Shida mnashindwa kujua Yote unayoyaona saizi yanatoka kwenye BAJETI YA AWAMU YA TANO. Ukisoma Ilani ya CCM 2015/20 iko wazi kabisa. Kuna miradi inatakiwa kumaliziwa, Kuendelezwa na kuanzishwa.
Sasa wewe ukisema REA kafanya JK sijui kama unataka kusema Jk alipotoka madarakan aliacha hela za kuhakikisha vijiji vyote vinapata umeme hata kama ni hadi 2050.JK kaacha Ujenzi wa Kinyerezi 1 na Jpm kaja kaendeleza kinyerezi 2,wewe ukija na hoja za kinyerezi ni mradi wa JK na JPM hana alichofanya sijui kama unakua na logic. JK kaacha mipango ya SGR,hajaacha hata sent na ilikua iwe mchina lkn JPM kampa mturuki, Reli inajengwa unakuja kusema ni kazi ya Jk na JPM hakuna anachotaka. Hivi huyo Jk toka alipoondoka 2015,haya yote yanayofanyika yeye ndio director?
Mradi wa Bagamoyo ulianzishwa na JK lkn JPM kaja kaupiga chini,kwanini hatuoni kuwa ktk miradi iliyoasisiwa na JK,JPM ananguvu nayo?Nilifuatilia uzinduzi wa hospital ya mloganzila Jk aliacha hatua ndogo sana pamoja na pesa ya mradi, lkn JPM kama Ilani ilivyosema kuwa anatakiwa akamilishe huo mradi tunaona fungu la kukamilisha hiyo hospital lilitoka kwenye bajeti yake.Leo unakuja unasema Jpm hospital ya mloganzila haimuhusu, ni Jk. Uko serious au unafanya SIASA UCHWARA?
Unajua mradi wa REA ulikua ukwame baada ya msaada wa 900B kupigwa chini 2016?Lkn je umekwama?Leo unaendelea kama kawaida, unasema mradi ni wa JK na JPM hana lolote. Are u serious?Miradi mingapi huwa inaishia kwenye makaratasi?Miradi mingapi huwa inakwama na mingine kwenda mwendo wa konokono?Kwamba mlitaka JPM aje apige chini terminal 3,apige chini mloganzila, barabara ambazo hazijaisha aachane nazo naye aanze zake, SGR apige chini au REA apige chini?Nini maana ya mipango ya serikali Kama kila kiongoz ili aonekane kafanya kazi lzm aje na mipango mipya?
Mtanzania wewe umesema vema,lakini napata maswali magumu kweli mnapofafanua haya mambo.
1.Umeme wa REA ulipaswa kupigwa chini baada ya kukosekana fedha za WB 2016,kwanini tunakopa hizo pesa wakati tayari kwa kitambo kirefu kulikuwa na tozo kwenye mafuta na umeme kwa ajili ya kukamilisha hiyo miradi?
2.Ujenzi wa bandari bagamoyo,uliafikiwa na serikali ya awamu ya nne,na kutengewa bajeti kuoitia bunge la JMT, na Mh.JPM alikuwa waziri wa ujenzi alisimamia ujenzi wa bandari hiyo hiyo, Ni nini kimefanya mradi aliousimamia kupigwa chini?(ametoa sababu kadhaa zilizipelekea kutupiliwa mbali kwa mradi ambazo nyingi zimeelekezwa kwenye MKATABA, swali ni je,wakati wa kuupitisha mradi huo yeye akiwa waziri,hakuona mkataba?)
3.Kila serikali kuja na mradi wake, ni swala lenye ukakasi,ni muhimu kuzingatia mipango mikakati ya kitaifa katika kuifanya nchi iendelee, lakini tukiangalia moango wa maendeleo ya uzalishaji nishati nchini STIEGLER'S GORGE haikuwepo kabisa,tulikuwa na mkakati mkubwa wa kuzalisha umeme utokanao na gesi,tukaamua kujenga bomba la kusafirishia gesi kutoka Mtwara kuja Dsm,tuliweka pesa nyingi kukamilisha mradi ule,watu waliumizwa sana kuhakikisha hilo linakamilika,lakini leo tumeanzisha mradi mpya kwa gharama mpya,pasipo kuelezwa gharama za mradi wa ujenzi wa bomba ni sh.ngapi, na zitarudishwaje?
4.Mradi huu wa umeme wa maji (stiegler's),kama nakosea naomba nirekebishwe,kwamba utafikia kilele cha uzalishaji wa MW 2150 itakapofika mwaka 2036, je,baaday ya 2020 au 2025 akiondoka JPM,mradi huu utaendelea kutekelezwa mpaka kufikia kilele cha uzalishaji? Au atakayefuata baada yake atakuja na mipango mingine kutuacha tuendelee kulipa deni la mradi uliozimika kama tunavyolipa deni la ujenzi wa bomba la gesi?
5.Fact zote za kusitishwa kwa baadhi ya miradi mikubwa imejengwa katika misingi ya MIKATABA, je, mikataba ya inayosainiwa sasa kama vile ununuzi wa ndege,ujenzi wa reli,Stiegler's gorge HPP tunaijua? Haitaleta taabu tena baadaye? Au tunapaswa kusubiri aondoke kwanza madarakani ndipo tuje tuambiwe udhaifu wa mikataba hiyo na atakayechukua nafasi kwa wakati huo?
Naomba kumalizia kwa kusema,katika kipengele cha mikataba pana mapungufu makubwa ambayo tukiendelea kuifuga itaendelwa kututia umasikini kwa miongo mingi sana ijayo.