Rais Magufuli amchenjia Makonda?

Rais Magufuli amchenjia Makonda?

Nyani Ngabu

Platinum Member
Joined
May 15, 2006
Posts
94,296
Reaction score
122,540
Rais Magufuli leo kasema, kama Makonda alizitumia fedha za TASAF, basi na azirudishe.

Vilisikika vicheko hafifu na vya chinichini baada ya Rais kusema hivyo.

Kamera nazo zikamwonyesha Makonda, aliyekuwa kakaa mbele pamoja na viongozi wengine, akitabasamu kana kwamba hana wasiwasi wowote. Yaani hakuna baya litalomtokea [sababu yaweza kuwa ni kwa sababu hakuzitumia kabisa hizo hela, au, alizitumia lakini anajua kuwa Rais hatomfanya chochote, n.k.]

Kamera pia ziliwaonyesha marais wastaafu wote watatu.

Kwa kuwasoma lugha yao ya mwili, ni kama vile walikuwa ‘embarrassed’ na alichokisema rais.

Ni kweli Rais Magufuli alimaanisha alichokisema au kasema vile ili kuonyesha tu kuwa ‘hampendelei’ Makonda?

Binafsi naona kama vile kasema tu ili kuonyesha ‘hampendelei’ jamaa huku kiuhalisia hakuna lolote atalomfanya maana jamaa ana madhambi mengi na makubwa kuliko hilo la kutumia fedha za TASAF.

Bofya video umsikie Rais alivyosema kuhusu Makonda. Kuanzia dakika ya kwanza hadi ya pili.

 
Ni hivi hizo pesa za TASAF ni enzi ya Mkapa,Makonda alikuwa hohehahe hivyo akasaidiwa.Hizo pesa ilikuwa ni halali kwake kabisa ukilinganisha na mission za TASAF.Akipenda atarudisha tu maana kwa sasa ana uwezo.
 
Hizi lugha kuzipambanua ni ngumu...fedha kuna wakati zikichukuliwa kuna mwanya wa kurudisha? ni wakati gani hasa inaitwa ''zimeibwa''....je ni pale Mchukuaji anapokuwa na mahusiano ya karibu na mkemeaji??
 
Hizi lugha kuzipambanua ni ngumu...fedha kuna wakati zikichukuliwa kuna mwanya wa kurudisha? ni wakati gani hasa inaitwa ''zimeibwa''....je ni pale Mchukuaji anapokuwa na mahusiano ya karibu na mkemeaji??
Toa mfano ili ueleweke bwashee!
 
Back
Top Bottom