Rais Magufuli: Aliyetangaza ugonjwa wa ZIKA nchini alikuwa anatumika na ndiyo maana nilipomfukuza, waliomtuma wakamteua kuwa Mkurugenzi

Rais Magufuli: Aliyetangaza ugonjwa wa ZIKA nchini alikuwa anatumika na ndiyo maana nilipomfukuza, waliomtuma wakamteua kuwa Mkurugenzi

Walimfukuza yule mama kwa kumuonea tu na Mungu amemlipa zaidi.

Moyo wa rais wetu umejaa chuki na visasi visivyo na maana.
Kabisa yaani ana roho ya ajabu sana,anaonekana aliumia Huyu mama kupata hicho cheo,lkn pia unashangaa eti anajiweka karibu na mzee Malechela tena bila haibu jamani muogopeni mungu
 
Apande tu huko watanzania hatumhitaji magonjwa ya mlipuko waziri wa afya ndie mwenye dhamana yeye akajiibukia tu na Zika yake hewa .Kuwa mtaalamu sio kuwa mwongo.

Aende kuwaongopea wazungu
Watanzania gani,labda mambumbumbu kama wewe
 
Na kuna mwingine anatumiwa na Mabeberu yupo Ulaya kutaka kuharibu amani ya Nchi yetu
Wewe na babu yako mnafanana, mnafuruhia kuona watu kuteseka!!
Watanzani sio watu wa roho mbaya sijui nyinyi mmetokea nchi gani!!
 
Wizara ina msemaji wake...alipaswa km aliona kuna haja ya kutangaza angepeleka kwa waziri.
Ugonjwa ni vita km vita ingine...imagine batalian ya kwanza ilivyoteketea vita vya uganda halafu jamaa angekuja tbc kusema aisee batalian nzima imekufa inabid tujipange... unadhani nyerere angechukua hatua gani?
Kuna msemaji wa wizara na msemaji wa serikali ..mganga mkuu wa serikali nk waPelekee huko ww ushakabidhi finding zako kutangaza haikuhusu... wangapi wanafuatwa na waandishi wanajibu wao sio wasemaje wa ofisi.
Km sampuli ilichukuliwa kimya kimya basi wagonjwa muwatibu kimya kimya..km mliwapata kliniki za mama waja wazito ilipaswa mrudi kule kule.
Kwani mradi wa chakula bora miaka ya 80 si ilikua finding walitangaza au serikali ilichukua hatua?
Inawezekana jambo ni fact lakini si kila ukijuacho lazima useme...njia bora kujua pa kusemea na wakati wa kusemea.
Kwa nafasi ya mkuu wa nimr umekuwa vetted hata vikao vya siri vya serikali vyaa mienendo ya afya unahudhuria why you do things like you are nothing wakati unajijuwa you are someone in inner core?
Kutaja mgogo inawezekana ni mtani wake ila pia kwenye kitabu cha uongozi wetu na hatma ya tanzania kuna mtu alikosa kitu mambo ya sirini akayafanya uwazi na ya uwazi akayafanya sirini kamati ikala kichwa.
Kuna namna nyingi ya kutumika eiza moja kwa moja au indirect..
Rejea kesi ya yule shushushu alikamatwa na barua kuhusu nyerere na vita vya ukombozi ambaye alikua pia dereva teksi na mfanyakazi wa hoteli kubwa jijin enzi hizo.
Kuna namna nyingi za kupewa zawadi au pole au pongezi na mwingine anakupa zawadi si kwamba anakuitaji sana ila anataka kumkomoa aliekuacha.
Sijafurahi kutangazwa hadharani ila sijaridhishwa dr alivyo itendea fani yake ...mfano yule mkuu wa taasidi ya takwimu sijui dr chuwa (sina uhakika) bongo...umemuona mara ngapi akitangaza takwimu au hajui taarifa halisi na za kupika?
 


Rais Magufuli amenukuliwa akisema haya..

Wakati tunaingia madarakani tuliambiwa Tanzania kuna ugonjwa wa Zika, aliyetangaza na aliyetumiwa kutangaza nikamfukuza kazi (bahati mbaya ni Mgogo); Baada ya kumfukuza yule Mgogo aliyesema Tanzania kuna Zika na waliomtuma wakamteua kuwa Mkurugenzi, mpaka leo miaka karibu mitano hapajawahi kuwa na kesi hata moja ya Zika hapa Tanzania.

Baada ya uzushi wa Zika kupita na kumfukuza kazi aliyesema kuna ugonjwa huo, tukakaa baadaye tukaambiwa kuna Ebola, walijua wakisema tuna Ebola Watalii hawatokuja, tukasema sisi hatuna Ebola wala Mjukuu au hawara yake Ebola, hatujaona Ebola wala nani amekufa kwa Ebola hapa Tanzania.


Pia soma
1. Rais atengua uteuzi wa Mkurugenzi NIMR Dkt. Mwele Malecela

2. Dkt. Mwele Malecela aula Umoja wa Mataifa. Kuongoza vituo vya magonjwa Afrika

3. Safari itasonga Kwa msaada wa Mungu: Dr. Mwele Malecela

4. NIMR: Asilimia 45 ya watoto wachanga wakutwa na Virusi vya homa ya ZIKA Tanzania

mtoto wa watu na tabasamu kama lote, Mungu akupe miaka minhi huku wasio kupenda , tena hasa wa jinsia nyingine washuhudie ukizidi kupaa
 
Huyu ni mtoto wa Mzee John Samwel Malecella Waziri Mkuu mara mbili wa JMT na Makamu Mwenyekiti CCM Taifa mstaafu. Sio mtu mwepesi kama wanavyomchukulia
Waziri Mkuu mara mbili? Lini na lini? Nchi hii waliowahi kuwa Mawaziri wakuu mara mbili ni David Msuya na Edward Moringe Sokoine!
 
Back
Top Bottom