Rais ni mtu mkubwa sana na ana njia nyingi za kupata information kuliko sisi raia na kwa mantiki sitaki kuyapuuza matamshi ya Raisi ila nina maswali machache.
Je Mwele alikuwa anatangaza ugonjwa upya aua alikuwa anatoa findings za utafiti uliofanyika?(mwenye clip ya press conference ile atuwekee)
La pili,kwa uelewa wangu mdogo ni kuwa kupata internationa job kama ya Mwele ni lazima serikali iridhie kama bado ana uraia wa Tanzania.Sijasikia Mwele kuukana Utanzania wake na maana yake ni kuwa ni raia wa Tanzania anayefanya kazi WHO.Kama hivyo ndivyo kwa nini serikali isondoe vetting yake kwa mtu "mbaya" kama huyu?
Je ni kutangaza kuhusu baadhi ya sampuli za damu kuna na dalili za virusi vya Zika ndizo zinampandisha hasira Mzee kila wakati au kuna jingine?(Mwele alikuwa mtia nia 2015)
Nitakupa majibu sahihi hapa hapa.
Dr.Mwele Malecela alitangaza nini?
Dr. Mwele Malecela alitangaza matokeo ya utafiti uliofanywa na wataalamu kadhaa wa afya kutoka hospitali kadhaa hapa Tanzania wakishirikiana na NIMR. Dr.Mwele hakutangaza mlipuko wa homa Zika hapa Tanzania bali alitangaza matokeo ya awali ya utafiti wa kisayansi, uliofanyika kwa miaka isiyopungua mitatu. Utafiti ule haukufanywa na Dr. Mwele Malecela, bali yeye kama mkurugenzi mkuu wa NIMR aliongea na waandishi wa habari kutangaza matokeo yale kwa sababu ya uzito na umuhimu wa utafiti ule. (Kifupi sana, wakurugenzi wa taasisi za kitafiti duniani hufanya vile ili kuongeza thamani ya taasisi wanazoziongoza kwa kutumia tafiti maana watu wengi watahamasika kuusoma huo utafiti au kuutumia kama rejea katika kazi zao za kitafiti, kitaaluma na kikazi). Yote kwa yote, utafiti ule tayari ulikuwa umechapishwa kidunia (Published) hivyo hata Mwele Malecela asingetangaza bado dunia ingejua. Pia tusisahau, hatua zote za wizara zilifuatwa kabla ya kufanyika utafiti ule, wizara ikatenga pesa za kufanya ule utafiti, na uongozi nzima wa wizara ilikuwa bega kwa bega na NIMR mpaka matokeo ya utafiti yalipotangazwa kwa umma.
Utafiti ulihusu nini?
Utafiti ulichunguza wakina mama waliojifungua watoto wenye vichwa vidogo ikiwa kama walikuwa wamepata maambukizi ya Zika kabla ya kujifungua watoto. Na sampuli za damu zilizopimwa zilileta matokeo yalionyesha idadi kubwa miongoni mwa hao wakina mama ni kweli walikuwa na maambukizi ya Zika.
Nini lilikuwa kosa la Dr. Mwele Malecela?
Hakuna kosa lolote kisheria, kisayansi au kitafiti ambalo alilifanya Dr.Mwele Melecela. Kosa pekee alilolifanya lilikuwa katika mlengo wa kisiasa. Yaani Rais hakupendezwa na kutangazwa hadharani matokeo ya utafiti ule hivyo Dr.Mwele Malecella akaadhibiwa kisiasa kwa kufukuzwa kazi. Kitu pekee ambacho Rais hakijui (hataki kukikubali?) ni kuwa, Utafiti ni mali ya jamii na sio mali ya mtu, hivyo kufanya utafiti wowote na kuficha matokeo au kuchakachua matokeo ni kosa kubwa kisayansi au kitafiti.
Kwa kumalizia tu ni kuwa tunapaswa kufahamu kuwa Utafiti hupingwa kwa utafiti, Dr.Mwele aliongea kwa kutumia utafiti na wanaotaka kumpinga waje na utafiti, tuache tafiti zipingane zenyewe.