Rais Magufuli: Aliyetangaza ugonjwa wa ZIKA nchini alikuwa anatumika na ndiyo maana nilipomfukuza, waliomtuma wakamteua kuwa Mkurugenzi

Unajivunia mtu mzushi. Ambae anatumika kuharibu hali ya hewa. Au kwa sababu ni hampendi magufuli. Mtu anakuzushia alafu umpende kweli? chuckie mbaya sana.
Mkuki kwa kunguruwe.
Wewe nichukie mimi nisichukie anaenifanyia tofauti.
Baada ya Dr Mwele kuondoka mbona ubalozi wa Marekani ili tanga za tahadhari ya Tanzania kuficha taarifa za maambukizi ya Ebola?
 
Uzalendo ni kitu cha msingi Sana, ni wazi kabisa Dr Mwele alitumiwa na wasioitakia mema nchi yetu kuichafua. Utaichafuaje nchi ya Baba na Mama yako kisa umepewa pesa au umeahidiwa cheo mahali?

Nani aliwahi kumuona mgonjwa wa zika? Alichokifanya Dr Mwele ni usaliti kwa nchi yake/yetu ambao ulilenga kuitia doa nchi ili kuharibu uchumi wake ili tuendelee kuwa tegemezi kwa wazungu na kukubali masharti ya kishetani kama ushoga.

Dr Mwele anapaswa atubu kwa Mwenyezi Mungu na atuombe radhi Watanzania kwa kitendo alichokifanya.Tanzania itajengwa na Watanzania wenyewe,maslahi ya nchi kwanza.
 
Walimfukuza yule mama kwa kumuonea tu na Mungu amemlipa zaidi.

Moyo wa rais wetu umejaa chuki na visasi visivyo na maana.
Unadhani huyo mdada an amani moyoni kufukuzwa na kuambiwa na mkuu wa nchi kuwa she was a mole
 
Hao waliomtuma na wakamteua baada ya kufukuzwa na ndio wanaotuonea wivu, tunawaomba pesa watusaidie kwa ajili ya CoRONA. Kweli za kuambiwa changanya na zako.
 
Yapo mambo unayoweza kuficha lakini sio ugonjwa, Zika ilikua inasambazwa sana na mbu, ikumbukwe ugonjwa unaoitesa nchi yetu miaka nenda rudi ni malaria kutokana na hali ya hewa na kimazingira inyasapoti mbu wengi kuzaliana. Ikiwa mbu ndo inasambaza zika unadhani rais angeficha idadi kubwa ya wagonjwa wa zika? Huku mtaani Buguruni tungeona wagonjwa wengi wasio wa kawaida.

Ugonjwa wa zika ulikua unasambaa sana duniani kipindi kile, kwa spidi ile kama ulikuepo nchini ni lazima tungeona dalili hata sie tusio wataalamu.

Kuhusu ugonjwa wa covid 19 na rais kuficha data pia ni hisia za watu tu. Kuna kipindi wagonjwa walifika mpaka 190, kama serikali ingekua na nia ya kuficha isingetangaza hata hyo idadi kubwa ya watu 190. Serikali iliamua kutotangaza updates za kila siku kwa sababu iliwaongezea wananchi hofu kuliko uhalisia.

Wakubwa huko nje wanaposema "maiti zitatapakaa mitaani" alafu serikali kila siku inatangaza idadi ya watu kuumwa, kisaikolojia unatengeneza nchi ya aina gani? Hata hao wanaotangaza wengine wameacha, mfano uganda na suala la muda tu kila nchi itaacha kutangaza na korona itakuepo kwa miaka kadhaa ijayo.

Wazungu hawakupi kazi kubwa na nzuri hivi hivi tu, ni watu wa masilahi muda wote ni hizi nchi zetu za dunia ya 3 ndo sehemu yao ya kufanyia mazoezi. Siamini rais anamchukia dr Mwele.
 
Taasisi ilifanya utafiti nchi nzima wakaona kuna viashiria vya uwepo wa ugonjwa huo.

Sasa wewe nani unayepinga utafiti kwa porojo ?
Umezoea umbea? Nimeuliza kama ilikuepo, nani aliugua zika? Au ndio yale maiti zitasambaa mitaani? Mtoto yupi wewe ulimuona kazaliwa na mapungufu sababu ikiwa zika?
 
Imagine ladies, boyfriend kakuacha, anajitapa kwa wenzakwe kakufumania ame ku-dampu"

Unajua kakusingizia ila hujitetei, instead you move on!

Baada ya miaka mitatu , Mwanaume huyo bado tu anazungumzia hiyo stori ya kuachwa kwa watu wale wale alio-wahadithia ; Wewe upo na mwenza mwengine umetulia unakula mema ya nchi, "Shida ya Jamaa ni nini?
 
Shida ni wewe
aah "sizitaki mbichi hizi" kwamba huyu mwanaume alitaraji atapigiwa magoti kuanzia IFM mpaka pale kwake kama walivyofanya akina nanii lakini hola badala yake mwanamke yupo na mabeberu huko Uswisi anakula raha na mwanaume wake mpya?
 
Si vibaya kutolea mfano, Magufuli kafanya mbaya gani kutolea mfano huyo mama kuonyesha hujuma katika magonjwa???
 
Baada ya Dr Mwele kuondoka mbona ubalozi wa Marekani ili tanga za tahadhari ya Tanzania kuficha taarifa za maambukizi ya Ebola?
Kuhusu Zika je?
Na kuhusu Ebola ni madhara gani yalionekana. Au ni invinsible. Maana kama wamarekani ni wakweli na hizo tuhuma zao. Sidhani kama madhara ya huo ugojwa yasingeobekana maana si rahisi kufichika sababu hakuna tahadhari yoyote so ni wengi wangeathiriwa na tungeona.

Kwa mantiki hio basi kuwa ulikuwa ni uzishi. Au Tanzania ina uwezo mkubwa wa kudhibiri magonjwa ya mlipuko. Mbona kikitokea kipindupindu wanatangaza na magojwa mengine vilevile kama ilivyo Corona.

Ni hakika kwamba kuna watu wanatumikia matumbo yao. Huyo mama hakuwa na lengo zuri na Mungu kamuibua ni miaka kadhaa hayo magojwa walidai yapo Tz still hayajaonekana kwamba yaliondoka bila legacy yoyote.

Mnyonge mnyongeni haki yake mpeni.
 
Bahati mbaya ni 'Mgogo' , kwahiyo wagogo akina Ndugai wana nini? Kauli mbovu na ya kibaguzi kutoka kwa kiongozi mkuu.
 
siyo vibaya, hata kucheka picha ya magufuli idriss alifanya kosa gani?
Unacheka nini sasa?? Kuweni na adabu sio kila kitu kujifanya kuwa wa kwanza... Kwahiyo angecheka bila kujirekodi.... Asingetosheka???
 
Unacheka nini sasa?? Kuweni na adabu sio kila kitu kujifanya kuwa wa kwanza... Kwahiyo angecheka bila kujirekodi.... Asingetosheka???
angegawa mapapai barabarani bila kuonyeshwa kwa TV isingetosha?
Angeenda kanisani na kuongea na washirika bila kutulazimisha na sisi waislamu kumuangalia huko kanisaini isingetosha?
 
Huyu mzee ana obsession ya ajabu na huyu mwanamama. Labda alitaka amfungulie mashtaka, kinachouma ni kumkosa.
 
Kwan haya mambo si yalishapita, kila mtu afanye yake, ni aibu sana kuwa mtu wa mipasho mipasho, afungue bendi ya taarabu basi tujue moja
 
Sasa na yeye lazima amtaje mtu,utafikiria alikuwa mke mwenzio zamani nilijua wanawake wana shida kumbe siku hizi wanawake wanaafadhali aisee karibu tutaiongiza dunia kama tutaendelea kuzaa wavulana na sio wanaume.
Shida ni kwamba hamjui nguvu ya upinzani anayokutana nayo Rais Magufuli kwenye vita ya kiuchumi,ushangai hadi leo ulaya nzima huko hadi mashuleni wanaambiwa mlima kilimanjaro upo kenya.sasa wewe nadhani kwa upeo wako mdogo hili jambo unalichukulia kawaida tu.
 
Dr Mwele yuko juu kileleni

wakati stone alitarajia angekuwa amechacha akikesha Mitaani akijiuza
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…