe wake watakija na kisingizio cha kumpa nafasi ya kumalizia SGR, bwana la kuzalisha umeme la Mwl. Nyerere na porojo nyingine kama hizo.

Mlisha sikia wenyewe kauli ya Mzee Mwinyi ya kutaka kubadilisha vifungu vya katiba, huku jamaa naye akizuga kuwa hataki, kumbe hiyo ni sitaki nataka huku akusubilia kwa hamu kupata theluthi mbili ya viti vya uwakilishi bungeni. Mzee Jakaya naye ameona ni heri aendelee kuwa upande wake, kwa kujali kesho ya kisiasa ya wana familia wake.

Maandalizi yalianzia ktk uchafuzi wa mwaka jana wa serikali za mitaa, vitongoji na vijiji, ambapo kwa hila na dhuluma kubwa waliolazimisha ushindi wao wa 99% bila hata ya aibu yoyote ile. Matayarisho ya uchafuzi wa mwaka huu yana baraka zote za NEC na ZEC ambao wamepewa jukumu la kucheza rafu za mapingamizi na hatimaye kuja kuwatangaza wakola hawa kuwa wameshinda kwa kishindo.

Kigingi kikubwa kwao ni Tundu Lissu na Maalim Seif. Ndiyo maana kila wanapotoa kauli za njama zao, wao hukereka sana kwa sababu wameazimia kutumia njia ya aina yoyote ile kukamilisha ufedhuli wao. Wapigakura bado wanasimama upande wa viongozi hawa wawili mashujaa na wazalendo wa kweli kutoka Tanganyika na Zanzibar.
 
Sheria gani inamzuia kujiongezea muda?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…