MISULI
JF-Expert Member
- Jan 15, 2014
- 7,843
- 5,476
Kama wewe mjanja kwanini utumie fake ID kumuogopa MSHAMBA?Kwanza inakuaje unaongozwa na MSHAMBA?Mkuu fake ID zilianza enzi za awamu ya tano!?
Sent using Jamii Forums mobile app
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Kama wewe mjanja kwanini utumie fake ID kumuogopa MSHAMBA?Kwanza inakuaje unaongozwa na MSHAMBA?Mkuu fake ID zilianza enzi za awamu ya tano!?
Kama wewe mjanja kwanini utumie fake ID kumuogopa MSHAMBA?Kwanza inakuaje unaongozwa na MSHAMBA?
Sent using Jamii Forums mobile app
Hela ya Mloganzila na SGR katafuta nani?Mradi wa REA ungekufa, lawama zingekua kwake ila umefanikiwa sifa ni kwa Jk. Huoni unashida ya akili sehemu?Unataka kusema mradi wenye timeframe ya miaka 5,pesa tayari zinakua zimetengwa na kilichobaki ni kutekeleza tu?Kama jibu ni ndio,hii miradi inayokua inakwama au kusuasua shida huwa nini ukitoa mattz ya mkandarasi?Kama jibu ni HAPANA, Huoni utawala unaokuwepo huwa na mkono wake ktk huo mradi?Kuendeleza siyo vibaya, ni jukumu kuendeleza Mazuri ambayo "wenzie" wamemuanzishia, ndiyo maana ya serikali, ni uendelevu wa mipango. Kama REA ingekwama basi hilo lilikuwa lake maana 2016 raisi alikuwa yeye
Kuhusu Hospitali ya Mloganzila, JK aliondoka madarakani 2015 kwa hiyo timeframe ya mradi ilikuwa lazima imkute raisi mwingine, hata ungekuwa wewe ndo raisi ungemalizia tu si kila kitu kipo, fedha imeshatafutwa shida ni kazi iendelee kufanyika
Sasa sisi tunachosema ni kwamba, Msitusumbue sana na Kelele za anajenga hiki, anajenga kile as if miradi kaibuni yeye na kaitafutia pesa yeye huko nje!. Mbona waliovianzisha hawakuwa na kelele saana kama sasa hivi?
Maana hiyo SGR na Stiegles haijafika hata nusu ya kazi lakini kelele nyingi utadhani mmeshakamilisha!
Haya yataendelea kuwa mwiba kwa majuha wa kitanzania wenye chuki binafsi na mpendwa rais wetu Magu na serikali yetu!Rais wetu John pombe Magufuli ameamua Nchi iende Mbele... hii ndio kusema Chagua Magufuli Kazi iendelee
1. Ujenzi wa barabara Nchi Nzima kwa gharama Sh. Trilioni 5.3 ili kurahisisha usafiri wa watu na mizigo ya biashara kutoka sehemu moja kwenda nyingine.....
2. Ununuzi Ndege Mpya Sh. Trillioni 1.3 ili kuchochea sekta ya Utalii na Biashara ya ndani ya nchi yetu....
3.Ujenzi wa Hospital za wilaya 67 Wakati tangu tupate Uhuru hadi Leo tulikuwa na hospital 77 za wilaya, vituo vya Afya Sh.Bilioni 321
4.Kufufua Mradi wa kuzalisha Umeme MTO Rufiji Sh.Trilioni 6.5 utakaozalisha MW 2100 Wakati tangu tupate Uhuru hadi Leo hii tunazalisha MW 1500 za Umeme tu......
5. Ujenzi wa reli ya kisasa (Standard Gauge) Sh. Trillioni 7 baada ya kukaa na reli ya mkoloni tuliyorithi zaidi ya miaka 200 iliyopita.....
6. Mikopo kwa Wanafunzi wa Elimu ya juu 2015-2019 Sh. Trilioni 1.6
7. Elimu Msingi bila malipo (Elimu Bure) kwa Shule za Msingi hadi kidato cha nne sh. Bilioni 945.9
8.Ukarabati Shule kongwe 62, Ujenzi wa Maabara, nyumba za Walimu kwa Sh. Bilioni 308
9.Ukarabati Viwanja vya Ndege Nchi Nzima Sh. Trilioni 1.8
10. Ujenzi wa meli Mpya na ukarabati za Mv Victoria na Mv Butiama katika Ziwa Victoria Sh. Bilioni 152,
Ujenzi wa meli Mbili Ziwa Tanganyika meli ya mizigo na Abiria MV Liemba, Ujenzi wa meli Mbili za Abiria na Mizigo Ziwa Nyasa MV Ruvuma na MV Njombe Umekamilika.....
11. Miradi ya Usambazaji Umeme vijijini kupitia Rea Umeme unaendelea kuchomoza vijijini....
12. Upanuzi wa Bandari ya Mtwara kwa kiwango kikubwa, Bandari ya Tanga, Bandari ya Dar es salaam
13 Ununuzi wa vivuko vya Majini maeneo mbalimbali ili kurahisisha usafiri wa watu na mizigo ya biashara......
14. Ujenzi wa madaraja mfano Mfugale, Ubungo interchange, Surrender bridge n.k
15. Miradi ya Maji inayoendelea Kujengwa Maeneo Mbalimbali ya Nchi yetu ni mapinduzi kwenye sekta ya Maji......
N.K N.K N.K
We are proud of you, our president Honorable John Pombe Magufuli.....
Naungana na Mwenyekiti wangu wa Vijana Taifa Comrade kheri James kuwa yoyote anaempinga Rais wetu kwa haya anayofanya kwa Mustakbari wa Taifa letu kuna mambo mawili kwa mtu huyu either ni Chizi au Mkimbizi nchini kwetu........
Fahami Matsawili
Mjumbe wa baraza kuu Uvccm Taifa..
Mtanzania wewe umesema vema,lakini napata maswali magumu kweli mnapofafanua haya mambo.Shida mnashindwa kujua Yote unayoyaona saizi yanatoka kwenye BAJETI YA AWAMU YA TANO. Ukisoma Ilani ya CCM 2015/20 iko wazi kabisa. Kuna miradi inatakiwa kumaliziwa, Kuendelezwa na kuanzishwa.
Sasa wewe ukisema REA kafanya JK sijui kama unataka kusema Jk alipotoka madarakan aliacha hela za kuhakikisha vijiji vyote vinapata umeme hata kama ni hadi 2050.JK kaacha Ujenzi wa Kinyerezi 1 na Jpm kaja kaendeleza kinyerezi 2,wewe ukija na hoja za kinyerezi ni mradi wa JK na JPM hana alichofanya sijui kama unakua na logic. JK kaacha mipango ya SGR,hajaacha hata sent na ilikua iwe mchina lkn JPM kampa mturuki, Reli inajengwa unakuja kusema ni kazi ya Jk na JPM hakuna anachotaka. Hivi huyo Jk toka alipoondoka 2015,haya yote yanayofanyika yeye ndio director?
Mradi wa Bagamoyo ulianzishwa na JK lkn JPM kaja kaupiga chini,kwanini hatuoni kuwa ktk miradi iliyoasisiwa na JK,JPM ananguvu nayo?Nilifuatilia uzinduzi wa hospital ya mloganzila Jk aliacha hatua ndogo sana pamoja na pesa ya mradi, lkn JPM kama Ilani ilivyosema kuwa anatakiwa akamilishe huo mradi tunaona fungu la kukamilisha hiyo hospital lilitoka kwenye bajeti yake.Leo unakuja unasema Jpm hospital ya mloganzila haimuhusu, ni Jk. Uko serious au unafanya SIASA UCHWARA?
Unajua mradi wa REA ulikua ukwame baada ya msaada wa 900B kupigwa chini 2016?Lkn je umekwama?Leo unaendelea kama kawaida, unasema mradi ni wa JK na JPM hana lolote. Are u serious?Miradi mingapi huwa inaishia kwenye makaratasi?Miradi mingapi huwa inakwama na mingine kwenda mwendo wa konokono?Kwamba mlitaka JPM aje apige chini terminal 3,apige chini mloganzila, barabara ambazo hazijaisha aachane nazo naye aanze zake, SGR apige chini au REA apige chini?Nini maana ya mipango ya serikali Kama kila kiongoz ili aonekane kafanya kazi lzm aje na mipango mipya?
Fahami Matsawili tuheshimu kazi za wengine,unataka kusema enzi za Jk wajanja wachache ndo walikuwa wanaamua? ( any way nikubaliane na wewe kwa hilo) unaweza kutuambia hapa kwamba kwa sasa nchi ipo mikononi mwa wengi?Waambie Comrade nchi ilikuwa mikononi mwa wajanja wachache wao ndio wamuaji na wanufaikaji wa rasirimali za Taifa Leo hali imebadirika Taifa letu limesimama katika misingi yake