Rais Magufuli alivyovuruga Uhusiano na Wadau wa Maendeleo

Rais Magufuli alivyovuruga Uhusiano na Wadau wa Maendeleo

Akili mgando kabisa hii.Kitu hujui n kuwa hakuna free lunch katika dunia ya leo na hiyo misaada iliyomingi Ina masharti magumu lukuki

Kwa mtazamo uliowazi n kuwa misaada hiyo n maney trap au mitego ya wafadhili kwa nchi maskini kufanyiwa ukoloni mambo leo

Magufuli n Rais pekee aliyethubutu kuweka maslahi ya nchi mbele kwakuhakikisha misaana inakuwa ni ileyenye mashart nafuu na Kuna kuwa na maslah kwq nchi

Usifurahi hata kidogo nchi kuwa top ten ya nchi zinazopata misaada sana Bali furahi pale nchi inapoweza kupunguza utegemezi


Piga kazi changia pato la nchi hamasisha na Alie karibu na wewe afanye kazi tulipe Kodi.Wengi was waliokata misaada n wale ambao masharti yao tumeyakataa na magumu kwa maslahi mapana ya nchi.

Sikuzote watoa misaada wanapenda nchi yetu iendelee kuwa tegemezi ili waendeleee kufaidi kwa mlango wa nyuma.Ukilitazama hili juu juu utamlaumu Magufuli lakini ukijaribu kutumia sehemu ya akili yako vzr kuelewa namna misaada na mikopo inavyotolewa na siasa zake nyuma ya kapeti utakubaliana na mm kuwa n Bora kumuunga Mkono Magufuli kwa jitihada anazofanya.

Rais akimaliza muda wake tutamkumbuka sana ingawa kwasasa kwasababu ya mihemko ya kisiasa baadhi wanamuona Kama ameshindwa
Bwana Ngapulila unachekesha sana, mtu aliyeangalia aya yako ya kwanza angedhani ulikuwaa thinker wa ukweli. Imekujacha f ua na kusifia ujinga baadaye.

Rais anajali maslahi ya nchi![emoji16],inachekesha! Anayaji kw a lipi. Kama ni kujali kila raisi alikuwa kabla ya Magufuli pia alijali maslahi ya nchi. Nyerere alijali,.mpaka mimi nikasoma nikaelimika, Mwinyi pia aliyajali, Mkapa aliyajali, Kikwete aliyajali, na Magufuli anajali. Kila rais ametekeleza wajibu wake kwa namna yake. Huwezi kubeza kazi za watu wengine na kusifia mtu mmoja ati ndiye unaona anajali kuliko wengine. Hii sasa ni mawazo ya siasa za maji taka.

Weka siasa mbali, fikiri kama thinker wa ukweli, je Magufuli hajakopa kwa hao mabeberu unaowasema? Unaamini miradi ya inayotekelezwa leo mnatumia fedha zenu kama ambavyo mnaimbiwa kila kukicha?

Ama kweli usilolijua ni kama usiku wa giza! Hivi Magufuli amebadilisha mfumo wa uchumi wenu wa Tanzania, na hivyo mtalipa kodi mfanye mambo yenu bila kukopa? Acheni ndoto za mchana, mnaota huku mnatembea, tutawona vichaa!
 
Tumeanza kupata misaada toka awamu ya mkapa yupo madarakani imetufikisha wapi? Hao wadau wa maendeleo wanaipenda tz kuliko magufuli? Au sababu kahoji makinikia??

Brother hakuna free lunch in capitalist economy.. nikikupa ina maana nataka. Wanatupa msaada wanata nini,? Is it the fair business? Hako ka wanafunzi wenye mimba ni kichaka tu, toka mwaka 90 tanzania hatukua na sera ya kusomesha wajawazito.

Wasomi wa nchi hiz masikini wanakalili vitabu vilivyoandikwa na wazingu, lakini reasing ni 0%. Yaani wazungu wakusanye kodi kwao waje watoe msaada bure!!! Inakuingia akilini?

Eti demokrasia, hivi kuna nchi inaweza kutekeleza demokrasia kama tunavyosoma kwwnye vitabu? Demokrasia ni lazima iendane na utamaduni wa watu husika. Hakuna demokrasia kwenye umasikini. Hakuna..
Tujifunze...
 
Wakikupa shilingi 100 hao wadau wa maendeleo unaowasema kisha ukalipa mishahara watu wao wanaokuja kwa majina ya expert 60% ya hiyo 100 kisha wakafanya manunuzi kwa hiyo hiyo 100 tena vifaa toka zilikotoka 30& na kisha ukawapa misamaha ya kodi kwa bidhaa zao zinazoingia hapa ndani utabaki na nini? Ni bora kubaki hauna ukajua hauna.

Sent using Jamii Forums mobile app
Tatizo Shule. Ndio maana unaonekana kutokuelewa mambo ya kiuchumi.
 
Utasubiri sana kuona anashindwa lakini hawezi shindwa. Unajua hii miradi imetoa ajira kwa watu kiasi gani?
Mimi kinachonikera ni kutokana na kauli chafu na kali za mkuu ugonjwa huu sasa umeenea kama hapo juu hana hoja lakini either anafichama kwenye kukosa uzalendo, au very very vague statements zisizo kuwa verifiable kama ajira , ni upumbavu wa kiwango cha juu
Usipojisaidia hausaiidiiki khaa, hata Ulaya na China kuna masikini sana. Muhimu ni Taifa kwa ujumla kusonga mbele. Kwani mataifa yanayotoa misaada hayajui kuwa kuna raia wao wanaishi katika mazingira magumu? lakini bado wanatoa fedha zao kusaidia nchi za nje. FIKIRIA KIDOGO au na wewe ni wale wa bora kuwa MBWA wa ULAYA?
angalia lugha ya watu maskini wa kutupwa
 
Jamaa yupo Teyali atakumwaga Damu ili nafasi yake ibaki
 
Wakikupa shilingi 100 hao wadau wa maendeleo unaowasema kisha ukalipa mishahara watu wao wanaokuja kwa majina ya expert 60% ya hiyo 100 kisha wakafanya manunuzi kwa hiyo hiyo 100 tena vifaa toka zilikotoka 30& na kisha ukawapa misamaha ya kodi kwa bidhaa zao zinazoingia hapa ndani utabaki na nini? Ni bora kubaki hauna ukajua hauna.

Sent using Jamii Forums mobile app

Kama mtu hujui jinsi development finance inavyofanyika ni bora ukauliza ili ueleweshwe. Ulichokiandika hapa ni zaidi ya upuuzi; haingii akilini hata kwa mtoto alie chekechea kuwa 60% ya donor funding itumike kulipa mishahara foreign expert. This is idiotic.
 
Ha
Tuna miradi mikubwa ambayo tunajenga kwa pesa zetu wenyewe, how come useme The GVT is broke.??

Utasukumwa ndani mkuu..

SGR, SG, Barabara 8 Morogoro road, Ubungo InterChange, Ununuzi wa ndege, Kuhamia Dodoma e.t.c.., miradi yote hii inatekelezwa kwa 'PESA ZETU WENYEWE' ,why saying serikali imefilisika.???

Sisi twatembea vifua mbele bhana ,hatutishwi na mabeberu..

Sent using Jamii Forums mobile app
Unayosema ni kweli Mkuu, lakini Je Watanzania wa kawaida hali zao kimaisha zikoje?..

Tunawaona Waithiopia wanakamatwa kama Wahamiaji haramu kila siku hapa Tanzania.. Ethiopia ilijikita kwenye miradi mkubwa bila ya kujali raia wake kama hivi wanavyofanya Tanzania..

Nyerere alishawahi sema "Maendeleo ya vitu sio Maendeleo ya watu" "
 
Heri maumivu ya kujitegemea kuliko furaha ya misaada yenye masharti
 
Jk alimjua huyu cameraman, mkapa Na lubuva awakumjua upande wa pili wanajutia sana maamuzi yao.Lawama zote juu yao.Uwezo wa kukariri kilometers za barabara Na vifaranga vya Samaki si kigezo cha utendaji wa MTU.Factors zingine ni lzm zizingatiwe.
 
Mkuu yaani katika watu ambao wamekaa nje kwa mda mrefu mpaka wana sahau kiswahili kama ulivyodai, basi wewe ni mtanzania wa kwanza ambaye amewahi kuandika upuuzi usio semeka ambao sijawahi kuusikia. Yaani kukaa kote huko Amerika umeshindwa kupata exposure kiasi kwamba unaandika madudu humu kama mtu ambaye hata Msumbiji hajafika?
Inasikitisha sana na nimekuwa very very disappointed. Yaani kuishi kote nje bado unatumia neno msaada. Yaani unaona ufahari kuwa na uhusiano mzuri na wazungu kwa ajili ya misaada?
Haya naomba nitolee list ya maendeleo ambayo hiyo misaada imefanya kwa watanzania. Una maanisha msaada ya wazungu ambao kwao ni jobless kuja kwetu kwa misingi ya kuwapatia kazi. Au una maanisha misaada ya NGOs ambao wanakuja Tanzania na Afrika kwa ujumla kuja kuishi maisha ya kifahari na kujiingiza katika sexual Business. Kuchezesha porno filams na dada zetu na shangazi zetu?
Ningekushauri kwa niaba ya watu ambao wamepata elimu nje na kufanya kazi nje kwa mda mrefu, watu ambao wameyaelewa maisha na dhamira za wazungu, kufutilia mbali hoja yako. Inatudhalilisha sisi tulio pata exposure. Kwa mtu anaye wajua wazungu kwa jinsi walivyo kuwa the Killing machines nisinge tegemea niger kama wewe kuwasifu kiasi hicho na kuwaona wao ndiyo kila kitu. Yaani bila wao hakuna kitu kinawezekana.
Jiamini kijana usiwe na mchecheto wa kukata tamaa ya maisha na kuji positon wewe mwenyewe katika kundi la watu ambao wako inferior. Kuto jiamini kwako ndiyo kitu ambacho kinawapa wao nguvu na kujiona kuwa wao ni Superior. Nakuomba usiruhusu mambo kama hayo.
Sasa kama wewe ambaye umeishi na wazungu na kuyajua maisha yao unakuwa mwoga na kuwababaikia wazungu kiasi hicho sasa yule mtanzania ambaye hajawajua wazungu na mifumo yao ya kutaka kuwa na control over our lives atafanya nini?
Nitarudi tena!!!
Sent using Jamii Forums mobile app

Umeniaibisha sana rafiki yangu
 
Ukiwa mwekeli daima utabaki huru .Wapo wasomi wanaompotosha kiongozi wetu kuhushu uendeshwaji maswala ya uchumi.Wao hawana cha kupoteza maana wanapalilia vyeo vyao.Uendeshwaji wa uchumi wa nchi hauchanganywi na sera za siasa maana viashiria ( indicators) zitaonyesha kama uko kwenye right track or wrong track.
 
Unaambaa ambaa, badala ya kujibu maswali, ndiyo sifa ya Utanzania. Kumbuka kuna nchi ambazo hazikuwahi kutawaliwa kabisa na hao wazungu. Ziko dunia ya ngapi? Kisha ujue kwamba wazungu hao walitawala Tanzania kwa takribani miaka 70 tu, na tangu tulipojitawala tuna zaidi ya miaka 57. Nipe bado mifano miwili tu ya kitu ambacho tunajivunia baada ya miaka 57, tangu tulipoachana na kunyanyaswa na hao wazungu. Something made in Tanzania, something a prestige of the country. Kwa mfano, wajapani ni watengezaji wa mameli makubwa duniani, watengezaji wa magari bora, wataalam katika electronics,camera nzsuri Japani, pikipiki nzuri Japan, genereta nzuri Japan, n.k.

Kitu gani tunacho?
Sisi tunaweza tukajivunia labda utekaji watu tunaoona hawataki kuunga mkono juhudi na pia kuvunja rekodi ya dunia kwa kujenga "Viwanda" zaidi ya 3,000 ndani ya miaka mitatu tu na bila kusahau kununua ndege kwa "Cash". NB: Maendeleo hayana chama!!
 
Mwitikio wa andiko langu wiki lililopita katika mtandao huu wa JF ulinipa hamasa kuendelea kuandika zaidi jinsi Rais Magufuli anavyoendelea kulipotezea mwelekeo taifa. Wiki hii naona nigusie kwa undani jinsi Magufuli anavyoharibu uhusiano mzuri sana uliokuwepo kati ya Tanzania na wadau mbalimbali wa maendeleo. Awali ya yote naomba mnisamehe, kiswahili changu si kizuri kama ambavyoningependa kiwe, ila anendela kujifunza;

Sio siri kwamba Tanzania ilijulikana kama kipenzi cha wadau wa maendeleo(darling of development partners); Ukiangalia twakimu za misaada iliyokuwa inaletwa na wahisani katika nchi za Africa, Tanzania ilikua haikosi katika 10 bora katika nchi za Africa. Umoja wa Ulaya, Benki ya Dunia, Marekani, China, Ufaransa, Uingereza, Ujerumani nchi zote hizi zilikua zinawekeza kwa nguvu kubwa katika maendeleo ya watanzania.

Magufuli alipoingia madarakani, mambo yakaanza kubadilika, mwanzoni walikua wanamvumilia sababu alionekana kama ni kiongozi mpya mwenye ‘zeal’ ya kupigana na rushwa ila siku zilivyokuwa zinazidi wakaona hali inazidi kuwa mbaya hususani katika utawala wa sheria, demokrasia na haki za binadamu.

Magufuli alipotangaza kuzuia wasichana wa kike kutoendelea na masomo yao kisa ya mimba alipiga msumari mkali katika mahusiano na hawa watu. Na hii ndio sababu husikii hawa development partners hawainvest kwenye sekta ya elimu, maana wakitoa msaada au wakiwakopa Tanzania, watanekana na wao wapo complicit kwenye hilo katazo. Athari zake tunaziona kwa jinsi hali ya elimu inavyozidi kuporomoka siku baada ya siku, madarasa hayatoshi, walimu hawashugulikiwi madai yao vizuri maana mzigo wa kuiinua hii sekta nyeti kwa Taifa limebaki tu kwa serikali.

Benki ya dunia

Katika wahisani ambao sikutegemea (hata Magufuli mwenyewe hakutegemea) wangeweza kuigomea serikali ni Benki ya dunia maana ndio ilikua taasisi iliyobaki ambayo ilikua inaipa serikali kiburi pamoja na kuwepo kwa ukiukwaji wa haki za kiraia.

Kwa msiofahamu wahisani wanachangia asilimia 40% ya bajeti ya Tanzania na Benki ya dunia inachakia takribani asilimia 10%(kubwa kuliko mdau yeyote) na hivyo kuifanya kuwa Tanzania’s biggest partner in development.

Benki ya dunia ilianza kuichoka serikali walipofanya marekebisho kwenye sheria ya twakimu ya mwaka 2018 ambayo inazuia taasisi yeyote kuto-desseminate statistics bila kupata verification kutoka NBS. Kazi kubwa za Benki ya Dunia ikiwemo repoti na miradi zinategema takwimu halisi, hii sheria mpya iliweka vikwazo vilivyoifanya WB kutofanya kazi zao freely and professionally

Tulisikia mwaka jana mwezi wa 11 jinsi benki ya dunia livyositisha mkopo wa $300million wa elimu (takribani billion 700tsh) kwa sababu ya sera ya serikali ya kutoruhusu hawa watoto kurudi shuleni. Magufuli anathamini na anajua mchango wa benki ya dunia katika maendeleo ya nchi na ndio maana alikubali kukutana na WB Regional Vice President wanegotiate kuhusu huu mkopo. Katika maongezi yao (japo hayajawekwa wazi) walikubaliana kuandaa program ambayo italipiwa na serikali itakayowawezesha watoto wa kike wenye mimba kupata elimu, kama mnakumbuka wakati ule nchi ilibujikwa katika sakata la ushoga lililoanzishwa na makonda, waliliongelea na Magufuli alimuhaidi kuwa amna mtu atakae kamatwa kwa ushoga na atamkataza Mkuu wa Mkoa kuongelea kuhusu swala hilo tena, tatu, alikubali kuendelea kuwa na maongezi juu ya ile sheria ya takwimu.

Cha kushangaza, siku chache tu baada ya kukubaliana nao, Magufuli wakati wa uzinduzi wa Library ya UDSM, akawakashifu kwa kuwapongeza waChina kwa kuwaambia kuwa, “misaada yenu hayana masharti, sio kama mashirika mengine”. Huyo makamu wa Rais alisikitiswa na kauli hii maana ilionyesha kuwa serikali haikuwa na commitment katika makubaliano hayo.

Ni kwa sababu hiyo mpaka leo hii mkopo haujatolewa na sidhani kama utaolewa. Sio hiyo tu, Benki ya Dunia imei-demote ofisi yake ya Tanzania. Benki ya Dunia inakuaga na Country Director- wa sasa ni ndugu Bella Bird lakini kuanzia June 2019, amabapo mda wake utaisha nchi itaanza kuwa na country manager.

Kuwa na country manager inamaanisha kuwa na portfolio ya nchi itapunguzwa. Miradi yote inayohusiana na P4R – Program for results, kwenye elimu, maji, umeme, yote inafutwa, maana huwezi kupata results without credible statistics.

Pamoja na balozi Mahiga na Prof Kabudi kwenda Brussels kuipigia magoti umoja wa ulaya bado wameendelea kusitisha msaada wao nchini.

Yamkini inabidi tutafute mbinu za kujitegemea lakini tupende tusipende bado tunawahitaji hawa wadau wa maendeleo. Hata Europe yenyewe iliendelea kwa kusaidiwa na Marekani through the Marshall Plan policy iliplay a big part in the reconstruction of Europe baada ya vita ya pili ya dunia.

Serikali ifanye nini

Kwanza wathibiti matamko ya Rais; Kuwaita mabeberu hadharani, kutangaza kwamba nchi ipo katika vita ya uchumi na kusema kwamba misaada yao inamasharti. Ushawahi kuona wapi jirani yako anakuja kukusaidia alafu unaanza kumtukana, unadhani ataendelea kukusaidia?? Sio lazima akubaliane nao ila awaheshimu, kiufuppi ajifunze lugha za kidiplomasia zaidi

Pili, na hii itakua ngumu kwake, aruhusu watoto wenye mimba waendelee na masomo yao, hii itabuild confidence kubwa sana kwa hawa wahisani. But we all know this is never going to happen maana Rais alishasema na ninanamnukuu, “katika utawala wangu watoto wenye mimba hawatarudi shuleni, siwezi somesha wazazi”. Kwa mtu mwenye ego kubwa kama Rais wetu, hawezi reverse such a statement, it will possibly be the biggest political miracle in our country’s history.

Tatu, Asisgn into law mswada wa vyama vya siasa. Hii itakua ushindi kwakwe in both the internal and external politics.. kwanini; 1. Itanesha kwamba kama Rais anaheshimu demokrasia ya vyama vingi, pili itabuild trust kwa wananchi kuwa rais kumbe anauwezo wa kutosign sheria mbaya hata iliyopitishwa na wabunge wa vyama vyake (hatausishwa na hii sheria kabisa), tatu, He will for once be on the positive side of the coverage of the international media. Tutaona makala mabali mbali za nje zitakavyomsifu jinsi kwa huo uwamuzi… But this is also never going to happen maana ukweli unajulika kuwa yeye ndio muasisi mkuu wa hiyo sheria.

Najua wengi mtasema kuwa “hatuitaji misaada yao” “serikali ina pesa” ila ukweli msioujua ni kuwa the government is sooooooooooo broke, na ndio maana unaona kuna msisitizo mkubwa hivi karibuni wa kulipa kodi na kufanya ulipaji kodi kuwa rahisi kwa watanzania.

Kama mnadhani tunaweza kuendelea bila ushirikiano na wadau wa maendeleo angalieni hali ya Zimbabwe wanaoenda nunua mkate na begi limejaa noti… Serikali ibadilishe mwelekeo, kabla mwelekeo haujatubadilisha… kuweni na siku njema
Sasa mijitu ya ivi ndo hatuitaki Africa ambayo imedorolesha akili ikitegeme a marekan ,China na ufaransa au misaada ya benki ya dunia....

Ebu niambie ni nchi gan ambayo imeendelea kutokana na misaa

Asia (3tigers of Asia)
Taiwan,south korea ,singapore
Au nyinginezo China ,japan


Europe
Uk,France, German,

Middle East
Israel,UAE, QATAR,
Waweza jitajia halafu utuambie huo ujinga unaodhan utatusaidia 5O years wametusaidia bado tukawa still the poorest country in the world

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom